Wema huponza

Wema huponza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Rafiki yangu na jirani yangu hapa nyumba ya pili, tarehe 08/07/18 alipokea simu kutoka kwa shost kuwa ana matatizo na mumewe anaomba aje alale mpaka kesho yake. Shost alijitoa kwenda kumchukua anamkuta mdada kapigwa uso ni wa blue.

Walikwenda polisi ili wapate PF3 ya matibabu. Wiki ya kwanza waliuguza michubuko. Wiki ya pili akipiga simu mume hataki hata kupokea. Amemwambia aendelee na maisha yake, yeye yuko fine kulea watoto wake.

Jirani hapa ananipa kuwa hakutegemea kama ungekuwa ni ugeni wa miezi miwili na hajui ataondoka lini. Kinachochosha ni kuwa shost akitoka kazini mgeni ndiyo anaanza leo nimepiga hakupokea, nimempigia baba mchungaji awaite wazee wa kanisa waongee nae.

Tumemshauri hata kama anampenda sana mumewe kwa muda huu aache kumpigia kwanza.

Wema huu unaponza.
 
Rafiki yangu na jirani yangu hapa nyumba ya pili, tarehe 08/07/18 alipokea simu kutoka kwa shost kuwa ana matatizo na mumewe anaomba aje alale mpaka kesho yake. Shost alijitoa kwenda kumchukua anamkuta mdada kapigwa uso ni wa blue.

Walikwenda polisi ili wapate PF3 ya matibabu. Wiki ya kwanza waliuguza michubuko. Wiki ya pili ski pigs simu mume hataki hata kupokea. Amemwambia aendelee na maisha yake, yeye yuko fine kulea watoto wake.

Jirani hapa ananipa kuwa hakutegemea kama ungekuwa ni ugeni wa miezi miwili na hajui ataindoka lini. Kinachochosha ni kuwa shost akitoka kazini mgeni ndiyo anaanza leo nimepiga hakupokea, nimempigia baba mchungaji awaite wazee wa kanisa waongee nae.

Tumemshauri hata kama anampenda sana mumewe kwa muda huu aache kumpigia kwanza.

Wema huu unaponza.
Ukiona hivyo ujue mwanamke atakuwa anatambua makosa aliyomtendea jamaa, na mwanaume kama hataki kabisa hapo ameshamchoka bibiye anataka kuleta kifaa kipya
 
Kabila gani huyo bi shost,maana kuna makabila mengine ukimkaribisha mmoja anaita na ndugu zake.
 
Ukiona hivyo ujue mwanamke atakuwa anatambua makosa aliyomtendea jamaa, na mwanaume kama hataki kabisa hapo ameshamchoka bibiye anataka kuleta kifaa kipya
Sasa hapa alipojibanza walijua mume angekuja the following day tena na magoti sasa ni mwezi wa pili anakula na kulala bure
 
Wanaume sikuhizi hawataki mchezo, bibiye aende kwao hata mm huwezi ukakaa kwa rafiki yako hafu utegemee nije kuongelea hapo
 
Sasa kama kosa ni kuchepuka atawaelezaje wazazi wake?
 
Mwanamke alichepuka? Lo! Hapo kama jamaa anaushaidi na anaendelea kukaa kwa rafiki itaonekana rafiki ndo kamharibu, kama jamaa anakinyaa kama nilichonacho mm ndo imetoka bibiye atakuwa single mam
 
Hawezi kuwa single mother baba amebaki na watoto miaka 3 na mmoja
 
Rafiki yangu na jirani yangu hapa nyumba ya pili, tarehe 08/07/18 alipokea simu kutoka kwa shost kuwa ana matatizo na mumewe anaomba aje alale mpaka kesho yake. Shost alijitoa kwenda kumchukua anamkuta mdada kapigwa uso ni wa blue.

Walikwenda polisi ili wapate PF3 ya matibabu. Wiki ya kwanza waliuguza michubuko. Wiki ya pili akipiga simu mume hataki hata kupokea. Amemwambia aendelee na maisha yake, yeye yuko fine kulea watoto wake.

Jirani hapa ananipa kuwa hakutegemea kama ungekuwa ni ugeni wa miezi miwili na hajui ataindoka lini. Kinachochosha ni kuwa shost akitoka kazini mgeni ndiyo anaanza leo nimepiga hakupokea, nimempigia baba mchungaji awaite wazee wa kanisa waongee nae.

Tumemshauri hata kama anampenda sana mumewe kwa muda huu aache kumpigia kwanza.

Wema huu unaponza.
Ugeni wa muda mrefu huwa unakela sana,au mtu anakuja unaona week imekata hana hata mpango wa kuondoka
 
Mume wa shemeji yangu alifukuzwa kazi na akapoteza kila kitu muhimu yakiwemo marupurupu ya safari na ana watoto watatu.

Wakaja kwangu na kuniomba sana ikiwa nitawaruhusu wakae kwa muda huku akitafuta kazi ingine.

Ilipita miezi 10 kabla ya mimi kuanza kuona kwamba huenda ntaishia kulea familia mbili za watu zaidi ya 10

Ila kila anapokwenda huyo jamaa kazi hapati na mkewe kazi hana na alikuwa akimtegemea yeye.

Nikapiga moyo konde na nikamtafutia kazi huko kwao (Iringa) na kumpangia nyumba kwa miezi sita ya kuanzia na nikawalipia nauli waende huko.

Cha ajabu akawa anakataa kazi hiyo na anadai anataka kuishi Dar na ataendelea kuishi kwangu hadi atakapopata kazi.

Nilipochachamaa na mke wangu ndipo kwa shingo upande wakaondoka na kazi anaendelea nayo huko Iringa lakini hatuzungumzi kwa uzuri kisa, nimekataa asikae kwangu na amesahahu amekaa kwangu miezi zaidi ya 10 akiwa anakula na kukaa bure.
 
Hongera sana miezi kumi! Mungu akuzidishie
 
Ahsante sana

Miezi kumi, mimi nasomesha, kila kitu ndani kilifanywa mara 3, nauli ya jamaa kuhangaika na daladala mjini, ada za shule za watoto.

Bahati watoto wake walikuwa wa kwanza hazidi 7 hivyo huyo nimemchukua atakuwa anasoma na wenzie.

Ila bado naonekana mjerumani mbele ya jamaa kisa . nimekataa asiishi Dar.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom