Mchumba
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 280
- 262
Msanii wa filamu na mjasiriamali Wema Sepetu amefunguka ya moyoni kutokana na namna mashabiki wake wa mitandaoni wanavyomchukulia na kumpa maneno ambayo muda mwingine yanamuumiza na kumkosesha amani na kumfanya ajione ni kama mkosaji mkubwa.
“Kitu ambacho nakiona kutoka mitandaoni, Watu wanapenda sana fujo fujo, Purukushani, mara huyu na huyu hawaongei, flani kamchukulia flani bwana, yule kafumaniwa.
Hicho ndiyo mnachokiona kina kick. Ila mwisho wa siku ukija kuangalia , ni kweli maana dunia ya leo umbea unauza. Ila jamani ifike muda tukue mimi binafsi kuna vitu vinanichosha actually vimenichosha ifike muda kila mtu aangalie maisha yake na afanye kile kinachomridhisha nafsi yake. kwangu naangalia wat God has to say bout wat im doin… Imekuwa too much tokea nilivyopost uzalendo ikaonekana all sorts of Crazy, But u know wat, I dont care” aliandika Wema Sepetu
“Sasa basi, nitapost ninachotaka nyinyi endeleeni kujudge na kuleta conclusion zenu mnazojua… Iwe nataka attention, iwe natafuta kick, iwe nitokeje, iwe najipendekeza, iwe vyovyote It all comes down to me. Kuna msemo unasemaga tenda Wema uende zako… Dats how I roll.
Na nimekuwa nikifanya hivyo siku zote. Sitegemei na wala sitaki mtu ninae msupport au kumuunga mkono na yeye afanye the same na wala sina haja na kupostiwa. Niwe sipindui au napindua It doesnt make A difference.
Kwanza haya mambo ya kupinduana yameanzaga lini Mungu wangu. Ila instagram mna majungu sana. Mimi siwezi jamani mniachage basi sometimes, sina amani imekuwa kama nimeua” aliongeza Wema Sepetu
Source: EATV