Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,430
SOKO LA NYUMBA NCHINI TANZANIA;
(RESIDENTIAL MARKET)
Soko la Nyumba nchini Tanzania limetawaliwa na Wamiliki binafsi (Wananchi) wa Tanzania na Mashirika ya Umma(NHC, NSSF na TBA).
WAHUSIKA WAKUU:-
1.Wamiliki wa Nyumba zisizo na Upimaji ( Individual Unsurveyed Dwellings )=70.00% Mfano Nyumba za Vijijini na baadhi ya Miji ambazo ni Nyumba Kuukuu &Kongwe)
2. Wamiliki wa Nyumba zenye Upimaji ( Individual Surveyed Dwellings)=13.50% Mfano Nyumba za Mijini.
3.Shirika la Nyumba la TAIFA( National Housing Corporation )=5.10%
4.Makampuni/Wawekeza &Waendelezaji binafsi ( Real Estate Developers)=3.90%
5.Serikali Kuu( Central Government)=3.00%
6.MIFUKO YA JAMII ( Pension Institutions such as NSSF &PSSSF )=2.40%
7.Serikali za Mitaa ( Local Government)=2.10%
KWA NINI UWEKEZE KWENYE NYUMBA/MAKAZI :
1. Ongezeko kubwa la Watu, Inakadiriwa 2050 Idadi ya Watu itakuwa mara mbili ya idadi ya watu leo hii, hivyo soko la Nyumba bado ni kubwa mno. Kwa sababu Watu zaidi ya Million 100 watahitaji Nyumba za Kuishi ( Binafsi au Kupanga)
2. Hitaji la Nyumba zenye muonekano wa Kisasa:, Kutokana na kuongezeka kwa Watu wa Kipato cha Kati na Juu inapelekea kuwa na hitaji la Nyumba za Kisasa. Mfano Mijini baadhi ya Nyumba hazina Mvuto kwa Wanunuzi na Wapangaji.
3.Kasi ya Kukua kwa Miji Mikubwa na Midogo, Miji Mikubwa inakuwa ( Majiji kama Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya n.k.) na Maeneo ya Vijijini yanakuwa kutokana na Kasi ya Maendeleo nchini . Mfano kuongezeka kwa Mamlaka ya Miji Midogo kila Wilaya.
4.Mchango wa Serikali na BENKI kukuza Makazi: Kutokana na Hitaji kubwa la Nyumba za KUISHI, Serikali imeagiza Benki zote nchini kuwe na Mikopo( Mortgages) ya Nyumba za Kuishi. Mfano MAKAZI LOAN ya NMB , n.k.
5.MUINGILIANO NA MATAIFA JIRANI: Kutokana na Utulivu wa Kisiasa na Amani unavutia Wageni kuja kufanya Uwekezaji mbalimbali na kuhitaji Nyumba za Kuishi aidha kwa muda mfupi au zaidi.
KUMBUKA: Hitaji la Nyumba nchini ni kubwa na litakuwa kubwa sana kutokana na kuhitajika kwa Nyumba tofauti tofauti kulingana na sifa husika.