Wenye majina ya watu walioweka fedha uswisi wawataje - Mkuchika!

Nadhani hii ni tabia ya serikali ya ccm, na hasa ukizingatia walioweka hizo pesa ni vigogo wa ccm
 
serikali isitufanye wananchi hatuna akili kwa sababu yenyewe inawafahamu.(kama MEMBE anawafahamu na membe ni waziri hivyo serikali inawafahamu).
 
Taarifa ya habari waziri Mkuchika anasema mwenye majina ya watu wenye fedha Uswiss wampelekee na kahaidi kutowataja kuwa wamempatia majina hayo kala kiapo cha kutunza siri.

Hivi kweli amefikiri kabla ya kuongea au au ndio media aonekane kaongea nae? maana waziri Mh. Membe alisema majina wanayo na yeye kama anataka kushughurikia maadili si amfate Membe amwombe majina tu?

Me nadhani angesema kwenye media majina nimeshamuomba Benard Membe hivyo nayashughulikia.........
 
Ni kero kubwa sana kuwa na viongozi wanaoropoka. Sikutegemea nilichosikia ktk taarifa ya jana. Wao ndio serikali na wao ndio wanatakiwa wafuatlie watuambie ni nani hao walioweka pesa nje na walizipataje.

Wanapiga chenga kwa vile ni wenzao? Ngoja upinzani uchukue 2015 tuone watakimbilia wapi?

Wasipofanya kazi yao hilo litakuwa ni mtaji kwa wapinzani ktk kampeni za 2015. Hich kilichopo tule wote. Dunia hii twapita.
 
wezi wakubwa hawa tutawaondoa kwa nguvu ya watu yaani ''peoples power'' siku zao zinahesabika
 
[h=1][/h]




mkuchika.jpg


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika
Source:Mwananchi 20/11/2012

"SERIKALI ya Uswisi imeitaka Tanzania kuwasilisha kwake majina ya watu wanaotuhumiwa kuficha mabilioni ya fedha nchini humo, kama sharti la kusaidia uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika amesema suala la kuwasilisha majina ya watuhumiwa ndilo sharti pekee ambalo Uswisi wametoa na kwamba ndiyo sababu
Serikali imekuwa ikitaka wanaofahamu majina ya watuhumiwa hao wayataje."


Wakuu mimi nimepata kugugumizi na kisebusebu cha kuielewa habari hii kulingana na tamko la Waziri Mkuchika.

Sitarajii kuwa inabidi serikali itegemee habari toka kwa watonyaji huku yenyewe imeweka mikoni kifuani kama jamaa asiyehusika wala kujua kiachoendelea!

Msimamo huu hauelekei kuwepo na nia ya dhati ya kutatua tatizo hili la ufisadi na utoroshwaji wa fedha za watanzania na kuzificha nje ya nchi.

Siyo siri Waswissi ni vinara wa kupokea fedha za rushwa dunia nzima na imekuwa ikifaidika na utunzaji wa heka chafu. Mchezo huu hawakuanza jana wala juzi, ni msimamo wao waliojiwekea kwa miaka mingi sana.
Kama ambavyo benki ingependa uwekezaji wa amana nao Waswissi wamekuwa waki encourage mafisadi kuweka fedha huko.

Msimamo huu wa maneno matupu kwa uhakika unanitia wasi wasi kama kuna nia njema katika kuwachukulia hatua mafisadi hao, wengine amba inasemekana ni watumishi wa umma na wnasiasa.

Kama mikataba ya serikali, mingine ambayo tunaambiwa ni ya "siri", watu wanafaidika nayo, na serikali haina habari, hapo nafikiri kodi tunazokatwa au kuto serikalini hazifanyi kazi inayotarajiwa-yaani kulinda mali ya umma.

Mimi mmoja wa watu naamini kuwa tamko la Mh Mkuchika ni la kutia ganzi tu na kupumbaza umma, na si kutata tatizo.
 
Huyu naona amechanganyikiwa! Hivi ni kazi ya nani kufatilia hayo majina? Ana msubilia nani amletee?

Kwani hajui hizo pesa zimetoroshwa na zina takiwa zirejeshwe!
 
Sasa mlango uko wazi,ebu tuingie ndani kuona maajabu ya kwanini sisi ni maskini ama kwanini sisi ni viwanda vya kutunga propaganda ili kujipatia umaarufu.
 
Sasa mlango uko wazi,ebu tuingie ndani kuona maajabu ya kwanini sisi ni maskini ama kwanini sisi ni viwanda vya kutunga propaganda ili kujipatia umaarufu usiokuwa na tija kwa taifa.na hapa ndipo tutakagundua ujasiri,uoga,hofu na udhaifu wa wanasiasa wa tanzania.
 
Hosea amesema wanataka watu woote wenye majina yao wampelekee ili waanze kuyashuhulikia, na hatua zichukuliwe.

Hapa naona wameanza kuweka vizuizi!
Huyu Mnyantuzu ananiudhi kweli yaani kazi yake anataka tumfanyie,mbona umbeya aliopeleka kwa balozi wa Marekani kumhusu aliyemteua hakusema tumpelekee .
 
Hii serikali inaongozwa na watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri;watz wenye mapenzi mema walitaja hadi akaunti namba ya Andrew Chenge kule visiwani ikionyesha katumbukiziwa dola milion 1.2 na mwenyewe Chenge kukiri kuwa hizo ni senti tu!

Jamaa yangu mchumi aliwahi niambia kuwa hata kama Chenge awe anaweka tu bank pesa zake za mshahara na marupurupu toka aanze kazi miaka ya 70's HAWEZI FIKIA kukusanya pesa nyingi kama hizo!Na kikubwa zaidi kuweka nje mabilion ya pesa inabidi uitaarifu BOT na Chenge hakufanya hivyo!

Chenge na Dr Rashid pamoja na ushahidi wote huo wapo uraiani,sasa mnataka mtz aseme nn zaidi?Acheni kutuona sisi majuha na your days are numbered!

Mkuchika umeshindwa uchaguzi majuzi na kijana asiyejulikana kabisa kwenye medani za kisiasa;Je hii siyo alarm kwako kama watu wamebadilika?
 
Back
Top Bottom