Wema, tatizo ni nini?

Jamani acheni mungu aitwe mung, ukiona mwenzako ananyolewa basi wewe tia maji. Sasa huyo mdada ni mdogo bado; akaingiwa na pepo la ngono, pepo likakuta yuko empty hana macho ya imani utategemea nini?

Wewe unayemshauri muombee tu kwa mwenyezi mungu amtie nguvu na kuondoa hilo pepo la ngono linalomsumbua.
 
Atakuwa na matatizo yeye na sio hao wanaume anaokuwa nao kimapenzi, haiwezekani kila siku aachane na kuanzisha uhusiano mpya. Ajiangalie sana huyu dada.

Tatizo kubwa la mabinti toka mikoani huwa ni ushamba. Alipokuwa undergrond alikuwa na Mr Blue(umesahau hilo), alipopanda chati akammwaga dogo akawa na wenye majina. Mwambie acheki na mimi nimshauri. Nina over 40 years na ni msahauri wa vijana.
 
Mtasema weeee, mwenzenu ndo kwanza karudiana na Chalz Baba wakati juzi kati alikuwa na Diamond na wote wawili walikuwa wakitamba sana kwamba sasa wamefika. Fuatilia kisa kamili hapa hapa: WEMA, CHALZ BABA.

wemanachalzbaba.jpg
 
Ni pepo la ngono baaasi! Na diamond limbukeni juzjuz alikua very very poor! Sasa amesaau si mbali sana kutoka sasa atarudia zama zake.
 
Kwako,
Mpendwa dada Wema Sepetu. Naamini u mzima kiafya na unaendelea vizuri na mchakato wa kutafuta mkate wa kila siku.
Kwanza kabisa, pole kwa matatizo. Nilisikia kuwa juzi ulipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumtolea maneno makali Bob Junior. Yataisha tu...usijali.

Nimeona leo nikuandikie barua dada yangu, maana nahisi kama hufahamu kinachoendelea huku uswahili. Washkaji wa vijiweni wamebadilisha stori, wanakuzungumzia wewe. Siyo Barcelona wala Arsenal tena, ni wewe tu. Unajua wanajadili nini kuhusu huyo Wema?

Ngoja nikuambie...wanazungumza kuhusu haya matatizo yasiyoisha unapokuwa katika ‘relationship’. Tatizo ni nini? Hivi, unakumbuka kipindi kile ulipotwaa taji ya Miss Tanzania? Wiki chache tu, yakaibuka mambo...kwamba ulikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wawili wa Bongo Fleva (kwa nyakati tofauti), ingawa mpaka leo unaendelea kukanusha.

Hayo tuyaache, hebu tuanzie pale ulipokuwa na Kanumba (Steven), baadaye ukahamisha majeshi kwa mjasiriamali Jumbe Yusuf Jumbe.
Nini kilitokea? Pamoja na kwamba ulikuwa umeachana na Kanumba, maneno yakaanza kiasi cha kuvunja vioo vya gari lake, mwisho wake ukawa Segerea! Aibu kiasi gani? Niliamini tukio lile lilikupa funzo lakini kumbe...!

Sitaki kufuatilia sana mambo yako ya ndani, lakini nakumbuka baadaye ulikuwa katika himaya ya mwanamuziki wa Twanga Pepeta Chalz Baba. Mkavuma kweli kweli. Kila mahali mlikuwa pamoja huku mkijinadi kwenye vyombo vya habari kwamba mngefunga ndoa. Uhusiano wenu ukawa gumzo jijini, lakini baadaye ukasafiri kwenda Marekani.

Ukiwa huko, uhusiano ukaanza kuyumba, uliporudi Bongo, ukaangukia kwa Diamond. Mapenzi yamekuwa ‘hot’ ile mbaya ingawa hivi sasa inaelezwa kwamba kuna harufu ya kuvurugika!

Lakini ukiwa na Diamond, ukakumbwa na hili balaa linalosumbua sasa hivi...kesi na Bob Junior ambaye ana bifu na boyfriend wako Diamond. Sitaki kuingilia sana suala hili, maana lipo mahakamani, lakini cha kujiuliza hapa, kwanini haya yote yanatokea?

Wema, nadhani kuna maeneo unatakiwa kujikagua. Kuna mahali kuna tatizo. Mosi, kujitambua na kuthamini thamani yako kama msichana uliyepata bahati ya kushika wadhifa mkubwa wa Miss Tanzania 2006. Hiyo ni heshima ambayo haiwezi kufutika. Ukisimama sehemu yoyote utajulikana kama Miss Tanzania.

Ni hadhi hiyo Wema. Hadhi ambayo inahitaji kutendewa haki. Naamini ukitulia na kujichunguza utagundua ni wapi unaposea. Nitakupa mwanga wa mahali pa kuanzia.
Kwanza; chunguza marafiki zako, maana kama ukiwa na marafiki wenye ushawishi wa kufanya mambo mabaya, utajikuta na wewe unafanya vitu kinyume na jamii halafu mwisho wa siku, unabaki na aibu zako mwenyewe.

Pili, nakushauri kabla ya kuingia kwenye uhusiano ni vizuri kumchunguza na kumjua vizuri huyo mtu ambaye unataka awe mpenzi wako.
Unaweza kuwa na mpenzi mwenye tabia za hovyo na ushawishi hasi, ambao utakufanya na wewe uwe mfuasi wa tabia zake, mwisho wake unaishia pabaya. Jichunguze, wapi unapokosea? Kujua tatizo ndiyo mwanzo wa kusonga mbele katika kufanya mabadiliko.

Naamini ukisoma maandishi ya barua hii kama simulizi za kusisimua, hakuna utakachoelewa, lakini ukisoma kama waraka kutoka kwa mtu ambaye anapenda mafanikio yako, utabadilika na kuwa bora zaidi. Wewe ni staa Wema. Hebu ishi kistaa.
Ahsante kwa kusoma barua yangu.
Wako katika kuwekana sawa,

Jamani tunaomba utupatie source ya hii kitu yako, wana JF tujaribu kutekeleza yale tunayowashauri wenzetu. Juzijuzi hapa Dr Shayo, H. alishambuliwa sana kwa ku copy na ku paste document ya mtu na kuiandika as if ni yake bila ku acknowledge source, naona na wewe umeyarudia yale yale ya Shayo. Pls dont repeat mistakes.

 
Back
Top Bottom