Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 1,726
- 3,367
Kuna mtu ukimpa au kumwachia kitu chochote iwe ni kikombe, sahani, bakuli, baskeli, pafyumu, kichanio, mbuzi ya nazi, gari, jiko, sufuria, beseni yani kitu chochote kile basi uwe na uhakika LAZIMA hicho kitu atakiharibu au kitaharibika kikiwa mikononi mwake.
Cha ajabu unakuta kitu husika ni kizima kabisa yani hakina tatizo lolote na nyinyi wengine mnakitumia au mmekuwa mkitumia kitu ichoicho bila shida yoyote tena kwa muda wote hadi kilipokutana na muharibifu.
Muharibifu haitaji awe ametumia kifaa au kitu husika kwa muda mreeefu, anaweza kukigusa tu kitu husika ukashangaa apoapo kimeharibika pakubwa sana au hakifanyi kazi tena mara baada ya kukugwa au kuwa mkononi mwa mharibifu.
Wakuu mmeshakutana na watu wa aina hii?
Je, watu hawa wana nini ndani yao?
Je kuna roho chafu au ni bahati mbaya tu ndio zinawakutanisha wahusika na matukio haya hasi?
Je, kwenye mahusiano kuna watu kama hawa?
Wanasaidikaje?