Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,638
- 220,409
Kidawa binti mrembo alimaliza masomo yake ya ukatibu muhtasi kule Tabora na kupata ajira mjini. Akiwa mgeni ofisini aliletewa kadi ya mchango wa harusi, ilikuwa ni harusi ya mdogo wa mfanyakazi mwenzao. Kidawa alitoa mchango na kupata kadi ya harusi. Kule harusini alikaa meza moja na mkaka ambae alikuja kuwa mume wake mwaka mmoja mbele.
Akiwa kwenye ndoa ya miaka mitano rafiki yake waliyekuwa nae chuoni Tabora alimtafuta Facebook. Shost alimuomba namba ya simu, walipoanza kuongea shost alifunguka kuwa amepata kazi Dar lakini hana pa kufikia.
Huyu ni rafiki yule wa kushare chips dume chuoni mpango wa pesa ukienda kombo. Kidawa alimueleza mume wake, nae aliridhia kumkaribisha kwa muda. Kidawa na mume wake walikuwa na nyumba ya vyumba vitano vya kulala.
Shost amefika alianza kuyaonea wivu maisha ya Kidawa, Kidawa hakujua hata bei ya mchele wala soko la samaki Ferry. Hata pesa ya petrol ya gari mume wake alimpa.
Shost alianza kuzidisha ufundi jikoni, mpaka mume wa Kidawa aliomba kabisa shemeji ninaomba unipikie chapati kama zile za wiki iliyopita. Kidawa alivyo naive hakuona kuwa ile ilkuwa a wake up call.
Kidawa alifurahi kukaa na shost nyumbani wala hakujali tena muda mume wake yuko bar na rafiki zake. Shost alimuuliza maudhi kwenye ndoa yapo? Kidawa alijibu jinsi alivyowanyoosha mawifi zake walipoanza kuleta kidomo domo. Kumbe shost ana mrekodi kwenye simu.
Shost alianza kupanga menu ya nyumba Kidawa aliona mmh huku tunakokwenda siko. Kwa muda huo alishakaa mwaka wala hazumngumzii tena kutafuta nyumba. Alianza kumtembelea shemeji ofisini na kumueleza jinsi Kidawa anavyowaponda dada zake na voice mail alumuekea.
Ndoa iliyumba sana, yule kaka alimuomba dada yake akae na watoto, shost aondoke na yeye na Kidawa waende Zanzibar kwa wiki moja. Kule waliongea mengi na walifanikiwa kuinusuru ndoa yao.