Wema ni akiba na hazina pia!

Wema ni akiba na hazina pia!

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,401
Reaction score
7,900
Kijana mmoja wa Kiume alikuwa akipita nyumba moja hadi nyingine kulilisha tumbo lake lililokuwa na njaa, mwishoe akaamua kuomba chakula katika nyumba iliyofuata. Lakini Katika hiyo nyumba alishindwa kutimiza dhamira yake pale binti mzuri na Mrembo alipofungua mlango, kijana badala ya kuomba Chakula aliomba glass ya maji.

Binti alimtazama na aligundua kijana yule alikuwa na njaa sana, binti alimletea maziwa na Viazi vitamu, Kijana aliketi na Kula.baada ya kumaliza akauliza "Unanidai kiasi gani kwa hichi ulichonipa?" binti alijibu "Sikudai chochote kwani Mama alitufunza tusikubali malipo kwa Jambo la fadhira" kijana Alimshukuru sana kisha aliondoka.

Miaka Mingi ikapita yule binti sasa ni Mwanamke, alipata maradhi mabaya na madaktari wa sehemu ile walishindwa kumtibu na kushauri apelekwe mjini kwa madaktari Bingwa. Alipofikishwa Mjini alikuwepo Daktari aliyeitwa Dr. Rajab, Daktari huyu alipewa taarifa za mgonjwa na Kuelezwa anapotoka, Dr. Rajab aliposikia hivyo alikumbuka kitu.

Mara moja aliinuka na kwenda chumba alichopo mgonjwa na alimtambua mara moja kisha akaamua kufanya kila awezalo kumponyesha mwanamke huyo. Jitihada kubwa ilifanyika na yule mwanamke alipona.

Dr. Rajab aliagiza ofisi impatie bill ya Mwisho ya mgonjwa , Aliitazama na akaandika maneno machache kisha Billi ikatumwa kwa mgonjwa.

Mgonjwa aliogopa kuisoma maana alijua anadaiwa pesa nyingi sana na Asingemudu kuzilipa zote. Kwa Kujing'ang'aniza sana alisoma, alikuta maneno yameandikwa "billi yako Imelipiwa kikamilifu na Kikombe cha Maziwa na Viazi vitamu".... Machozi yalimtiririka sana alipokumbuka Tendo la fadhira alilofanya Siku za nyuma.

FUNZO
Ndugu Tendo lolote la fadhira unalolitenda halipotei,hujirudia kwa Namna tofauti hivyo tuweni watu wakujitolea kwa ajiri ya wengine , tuwe watenda mema, maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mwenyezi Mungu.
TUPENDANE[emoji120][emoji120]
 
Uzi mzuri sana ili mwandishi amekosa utulivu alipotupeleka kwa Dr Rajab ilikuweje mpaka jamaa amekuwa daktari lakini pia namna alivyopatq taarifa yamgonjwa wa kutoka kijiji ambacho pengine daktari huyo ametokea pia,
 
Back
Top Bottom