Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Nimecheka, nimehuzunika na nimewaza maisha ya utoto na uvulana. Kwa kweli kuna muda unatamani wakati urudi nyuma, ila haiwezekani. Nadhani watoto wa 80s na 90s tumepitia same parenting culture.

Mimi mzee wangu alikuwa Dingi na Mshua. Mshua kwa maana was a provider ila kwenye malezi alikuwa ni dingi.

Kuna visheria vya ukax sana. Mfano, sikukuu ilikuwa ni marufuku kutoka nje. Au nguo za sikukuu hakuwahi kutununulia. Alikuwa na falsafa kuwa ukizoea siku akikosa, itakuwa depressed.

Kipigo pia mzee katembeza sana.

Nakumbuka kuna siku weekend tunaenda kupanda maharage, asubuhi bimkubwa kapika uji. Jamaa tukagoma kunywa uji mkavu. Hatuna hili wala lile, mida ya saa 7 msosi kavu haujaja. Basi tukagonga maembe , tumerudi home, kumbe mzee aliambiwa na maza tumegomea msosi, aise. Tukapiga msosi mida ya saa 10. Saa 1 usiku, tukaitwa tukaambiwa kila mmoja abaki na bukta tu. Zilitembea stick, unapigwa tano, anaingia mwingine kamzunguko. Aise, hesabu yangu nakumbuka zilifika zaidi ya fimbo 50. Kilituokoa Babu aliingilia kati. Akamuambia nipige mimi🤣
 
Mzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.

Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.

Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.

Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
Dingi ako mshenzi sana🤣🤣 et utakuwa unapaka kiwi kichwani mpaka nywele ziote
 
Baadhi ya wazazi wa siku hizi wamekuwa kama wasseenge. Wao walilelewa kikamanda ila hawataki watoto wao walelewe kikamanda.
walimu wa zamani walitunyoosha. Ila walimu wa siku hizi wakimpiga tu mtoto wa mtu KESI IPO KISUTU
 
Wazazi wengi walikuwa wakatili na sio kufanya malezi

Kupigwa nimepigwa ya kunywa na kufuata nachoambiwa na sio napigwa kama mtuhumiwa

Poleni sana..... Wanangu wanabamiza kisawasawa Ila siwafanyii ukatili wa kishenzi wa kizamani cc BICHWA KOMWE na Dr Matola PhD
 
Baba akuwa mkali kwakweli. sijui nilipokuwa Mdogo ilantangu nilipopata Akili sikumbuki Kama alishawahi kunyanyua mkono wake kunipiga, Ila mtiti kwa bi mkubwa ni balaa.

Ilikuwa inafika kipindi ukichezea bakora kwa mama Baba anagombelezea Apumzike kwa amani.
Huyo baba yako anafanana na mimi.
Kidos wangu wakifika miaka 5 siwezi kuwachapa kabisa.
Hata kuwagombeza sitaki.
Nawaelekeza Kama watu wakubwa vile, wananisikikiza Sana kuliko bimkubwa wao.
Yeye mkali sana , anawachapa hovyo lakini hawamsikilizi kama wanavyo nisikiliza na kutii amri zangu.
Huwa namzuia kuwachapa namwambia awape adhabu mbadala mfano kazi flani, n.k.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom