Niko katika wakati mgumu kuliko wakati wowote wa maisha yangu

Firmino bobby

JF-Expert Member
Mar 7, 2018
228
589
Habari wakuu,

Kimsingi mimi ni miongoni mwa wanadamu wasiokua na furaha kabisa, nilimaliza chuo miaka miwili iliyopita nikiwa na degree yangu ya sheria mkononi, sikua na sababu ya kurudi nyumbani tena, kwani kwetu ni masikini sana nisingeeleweka tena, nimalize chuo kikuu alaf nirudi tu nyumbani kuwapa mzigo mwingine wazazi na bado kuna wadogo zangu wengine wanasoma na huenda na wao walikua wanajua kaka yao si nimemaliza chuo basi nitapata kazi na kuwasaidia sana.

Nikabakia hapa Dar, nikiwa nimepanga chumba mimi na rafiki yangu nikaanza harakati za kutafuta kazi na naomba kusema kuwa nilipambana isivyo kawaida, hakuna kazi niliyofanikiwa kupata kwa kweli, basi ikanibidi nianze kusajili line kama freelancer tu, nikawa nazunguka mitaani siku nyingine nakutana na marafiki zangu wa chuo wananishangaa na kucheka sana, sikujali ilo kwakua nilikua nimeweka target zangu.

Kazi ile ilikua ngumu, hakuna kona ya Dar nisiyoijua, pote nilifika kwa miguu, nashukuru Mungu tu hela niliyokua naipata niliweza kula na kulipia kodi ya chumba uswahilini, muda ukafika nika apply law school kwenda kusomea uwakili pale, nikachaguliwa kujiunga nao pale mwezi april mwaka 2017, mpaka muda huo unafika sikuweza kua hata na elf 50 tu huku fedha zote hadi usajiliwe pale ikiwa ni milion 1 na laki 5.

Sikuwa na la kufanya tena nikaandika barua ya kughairi na kuomba waniunganishe na intake ya mwezi wa 8 mwaka huo, huku mtaani hali ikawa mbaya kabisa baada ya tigo nao kuanzisha utaratibu wa kuuza line za chuo elfu 10, ni line hizi ndio zilikua zinaniweka mjini, kazi ikaanza kua ngumu rasmi.

Nikaachana nayo nikarudi tena kuanza kutafuta kazi za maofsini nikaomba hadi za kuvoluntia lakini wapi sikupata chochote, mwezi wa nane ukafika sikua na chochote na kule excuse ikawa imepita hivyo basi law school nikaendelea kuisikia kwa wenzangu tuliokua tunasoma wote, kwa baadae nikapata kazi ya kuosha magari Tabata, wala hata sikujivunga nikaanza kuosha magari pale wale jamaa kutwa wananitania wewe dogo si ulikataa shule piga kazi maisha haya magumu, hawakujua.

Ninachoshukuru hela niliyoipata hapa iliniwezesha kulipa kodi ya chumba mwaka mzima ya laki tatu na 60, na kumudu gharama za chakula vyema, nikaanza kuweka akiba kidogo target yangu iko pale pale, kwa baadae carwash hii ikafungwa na mwenye nayo akidai hana anachokipata hela yote inalipia tu madeni bora auze mashine amalize deni aangalie ishu zingine, nikaondoka hapo nina karibu akiba ya laki mbili.

Mwezi Disemba mwaka jana shule ya sheria ikatoa tena nafasi kwa intake mbili ya mwezi wa kwanza na wa sita, nika apply tena upya kabisa, wakanipanga January, na hapo sasa sina kazi sina mfadhili yoyote, na nimekwisha andika barua za kila namna, nimeomba ufadhili kwa ndugu zangu wenye uwezo ninao wafahamu hakuna hata aliejisumbua kunijibu.

Mwezi wa kwanza umefika nikaenda tena kuomba kuairisha mpaka June, na yule dada wa mapokezi pale mpaka kashanikariri, mwisho akanishauti tu wewe hauna uwezo wa kulipa ada yote hapa anza kulipa taratibu kidogo kidogo ukija mwezi wa 6 utatuletea risiti zote tutakupokea, basi sikukata tamaa nikaanza upya tena.

Kimsingi hakuna nililofanikiwa, Roho huwa inaniuma sana nikikutana na mawakili, ninajiona kabisa kua wao ninahitaji nafasi moja tu katika maisha yangu nibadilishe kila kitu, ninahitaji law school tu, roho inaniuma kila siku, nina stress zisizo za kawaida, usiku hua silali, saa zingine naamka naanza kujisomea madaftari yangu ya sheria, napitia sheria mbali mbali, kujifariji tu, hakuna kinachoongezeka.

Kuna muda hua naenda pale law school nakaa nje ya geti pale hata masaa mawili nawaangalia watu wanavyotoka na kuingia, wanafuraha sana, naumia roho narudi geto kulala tu na kila siku namwambia Mungu ukunipa hii nafasi ya kujiunga na hio shule Tanzania itafahamu kuna mwanasheria wa aina yake aliwai kutokea.

Kimsingi sina furaha wala amani kabisa na maisha haya muda mwingine najilaumu au pengine nisingezaliwa tu kuja kukutana na maumivu kama haya, nina kiu ya elimu kupindukia, kwangu wala sijali hata chakula au mavazi, ila tu hili swala la kwenda hio shule ya vitendo kwa wanasheria.

Kwa heshima na taadhima ndugu zangu naombeni mnipatie ushauri utakao nituliza kisaikolojia na kwa yoyote atakaeguswa kwa namna moja au nyingine anaweza nisaidia kwa vyovyote vile iwe kazi hata Garden Keeper I,m ok with that swala tu itanisaidia katika kupata pesa itakayotimiza ndoto zangu.

Mpaka naandika haya amini ya kwamba nimevuka mipaka yote ya aibu na sense of human, nitakufa siku sio zangu ni bora niliweke hadharani huenda kuna mtu au watu wakaguswa kwa namna moja au nyingine. Kama kuna watu wanaomba msaada kwa namna moja au nyingine na wanasaidiwa kwanini nisiwe mimi?

Sorry kwa maelezo marefu.

UPDATES

Nimejaribu kuwasiliana na mods napata poor response kutoka kwao, isipokua muda mchache uliopita walinijibu kwa kifupi ili waweze kuniverify niwape details zangu na supportive evidences na wao watanitangaza hapa kwa majina yangu yote matatu, kitu kilichowapelekea mimi kuwauliza haki yangu ya privacy itakua wapi? Ni kwanini nisiwape wao supportive evidences na kila kitu watakachohitaji kufahamu nikawapa bila shida na wakaridhika kwa asilimia zote alaf ndio wakaja hapa kukiri hay niliyoyasema then wanithibitishe bila kuvunja haki yangu yoyote kama member, na tena basi nimekubaliana waweke hapa documents zangu zote ila wafiche majina mengine waache jina moja tu maana hoja ni uhalisia wakutaka msaada na hoja sio mimi ni nani? Kutaka msaada haina maana kua mtumwa, na msaada sidhani kama una masharti ni kiasi cha kukubali au kukataa, mie nna mda kidogo hapa jf na nimeona watu wakinyanyasika kisa kutaka kwao msaada kwenye majukwaa ya afya na mahusiano tu, hali ilitisha... Wakiendelea kukataa sanaa sitakua na cha kufanya nitaleta vyote alafu wao ndio wataamua maana mie sindio natak msaada bhana, ila bado sipati mantiki ya maneno ya melo siku ile mahakamani akililia privacy ya hawa watumiaji wa jf... Ni matumaini yangu sijawa kikwazo kwa namna yoyote ile, na kuna members wa humu ambao nakosa namna y kuwashkuru kwa jinsi walivyonifariji na kuniPM na karibj wote ambao nimewasiliana PM nimewapa documents halisi na ushaidi wa kila namna ikiwemo namba zangu na niko tayari kufanya hivi kwa yoyote atakaeguswa na mimi.... Wanaokejeli nimesoma text zao sina chakuwajibu uenda wako ktk nyakati zao bora za maisha.


UPDATES
Nikaribu wiki mbili sasa zimepita tangu nilete maswaibu yangu haya nnayoyapitia kwenu, nimefarijika na namna watu walivyo respond kwenye huu uzi, ushauri wenu na maneno yakunitia moyo vimenipa nguvu sanaa, nawashukuruni sanaa sanaaa kwa hili, lakini pia baadhi waliaidi kunisaidia na kunipa ahadi zao kabla ya huo mwezi wa sita kufika, na ninawaombea, lakini vile vile ni lazima nije hapa jukwaani kuleta mrejesho wa kiasi nilicho kipata hili watu wajue watanisaidia vp hapo nilipo kwama.

Tangu nilete maombi haya kwenu, kuna wadau waliguswa na wakataka niwathibitishie habari za maombi yangu kwao na waliporidhika na uthibitisho wangu wakanichangia pasipo tabu yoyote, na mpaka kufikia tarehe ya leo jumla ya kiasi kilichopatikana mpaka sasa ni laki 6 na elf 30 (630,000/=) huku kiasi kinachotakiwa kwa ajili ya usajili ni 1560,000/ (milion moja laki tano na elf 60). na kuna baadhi ya wadau walioaidi kutoa chochote watakachopata mwishoni mwa mwezi huu, na penyewe nitaleta updates pia.


Swala lingine lilikua la uthibitisho wa angalau hata CV tu na barua ya kweli kua selected na kujiunga hapo Law School mwezi june, hili sina shaka wala hofu nalo, tayari nimeshawathibitishia watu wengi na nitamthibitishia yoyote yule muda wowote ule PM kwake au hata face to face akihitaji tuonane na nikiwa na nyaraka zote za uthibitisho.

Ahsanteni, nitaendelea kuleta upadates kadri lengo linavyofikiwa na kwenda, nawashukuru sanaa.

UPDATES 10 may 2018

kama nilivyowai kuahidi kua ntakua naendelea kuleta updates za mara kwa mara kwa pale ntakapokua nimefikia.

sasa ikiwa imepita miezi miwili toka nianze harakati hizi, atimae kuna wadau wengi tuliwasaliana nao PM wakanitumia michango yao kwa kadri ya uwezo wao na kadri Mungu alivyowajalia, na hapo juu kuna baadhi ya updates, atimae mie pia nilijicommit kuakikisha nafikia lengo hili ikiwemo kuuza baadhi ya vitu vyangu, atimae nilifikisha milion moja na kwenda kuilipa CRDB nimeambatanisha na nakala ya risiti yake hapa.

sasa nimebakiza kiasi cha laki tano na sitin elfu (560000) ili ada ya shule ya sheria itimie nikaanze mwanzo wa kutumiza ile ndoto ya siku zote.

bado napambana na bado nahitaji msaada wenu pia, walionisaidia kwa kila namna wameingia kwenye historia ya maisha yangu.... na vile vile ntaendelea kuwa proove wrong wale ambao wamekua wakituhumu juu ya utapeli.

EXCLUSIVE UPDATES 04 July 2018

Wakuu kwema, nilikua naisubiri hii siku kwa mudà mrefu sanaa, nina maneno mengi ya kusema na asilimia 90 yake ni ya kushukuru sanaa, Kwanza nikiri kua Mungu ni mkubwa sanaa, ni usiku mmoja tu nikiwa nimekosa usingizi kabisa kwa sababu ya stress na kukosa future mtaani na baada ya kua nimejaribu na kufanya kila kitu, nilipata wazo tu nakusema ngoja niandike history yangu fupi ya hustlin, wishes na maombi JF kwakua nimekua member wa JF kwa muda mrefu na kuona watu mbali mbali wakielezea matatizo yao, awali kabla sikuwai kuhisi lolote et nnaweza kusaidiwa na JF na sikujua ntafika umbali wowote au kupata msaada wowote wa maana na nilisema ngoja ñijiandikie tu ukweli wabyote nnayopitia as long as sina ntakalopoteza maana hali ni ile ile tu.

kama mnavyoona historia nzima hapo juu, atimae nilikutana na watu wa kipekee sanaa dunia kupata kuwaona, kwa hawa watu ngoja niache space maana wikiend hii ntaandika jambo juu yao na watu wengine watajifunza kitu na kujua watu wema bado wanaishi.

kufànya mambo yasiwe mengi hivi ñnavyoandika ni mwanafunzi tayari wa chuo cha sheria (Mafunzo kwa vitendo)/TLS nikiwa nimekamilisha kila kitu, mwenye furaha na hakuna wakati nnaoelewa mambo kama huu.

nnawashukuru sanaa, nna deni kubwa la kulipa, mmeingia kwenye historia ya maisha yangu, nimewakalili nakuwahifadhi kwenye moyo na fikra zangu siku zote, kwanza bado nawahitaji na tuko pamoja.

kwa wale waliojua kua mim ni tapeli na nimekuja kuwatapeli watu nafikiri mtakua mmejifunza kutokuhukumu watu kirahisi tu, na kuna wale sijui niseme haters au kitu gani wale ambao mtu anatukana page hata 6 mim na wale wanaochangia kwa maneno mazito na yale yale ilihali hajakosewa na wala hajatoa hata mia hawa nao niwashukuru kwa kuja kupoteza muda mitandaoni na kusema wasamehewe tu.

Mungu ni mkubwa kanikutanisha na nyinyi na nyie mmefanya niingie COHORT 27.

kuingia Law School ni jambo moja na kufaulu ni jambo jingine, huko niliko toka kunatisha, ntapambana kufa kupona hakuna muda wa kurudi nyuma tena.... kwa sasa changamoto zipo kwenye hizi stationaries na material mengine ya kisheria haya maisha ya kawaida, nnaishi kigumu tu na kujibana n kujinyima ila Mungu bado ataendelea kutenda miujiza kama alivyoanza.

ada ilikua ni miliona moja laki tano na sabini kwa muda wote wa masomo na tayari imeshalipwa baada ya kuanza kukusanywa kwa muda wa miezi mitatu na nusu yote ikiwa michango ya wadau wachache toka hapa JF.

ahsanteni sanaa sana sanaa, ahsante kuliko nnavyoweza kushukuru, Your too far kind.

NB. kutakua na mfululizo wa updates pale kutakapokuwepo na ulazima, kila kitu kitakua wazi tu.
 

Attachments

  • Screenshot_2018-05-10-01-45-41.jpg
    Screenshot_2018-05-10-01-45-41.jpg
    6.6 KB · Views: 243
Kuelewa tatizo lako ni mwanzo wa ufahamu,na kuweka tatizo lako hapa ni mwanzo wa mafanikio,watu wengi wamepitia vipindi vigumu mpaka wakafika hapo walipo,

Endelea kuvumilia tu mkuu na huenda hapa ukapata msaada wa kimawazo,kimali au kazi yeyote,endelea kumuomba Mungu na kumuamini hii ni mitihani ya dunia tu na haya yote yatapita.
 
kwahiyo jamaa yangu wewe mpaka usome law school ndio utahisi umeyapatia maisha kabisa!!!!!.

ni muda muafaka kujua kwamba si lazima sana kuishi ndoto zako,embu badili mtazamo.

Hapana mkuu, hata sasa ni miaka miwili imeisha niko nje ya mfumo wa ndoto zangu, nimeuoña uhalisia mitaani, na nimefanya hesabu zangu kamili kwa hakika nna staili kua pale ili nitimize ndoto zangu kwa uwepesi zaidi na nna deni kubwa sanaa, kuna wakati niliwai kukamtwa uzururaji usiku mambo niliyoyakuta polisi yalinitia hasira sanaa ya kusaidia mamia ya watu wanaonewa uko, kwanin niliache hili lipite mkuu? Miaka minne chuoni iende tu bure?
 
Kuelewa tatizo lako ni mwanzo wa ufahamu,na kuweka tatizo lako hapa ni mwanzo wa mafanikio,watu wengi wamepitia vipindi vigumu mpaka wakafika hapo walipo,

Endelea kuvumilia tu mkuu na huenda hapa ukapata msaada wa kimawazo,kimali au kazi yeyote,endelea kumuomba Mungu na kumuamini hii ni mitihani ya dunia tu na haya yote yatapita.

Mkuu nakushkuru sana
 
Daah pole sana mkuu , wakati mwingine inaumiza.

Ila unajua nn ?wala usiumie kuwaona wenzako waendelea na shule uku ww upo kitaa.

Mungu ni waajabu sana , Mungu anamambo makubwa makubwa na mazito na matamu anayompangia mtu nakatika wakati wake.

Wenzako watamaliza mapema lkn chakushangaza Kupata kazi bado itakua shida , kuna wengine watakufa mara baada ya kumaliza ,wengine wanapata magonjwa mazito mazito ,, LAKINI WEWE SIKU ILE TU UTAKAPOMALIZA , TAYARI MAHALI FULANI UTAHITAJIKA ON THE SPOT KUANZA KAZI NAUKIWA MWENYE AFYA NJEMA KABISAAA.

usione unachelewa ,usijilaani , niivi tu hujui nikitu gan Mungu anakuepusha nacho ,, laiti ungejua nahakika Kabisa ungesema ASANTE MUNGU.

Yangu nihayo ndugu ,, kuhusu kupeana Channel za kutafutia kisalio , ngoja ngoja nitakushtua .

uzi nmeusasikiraibu.
 
Kuelewa tatizo lako ni mwanzo wa ufahamu,na kuweka tatizo lako hapa ni mwanzo wa mafanikio,watu wengi wamepitia vipindi vigumu mpaka wakafika hapo walipo,

Endelea kuvumilia tu mkuu na huenda hapa ukapata msaada wa kimawazo,kimali au kazi yeyote,endelea kumuomba Mungu na kumuamini hii ni mitihani ya dunia tu na haya yote yatapita.
Very encouraging words from you brother, God bless you. Nasikitika kusoma michango ya kejeri kwa baadhi ya watu kumuhusu mleta UZI; Huyu anahitaji FARAJA hata ya maneno tu.
 
Daah pole sana mkuu , wakati mwingine inaumiza.

Ila unajua nn ?wala usiumie kuwaona wenzako waendelea na shule uku ww upo kitaa.

Mungu ni waajabu sana , Mungu anamambo makubwa makubwa na mazito na matamu anayompangia mtu nakatika wakati wake.

Wenzako watamaliza mapema lkn chakushangaza Kupata kazi bado itakua shida , kuna wengine watakufa mara baada ya kumaliza ,wengine wanapata magonjwa mazito mazito ,, LAKINI WEWE SIKU ILE TU UTAKAPOMALIZA , TAYARI MAHALI FULANI UTAHITAJIKA ON THE SPOT KUANZA KAZI NAUKIWA MWENYE AFYA NJEMA KABISAAA.

usione unachelewa ,usijilaani , niivi tu hujui nikitu gan Mungu anakuepusha nacho ,, laiti ungejua nahakika Kabisa ungesema ASANTE MUNGU.

Yangu nihayo ndugu ,, kuhusu kupeana Channel za kutafutia kisalio , ngoja ngoja nitakushtua .

uzi nmeusasikiraibu.

Mkuu wangu nimefarijika sanaa na maneno haya, ubarikiwe sana sanaa sanaa mkuu, nimekua nikiombea sana uwepo wa siku za namna hii may b zitakuja siku moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom