Wema, tatizo ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wema, tatizo ni nini?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by didas, May 11, 2011.

 1. d

  didas Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwako,
  Mpendwa dada Wema Sepetu. Naamini u mzima kiafya na unaendelea vizuri na mchakato wa kutafuta mkate wa kila siku.
  Kwanza kabisa, pole kwa matatizo. Nilisikia kuwa juzi ulipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumtolea maneno makali Bob Junior. Yataisha tu...usijali.

  Nimeona leo nikuandikie barua dada yangu, maana nahisi kama hufahamu kinachoendelea huku uswahili. Washkaji wa vijiweni wamebadilisha stori, wanakuzungumzia wewe. Siyo Barcelona wala Arsenal tena, ni wewe tu. Unajua wanajadili nini kuhusu huyo Wema?

  Ngoja nikuambie...wanazungumza kuhusu haya matatizo yasiyoisha unapokuwa katika ‘relationship’. Tatizo ni nini? Hivi, unakumbuka kipindi kile ulipotwaa taji ya Miss Tanzania? Wiki chache tu, yakaibuka mambo...kwamba ulikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wawili wa Bongo Fleva (kwa nyakati tofauti), ingawa mpaka leo unaendelea kukanusha.

  Hayo tuyaache, hebu tuanzie pale ulipokuwa na Kanumba (Steven), baadaye ukahamisha majeshi kwa mjasiriamali Jumbe Yusuf Jumbe.
  Nini kilitokea? Pamoja na kwamba ulikuwa umeachana na Kanumba, maneno yakaanza kiasi cha kuvunja vioo vya gari lake, mwisho wake ukawa Segerea! Aibu kiasi gani? Niliamini tukio lile lilikupa funzo lakini kumbe...!

  Sitaki kufuatilia sana mambo yako ya ndani, lakini nakumbuka baadaye ulikuwa katika himaya ya mwanamuziki wa Twanga Pepeta Chalz Baba. Mkavuma kweli kweli. Kila mahali mlikuwa pamoja huku mkijinadi kwenye vyombo vya habari kwamba mngefunga ndoa. Uhusiano wenu ukawa gumzo jijini, lakini baadaye ukasafiri kwenda Marekani.

  Ukiwa huko, uhusiano ukaanza kuyumba, uliporudi Bongo, ukaangukia kwa Diamond. Mapenzi yamekuwa ‘hot’ ile mbaya ingawa hivi sasa inaelezwa kwamba kuna harufu ya kuvurugika!

  Lakini ukiwa na Diamond, ukakumbwa na hili balaa linalosumbua sasa hivi...kesi na Bob Junior ambaye ana bifu na boyfriend wako Diamond. Sitaki kuingilia sana suala hili, maana lipo mahakamani, lakini cha kujiuliza hapa, kwanini haya yote yanatokea?

  Wema, nadhani kuna maeneo unatakiwa kujikagua. Kuna mahali kuna tatizo. Mosi, kujitambua na kuthamini thamani yako kama msichana uliyepata bahati ya kushika wadhifa mkubwa wa Miss Tanzania 2006. Hiyo ni heshima ambayo haiwezi kufutika. Ukisimama sehemu yoyote utajulikana kama Miss Tanzania.

  Ni hadhi hiyo Wema. Hadhi ambayo inahitaji kutendewa haki. Naamini ukitulia na kujichunguza utagundua ni wapi unaposea. Nitakupa mwanga wa mahali pa kuanzia.
  Kwanza; chunguza marafiki zako, maana kama ukiwa na marafiki wenye ushawishi wa kufanya mambo mabaya, utajikuta na wewe unafanya vitu kinyume na jamii halafu mwisho wa siku, unabaki na aibu zako mwenyewe.

  Pili, nakushauri kabla ya kuingia kwenye uhusiano ni vizuri kumchunguza na kumjua vizuri huyo mtu ambaye unataka awe mpenzi wako.
  Unaweza kuwa na mpenzi mwenye tabia za hovyo na ushawishi hasi, ambao utakufanya na wewe uwe mfuasi wa tabia zake, mwisho wake unaishia pabaya. Jichunguze, wapi unapokosea? Kujua tatizo ndiyo mwanzo wa kusonga mbele katika kufanya mabadiliko.

  Naamini ukisoma maandishi ya barua hii kama simulizi za kusisimua, hakuna utakachoelewa, lakini ukisoma kama waraka kutoka kwa mtu ambaye anapenda mafanikio yako, utabadilika na kuwa bora zaidi. Wewe ni staa Wema. Hebu ishi kistaa.
  Ahsante kwa kusoma barua yangu.
  Wako katika kuwekana sawa,
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Atakuwa na matatizo yeye na sio hao wanaume anaokuwa nao kimapenzi, haiwezekani kila siku aachane na kuanzisha uhusiano mpya. Ajiangalie sana huyu dada.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  "...I do fall in LOVE at First Sight..."

  By Wema (Mtoto wa Balozi) Sepetu
   
 4. RR

  RR JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Anafanya rihaso ya muvi ya mapenzi...
   
 5. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Lakuvunda!!
   
 6. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  :bange:
   
 7. ALLEX

  ALLEX JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 2,046
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Huo ushauri alishapewa sana... Kutakuwa na mtaalam kamwekea kipele maji kinamuwasha ndiyo maana anatafuta wa kumkuna hampati..

  ushauri; rudi kwa yuleyule uliyegoma kumtaja kwenye tv interview
  didas; unambembeleza wa nini mpaka unamwita dada kuwa bwana.. Kama unataka na wewe kuwa wazi///
   
 8. misnomer

  misnomer Senior Member

  #8
  May 11, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Didas, huu ukumbi wa picha, nadhani siku nyingine utarekebisha hiyo. Ila kwa vile bado junior, ngoja basi tukuwekee japo hii ya huyo Wema unayempa ushauri nasaha.
  WemaIsaacSEPETU.jpg
   
 9. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hivi Liyumba hakupita hapa?
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Unauliza majibu?
   
 11. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nami namshangaaa!
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ukumbi wa picha ... then mtu analeta mkeka wake hapa!
   
 13. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tukiwa watoto.....ukipenda kuzurura......unaambiwa umekula miguu ya kuku
  ukiwa msahaulifu.....umekula kichwa cha samaki
  na simulizi zinasema kondoo ana wadudu wawili kichwani, wakianza kuwasha ndo pale wanapopigana ili kuwatuliza/kujikuna
  SASA UKILA KICHWA CHA KONDOO...TENA UKAWA NI BINTI.....WAHENGA WANAMAJIBU SAHIHI
   
 14. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  halina ubani
   
 15. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  m mwenyewe nashangaa imebaki na mm niwe nae
   
 16. DON KILLUMINATI

  DON KILLUMINATI Senior Member

  #16
  May 11, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  HILI LISHAWAHI JADILIWA HAPA JAMVINI:

  https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/24332-amatus-liyumba-balaa-20.html
   
 17. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Ili ni jukwaa la picha, sasa picha ya Wema iko wapi?
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Binti ana kale kapepo ka ngono nadhani.Si bure.
   
 19. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  iko siku atatulia na kujirekebisha
   
 20. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hajatulia anakilanga huyu Binti.
   
Loading...