Wenye magari: Mnaibiwa sana kwenye petrol station

Wakuu,

Kutokana na vyuma kukaza na havina expansion joints nimekua makini sana kwenye kuweka mafuta kwenye gari.

Nikagundua kituo fulani fulani wanaiba sana, niliowa experience ni Oilcom Magomeni Kagera, Oilcom Ubungo mataa na Morroco pale niliweka mafuta Oilcom Magomeni Kagera kuna mdada anakitumbo kikubwa sana kaniibia kwakua anaibinya pump kupunguza outlet flow.

Hivyo hivyo Ubungo Oilcom na Morroco, sasa kuanzia leo, nilikifika filling station nashuka na ninamwambia aachie pump.

Ushauri wangu pia kwenu mkifika filling stations please hata kama unaweza mafuta ya 4000 shuka na akiset amount ya pesa mwambie aachie pump ijikate yenyewe, kumuacha aishike wanawaibia sana, mi nimepigwa three times.


Blue monday
Tembea na dumu
 
Wewe unaenda na corolla sijui passo ndiyo unalalamika unaibiwa kumbe gari yako mbovu inanyonya mafuta tumia kitu cha ESCALADE , LEXUS SUV, CHEVROLET , hutojuta kutembea na gari hii.....
 
Kwa iyo wakibana ndio inakuaje, maana mwisho si inaandika litres imeingia na amount umelipia

Pump inatumia upepo. Wakibana kidogo flow /kinachopita ni mafuta kidogo, upepeo/povu kwa wingi na mita inaendelea kusoma.

@Uwura Jamani mbele ya safari kama teknolojia ina ruhusu kannuni iagize pipe ziwe clear pipe ili mteja ajionee kinachoingia
 
Hapana hakuna wizi hapo kilichokuwa kinafanyika zamani ni kukubambikia bili ndogo ndogo zilizotangulia kwa kutorudisha vizuri mkono wa kujazia mafuta sehemu yake hivyo pump inakuwa imepause ikisubiri kubinywa tena ili iweze kuendelea,kumbuka pump ili iweze kufuta bili iliyotangulia lazima mkono wa kujazia uludiswe sehemu yake,lakini hilo tatizo sasa hivi TRA wamelikomesha baada ya kuwafungia auto efd machine ambayo inatoa risiti pindi mkono unaporudishwa sehemu yake,wewe unatakiwa kudai risiti yako tu.
 
Hakuna wizi kama huo labda ushauri n kwamba kabla hjaongea au kuwaharibia watu biashara jifunze kufanya uchunguz na kuuliza ...nmefanya hiyo kaz kwa zaidi ya mwaka mmoja kitendo hicho hakimaanishi kua mtu anaibiwa.uliza kabla hjatenda na kataa kuongozwa na fikira fupi.
 
Sawa,mi ndo nimeibiwa,nimekupa tahadhari tu,
Ni kweli huwa wanaiba ila kwa njia tofautofauti
Kulingana na uzoefu wa mtu binafsi, MIMI nilishawahi kuibiwa kwny kituo flani cha goba road,
Nanilikua makini kusoma price total na liters lkn baht nzuri gari ilizima mbl kdg ikabidi nirudi na wakajiridhisha kwl mafta hayakuingia na wakanipatia mengine baada ya mkwara mzito
Siku hz huwa naenda na geleni kabisa

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Kubana pump hakuwezi iba mafuta, kinachozungusha mahesabu ni floor ya mafuta kutoka, abane asibane kinachosoma ni mechanism ya mafuta, hauna point hapa!
kama hujui kitu ni bora ukanyamaza au ukauliza uelimishwe kuliko kubisha!!!!
 
Dawa ni kwenda na transparency bottles tu kujaza mafuta.

Nakumbuka kuna siku kuna sheli moja nlikwenda kutia mafuta, walikuwa na old style pumps sio digitai, ni zile namba zinazunguka. Ile mashine ilikuwa inafanyiwa maintainance. sasa wakati naekewa mafuta, zile namba zilikuwa zinazunguka kidog kidogo mpaka mhudumu akashtuka ikabidi amwite fundi. Fundi kuja, yaani nafikiri kakazua nati tu, basi huwe mwendo wa izo namba zinavozunguka utafikiri zinafukuzwa..... Ilikuwa ndio mwisho wangu kuingia kwenye icho kituo.
 
Back
Top Bottom