Wengi wasingekubali kuja, na sasa hawatakubali kurudi

Wengi wasingekubali kuja, na sasa hawatakubali kurudi

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,564
Reaction score
91,857
WENGI WASINGEKUBALI KUJA, NA SASA HAWATAKUBALI KURUDI

Na, Robert Heriel


Wengi pengine tusingekubali kuja, hata hivyo hatuna namna tumeshakuja lakini ni hakika hatutakubali Kurudi Kama tukiambiwa turudi tena.

Sisemi nakufuru, wala simpi lawama yeyote isipokuwa naongea iliyoamini kabisa, wengi tusingekubali kuja huku.

Kama ningeambiwa mapema mambo haya walahi wabinlahi nisingeleta pua yangu, haya niyaonayo yanatia uchungu, yanatoa machozi na kuvunja moyo.

Wengi wetu tungejua kuwa huku Duniani kuna kushinda na njaa, na kukonda kisa ukosefu wa chakula alafu wakati huo huo kuna wenzetu wanakula na kusaza chakula.

Tena tungejua kuwa wakati Sisi tukisota Kwa Miayo, midomo ikipasuka Kwa ukosefu wa vitamini B, tena ikipauka wakati wapo wenzetu wanawapa mpaka mbwa wao minofu ya nyama. Hakika nakuambia tusingekuja Duniani.

Wengi tusingekuja Kama tungejua mapema kabisa huku Duniani tutakataliwa na Mademu pisi kali, Kama tungejua mapema kuwa Warembo na walimbwende wangetusonya wakitupandisha Kama bendera na kutushusha Kwa Dharau, hakika tusingekubali kuja huku.

Kama tungejua mapema kuwa tutaolewa na wanaume wakatili, wasiotujali Kama wake zao, Kama tungejua tutaolewa mafungu Kwa mafungu Kama Majike ya Nyani, tusingekuja Duniani, masuala ya kuolewa wake wengi ningejua walahi wabinlahi waswabrina tusingekuja.

Wengi tungejua mambo yapo hivi yalivyo, kutekekezwa na Baba, na kuishi maisha Kama wadudu watambao, amini! Amini nakuambia wengi tusingekuja.

Wengi tusingekuja Kama tungejua kuwa tungeongozwa na wanasiasa Matapeli, wabinafsi ambao wapo tayari kumwaga damu za watu kisa Madaraka, hakika tusingekubali kuja huku Duniani.

Wengi tusingekubali kuja huku Kama tungejua kuna kudhihakiwa na Vibamia vyetu, Ufupi wetu, ubonge wetu, Papuchi zetu kuwa bwawa.
Kamwe tusingekubali kuja naapia, Kama tungejua Ualbino wangu ni Dili na kuwindwa Kama panya kwenye Ghetto la msela Nondo, tusingekuja.

Wengi tusingekubali kuja Kama mambo yenyewe ndio haya kuugua magonjwa ya kuumiza, tena magonjwa hayo hayo ndio biashara inayolipa hasa wenzetu wanajipigia mapesa huku Sisi yakituacha na Ufukara Kama sio majonzi ya kufiwa na wapenzi wetu. loooh!

Wengi tusingekubali kuja Kama Wake tuliowaoa ndio hao hao wananyanduliwa na kutuzalia watoto wasiowetu. Kama mambo haya tungeyajua mapema walahi wengi Wasingekubali Kuja.

Wengi Wasingekubali Kuja Kama tungejua kuja vita na mauaji ya kikatili ambayo hufanywa na watabe na wababe WA dunia. Eeeh! Naapia walahi tusingekuja.

Wengi Wasingekubali Kuja Kama ishu zenyewe ndio hizi za kulipwa vimishahara vya watumwa vya sogeza siku, nakuhakikishia tusingekubali.

Wengi Wasingekubali kuoa/kuolewa na wanaume walionao hivi leo.

Wengi tulitaka wanawake wakali, warembo Kama Malaika.

Tungechagua wanaume handsome boy, wenye pesa na magentlemen

Wengi Wasingekubali Kuja hapa Duniani Kama wangejua wangezaliwa Afrika. Wangechagua kuzaliwa Ulaya huko.

Sasa tumeshakuja Duniani hatuna jinsi,

Sasa tukishakufa maana tutakufa hiyo ni hakika, Kama tukiambiwa turudi tena Duniani Nina uhakika wengi watakataa kurudi Kwa Hali ilivyo wengi wataona imetosha.

Nani Arudi ili achekwe Kwakuwa single mother

Nani Arudi adhalilike Kwa kushindwa kulisha watoto wake

Nani arudi?

Nani arudi ambaye hajachoshwa na stress za mapenzi?

Nani arudi mumewe/mkewe akimtelekeza na kuoa/kuolewa na mtu mwingine, Nani huyo?

Nani arudi ashuhudie uharamia unaofanywa na wanasiasa ambao kazi kujilimbikiza mali na kuwaacha raia wakipiga Miayo? Nani huyo??

Wengi tusingekubali kuja lakini Kwa vile tumekuja tunaishi kishingo Upande, lakini tukiondoka wengi hatutakubali Kurudi Duniani.

Haya nayo niliyasema;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa MOROGORO
 
Wengi tungejua mambo yapo hivi yalivyo, kutekekezwa na Baba, na kuishi maisha Kama wadudu watambao, amini! Amini nakuambia wengi tusingekuja.
 
Wengi tusingekubali kama mwendazake hata kuwepo na watu wake
 
Unaposema Kuja..., una-assume kuna huko kulikotoka na huko ni pazuri kuliko hapa / sasa.... Anyway its just state of Mind Ukitoa wale wanaobakwa / kunyanyaswa n.k. wengi maisha yetu ni mazuri tatizo haturidhiki na tunaishi kwa uwiano wa waliotuzidi na sio tuliowazidi au binafsi tunataka nini (Peer Pressure)

Mimi ninakupa another challenge..., huko tunakoenda kama ni kuimba, hakuna kulala wala usingizi, hakuna njaa wala huzuni..., yaani ni state ya kusifia na kuomba (unadhani wengi wakijua watakubali kwenda)? Au life will be boring na wataona bora tulipotoka..., AU the main question is Tunapokwenda kuna nini
 
Hujachagua kuja. Mama na baba yako ndiyo wamelazimisha uje. Kama usingekubali kuja, basi usiwe sababu ya wewe kuwaleta wengine.

Usitafute mtoto Mkuu. Utabaki na amani.
 
WENGI WASINGEKUBALI KUJA, NA SASA HAWATAKUBALI KURUDI

Na, Robert Heriel


Wengi pengine tusingekubali kuja, hata hivyo hatuna namna tumeshakuja lakini ni hakika hatutakubali Kurudi Kama
You can't stop it, na ndio maana umekuja. Lazima uelewe kwamba kila kiumbe ameumbwa na future yake.
Kwa maana future ni mambo yatarijiwayo na nibayana ya mambo yasiyoonekana.

But "unaposema wengi wasingekuja duniani kama wangejua wangezaliwa afrika". Haya ni mawazo mgando yanayoletwa na Inferiority complex.
 
Mimi ningeambiwa nije maisha haya nisingekataa.

Yani nimewekwa katikati.

Nikiangalia chini naona watu kibao wamepigika, wananihusu, halafu mimi ndiye msaada kwao, nisingekuwepo wangefanyaje?

Halafu nikiangalia juu naona watu kibao wamenipiga, wananipa motisha ya kufanya mambo vizuri zaidi nijiongeze, nisibweteke.

Yani hii nafasi ni nzuri zaidi ya kuwa top, maana unaweza kuwa top ukawa bored huna challenge, au unaweza kuwa chini ukakata tamaa na kutaka kujiua.

Kanuni yangu ya maisha ni kufanyia kazi mapungufu, ili kupata ninachotaka, na nikishindwa kabisa, nikubali hali yangu bila ya kuwa na tamaa ya vile ambavyo viko nje ya uwezo wangu.
 
Mimi ningeambiwa nije maisha haya nisingekataa.

Yani nimewekwa katikati.

Nikiangalia chini naona watu kibao wamepigika, wananihusu, halafu mimi ndiye msaada kwao, nisingekuwepo wangefanyaje?

Halafu nikiangalia juu naona watu kibao wamenipiga, wananipa motisha ya kufanya mambo vizuri zaidi nijiongeze, nisibweteke.

Yani hii nafasi ni nzuri zaidi ya kuwa top, maana unaweza kuwa top ukawa bored huna challenge, au unaweza kuwa chini ukakata tamaa na kutaka kujiua.

Kanuni yangu ya maisha ni kufanyia kazi mapungufu, ili kupata ninachotaka, na nikishindwa kabisa, nikubali hali yangu bila ya kuwa na tamaa ya vile ambavyo viko nje ya uwezo wangu.

Hahahaha
 
Tulikuwa wapi kabla ya kuja duniani?
 
Tusingekubali kuja penzi lenyewe tunapewa kwa kufikiriwa
Nalog off
 
Back
Top Bottom