Wekeza Kwa ndugu zako usaidiwe Majukumu!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,518
6,497
Jamii zetu nyingi ni masikini na ni watu wachache Sana ambao ndio wamefanikiwa na hivyo kuwafanya wawe na majukumu mengi Sana katika ukoo....na kuwafanya wawe kimbilio ktk maswala mbali mbali yawe ya furaha na kuhuzunisha.

Na kibaya Zaidi ni kama vile watu hawa waliofanikiwa wanainjoi Sana kuwa wabwana wakubwa ktk ukoo au jamii Yao inayo wazunguka.....najua hapo akili yako imekliki paap je kwanini nasema hivyo! Relax....kama kawaida nyuzi zangu huwa zinasindikizwa na maudambu udambu...kamata popcorn au tende twende pamoja...

Naam wanapenda kuitwa mabwana wakubwa kwasababu....Ile Hali ya watu kuwafuata fuata na Kulia shida kwao wanaona raaaha Yani buruuudani! Yaani mtu akimcheki yeye kuwa ''anko Leo sipo vizur hata hela ya kula sina tafadhali naomba msaada wako'' wanapenda Sana yale mambo.....au ''brother Ada ya mwanangu imepelea naomba msaada wako'' ofcoz mifano IPO mingi Sana nadhani hata wenyewe mnaijua Sana Tu.

Na wengi wao kwakuwa wanapenda ukubwa ktk ukoo matokeo yake wanashindwa kuwasaidia ndugu kutoka kimaisha...ili waendelee kulambwa miguu kila siku ktk ukoo wao...kwasababu wengi wakifanikiwa ukubwa unaisha!

Napenda kuwashauri hawa mabwana kuwa hakuna ufahari wowote WA kuendelea kuwa hivyo kumbuka kuna kufa na kuna Leo na kesho....vipi mara paap! Kazi huna tena au biashara imeanguka hamuoni kwamba hapo ndo ukoo mzima umeanguka?

Ebu badilikeni sasa...Una uwezo wa kusomesha ndugu zako fanya hivyo,unauwezo wa kumpa mtu mtaji WA biashara fanya hivyo...Una konection ya kazi sehemu mpachike ndugu Yao aweze kujisimamia na kuendesha Maisha yake....hii itasaidia kuinua uchumi wa ukoo wenu na kesho au kesho kutwa mnasaidiana ktk majukumu mbali mbali na kukuondolea mzigo mzito ambao ulikuwa unaubeba wewe mwenyewe. Na kumbuka hata Kwa Mwenyezi Mungu utapata fungu lako kwani kusaidia watu ni IBADA.

Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) alipohama kutoka Makka kwenda Madina....alimtengenezea mazingira swahaba wake mmoja aliyeambatana naye ili ajikwamue kimaisha au Kwa lugha ya sasa alimtafutia connection! Alikuwa Anaitwa Abdallarahmani raufu kama nitakuwa nimekosea hili Jina naomba nirekebishwe....sasa pale Madina kulikuwa kuna mtu mmoja Anaitwa Abu sadi...huyu alikuwa miongoni mwa matajiri wa pale Madina.

Basi Mjumbe wa Mwenyezi akamwambia Yule Tajir kuwa...nakukabidhi huyu bwana Abdallahraman umsimamie malazi yake na Kula yake...basi Yule Tajir hakuchukua uamuzi wa kukaa naye pale nyumbani na kumlisha na kumpa sehemu ya kulala Ila alitaka Ampe ndoano avue samaki mwenyewe...hakutaka ubwana ukubwa!

Cha Kwanza alimwambia ndugu yangu Nina wake wawili hapa basi chagua yoyote unayempenda Kati Yao kisha Mimi nitamuacha kisha umuoe wewe...najua baadhi yenu msio waislamu mnaweza shangaa daah inakuwaje tena jamaa anampa mwamba achague mke wake? Hayo yalikuwa mambo ya kawaida Sana Kwa waislamu kufanyiana kipindi kile ambacho waislamu walipotoka Makka kwenda Madina kukimbia mateso waliyokuwa wanafanyiwa na washirikina wa Makka....kwahiyo ndugu zao wa Madina waliwakirimu kwa kuwapa wake zao...tena sio kwamba labda anamwacha mke Fulani na kumpa ndugu yake muislamu laa! Bali anamwambia chagua unayempenda wewe nimwache umuoe Mashallah walikuwa wakarimu Sana...

Pili yule Tajiri akamwambia...katika hii Mali yangu...nitaigawa nusu mbili,moja yako na moja yangu tuendeshe Maisha yetu...ebu angalia jinsi hawa watu WA enzi zile wenye hofu ya Mungu walivyokuwa wanajali! Lkn ndugu yako Tu anakuomba laki mbili ya mtaji unamnyima na uwezo huo unao...pumbavu Sana! Lakini Yule anayesaidiwa akamwambia mwenyeji wake naomba tu unionyeshe soko lipo wapi penye kuuza na kununua Kwa maana akafanye biashara na hakuhitaji hela zake...ingawa huenda alimpa cha kuanzia biashara au mtaji.

Undugu ni kusaidiana kuonyeshana njia....kupeana ramani na kupeana ushauri ili wote msonge mbele na si kuwabania wenzako ili ubakie bwana mkubwa na kupata sifa za kijinga.

Ni hayo tu
 
Mkuu Bey, amani iwe kwako. Shukran sana kwa uzi huu. Haya mambo yapo sana. Hawa mabwana huenda mbali zaidi kwa kuhakikisha hakuna ndugu anaetishia ubwana wao. Yan wale ndugu zake wanaopambana na kuonesha angalau wanamkaribia kipato, anakuwa tayari kuwaharibia kwa njia yoyote ile ili kuwadidimiza na yeye abaki kileleni daima aendelee kuabudiwa. Huu ni ujinga na upumbavu wa kiwango cha kimataifa. Harafu utakuta mara nyingi ni huku kwetu tu watu weusi kwa baadhi ya makabila. Hovyo sana.
 
Lipo sana hilo

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Bey, amani iwe kwako. Shukran sana kwa uzi huu. Haya mambo yapo sana. Hawa mabwana huenda mbali zaidi kwa kuhakikisha hakuna ndugu anaetishia ubwana wao. Yan wale ndugu zake wanaopambana na kuonesha angalau wanamkaribia kipato, anakuwa tayari kuwaharibia kwa njia yoyote ile ili kuwadidimiza na yeye abaki kileleni daima aendelee kuabudiwa. Huu ni ujinga na upumbavu wa kiwango cha kimataifa. Harafu utakuta mara nyingi ni huku kwetu tu watu weusi kwa baadhi ya makabila. Hovyo sana.
Futa hayo mawazo kichwani mwako. Kwa nini usijiangaishe na wewe ukawa mkubwa na kumiliki chako. Kuna msemo unasema mtumaini cha nduguye ufa maskini

Kama ukiamua kutotegemea mtu na ukalomaa unatoboa kirahisi tatizo mnategemea sana watu/ndugu wakati nao wana matatizo yao.

Mie hata ningekuwa na ndugu Rais nisingebweteka
 
Sina hakika kama umenielewa mkuu.
Haya. Mfano ndugu yako yuko juu na uwezo wake kiuchumi, ila wewe hata humtegemei yeye, unapambana kivyako, sasa umeanza kuzipata kiasi kwamba umeanza kumkaribia hivyo yeye anaanza kuwa na hofu kwamba sasa heshima yake itapungua akipata ndugu mwingine mwenye uwezo, anajaribu kukuangusha usifanikiwe mathalan anakuuzia gari ambalo anajua kabisa ni bovu ili ukilinunua likuhangaishe hadi uishe kabs au likupotezee muda na pesa nyingi udidimie. Ndugu wa aina hii ndio nimewazungumzia mimi. Hawafai kabs.
 
Amani iwe kwako pia Ndugudu ...

Ni mtihani Sana kwakweli....badala ya kufurahi ndugu zako wakiinuka wao ndio Kwanza wanataka kukugandamiza...halafu baadae wanaona Raha kujisifia ''mimi bwana ndio nilikuwa tegemeo la ukoo mzima....nimewasaidia Sana mimi''.....yaani ujinga mtupu mkuu
 
Nadhani umemiss the point mkuu...ishu wala sio kubweteka....Bali ni kupeana kampani....hata ukiamua kuhangaika kivyako lkn kuna mtu mahali Fulani ima atakuonyesha njia au kusaidia Kwa namna moja ama nyingine....je kwanini mambo hayo asikufanyie ndugu yako kama anauwezo nayo?
 
Saana yan mkuu, hayajielewi kabs.
 
Sina hakika kama umenielewa mkuu.
Haya. Mfano ndugu yako yuko juu na uwezo wake kiuchumi, ila wewe hata humtegemei yeye, unapambana kivyako, sasa umeanza kuzipata kiasi kwamba umeanza kumkaribia hivyo yeye anaanza kuwa na hofu kwamba sasa heshima yake itapungua akipata ndugu mwingine mwenye uwezo, anajaribu kukuangusha usifanikiwe mathalan anakuuzia gari ambalo anajua kabisa ni bovu ili ukilinunua likuhangaishe hadi uishe kabs au likupotezee muda na pesa nyingi udidimie. Ndugu wa aina hii ndio nimewazungumzia mimi. Hawafai kabs.
Sasa utanunuaje gari kwa ndugu yako wakati umehamua kujitegemea kwenye maisha yako. Ondoa hiyo mentality maana hata kununua gari kwa ndugu ni sehemu ya kutegemea vya ndugu.

Badilika mzee nakushauri. Simama wewe kama wewe na amini ndugu hawezi kukuangusha kama hujihusishi nae au kumtegemea/ Usimpe adui yako plans zako wala malengo yako na pia usimweke karibu mtu ambaye una mashaka nae.

Maisha yana kanuni zake za kibabe ili uweze kutoboa ukiendekeza sana ndugu haswa maskini hutoboi maana utakuwa na mentality ya kimaskini
 
Nadhani umemiss the point mkuu...ishu wala sio kubweteka....Bali ni kupeana kampani....hata ukiamua kuhangaika kivyako lkn kuna mtu mahali Fulani ima atakuonyesha njia au kusaidia Kwa namna moja ama nyingine....je kwanini mambo hayo asikufanyie ndugu yako kama anauwezo nayo?
Sijamiss point yoyote. Nachokisema nimekiishi na nilihamua kufuata yangu na nimefanikiwa sana kimaisha ukilinganisha na watanzania wengi sana na nimewasaidia ndugu kwa mipaka kwa kuwa ukifungua milango kwa kila mtu ni tatizo kubwa sana

Nasaidia mtu lakini akiwa huko huko kwake na simzogezi karibu kwa kuwa wengi wanataka kula samaki bila kujifunza kuvua samaki

Nina miradi ambayo ndugu zangu walifilisi kabisa mpk nilihamua kutumia approach nyingine. Hapa nilipo nasomesha watoto watatu wa ndugu zangu na mmoja wa baba yangu alizaa uzeeni.

Tanzania ukiwa na uwezo na moyo wa huruma, nyumbani kwako kunaweza kugeuka kituo cha kulelea watu wazima waliobweteka kimaisha. Nililiona hilo mwanzo kabisa na niliweka kanuni za maisha

Ulevi na uzinzi wa ndugu zinarudisha nyuma sana wenzao katika familia zetu za kitanzania. Nimeongea machache tu kutoa sumu mwilini ila muhimu tufanye kazi na kujitegemea wenyewe na tuache kutegemea ndugu
 
Jamii zetu nyingi ni masikini na ni watu wachache Sana ambao ndio wamefanikiwa na hivyo kuwafanya wawe na majukumu mengi Sana katika ukoo....na kuwafanya wawe kimbilio ktk maswala mbali mbali yawe ya furaha na kuhuzunisha.

Na kibaya Zaidi ni kama vile watu hawa waliofanikiwa wanainjoi Sana kuwa wabwana wakubwa ktk ukoo au jamii Yao inayo wazunguka.....najua hapo akili yako imekliki paap je kwanini nasema hivyo! Relax....kama kawaida nyuzi zangu huwa zinasindikizwa na maudambu udambu...kamata popcorn au tende twende pamoja...

Naam wanapenda kuitwa mabwana wakubwa kwasababu....Ile Hali ya watu kuwafuata fuata na Kulia shida kwao wanaona raaaha Yani buruuudani! Yaani mtu akimcheki yeye kuwa ''anko Leo sipo vizur hata hela ya kula sina tafadhali naomba msaada wako'' wanapenda Sana yale mambo.....au ''brother Ada ya mwanangu imepelea naomba msaada wako'' ofcoz mifano IPO mingi Sana nadhani hata wenyewe mnaijua Sana Tu.

Na wengi wao kwakuwa wanapenda ukubwa ktk ukoo matokeo yake wanashindwa kuwasaidia ndugu kutoka kimaisha...ili waendelee kulambwa miguu kila siku ktk ukoo wao...kwasababu wengi wakifanikiwa ukubwa unaisha!

Napenda kuwashauri hawa mabwana kuwa hakuna ufahari wowote WA kuendelea kuwa hivyo kumbuka kuna kufa na kuna Leo na kesho....vipi mara paap! Kazi huna tena au biashara imeanguka hamuoni kwamba hapo ndo ukoo mzima umeanguka?

Ebu badilikeni sasa...Una uwezo wa kusomesha ndugu zako fanya hivyo,unauwezo wa kumpa mtu mtaji WA biashara fanya hivyo...Una konection ya kazi sehemu mpachike ndugu Yao aweze kujisimamia na kuendesha Maisha yake....hii itasaidia kuinua uchumi wa ukoo wenu na kesho au kesho kutwa mnasaidiana ktk majukumu mbali mbali na kukuondolea mzigo mzito ambao ulikuwa unaubeba wewe mwenyewe. Na kumbuka hata Kwa Mwenyezi Mungu utapata fungu lako kwani kusaidia watu ni IBADA.

Mtume Muhammad (rehma na Amani ziwe juu yake) alipohama kutoka Makka kwenda Madina....alimtengenezea mazingira swahaba wake mmoja aliyeambatana naye ili ajikwamue kimaisha au Kwa lugha ya sasa alimtafutia connection! Alikuwa Anaitwa Abdallarahmani raufu kama nitakuwa nimekosea hili Jina naomba nirekebishwe....sasa pale Madina kulikuwa kuna mtu mmoja Anaitwa Abu sadi...huyu alikuwa miongoni mwa matajiri wa pale Madina.

Basi Mjumbe wa Mwenyezi akamwambia Yule Tajir kuwa...nakukabidhi huyu bwana Abdallahraman umsimamie malazi yake na Kula yake...basi Yule Tajir hakuchukua uamuzi wa kukaa naye pale nyumbani na kumlisha na kumpa sehemu ya kulala Ila alitaka Ampe ndoano avue samaki mwenyewe...hakutaka ubwana ukubwa!

Cha Kwanza alimwambia ndugu yangu Nina wake wawili hapa basi chagua yoyote unayempenda Kati Yao kisha Mimi nitamuacha kisha umuoe wewe...najua baadhi yenu msio waislamu mnaweza shangaa daah inakuwaje tena jamaa anampa mwamba achague mke wake? Hayo yalikuwa mambo ya kawaida Sana Kwa waislamu kufanyiana kipindi kile ambacho waislamu walipotoka Makka kwenda Madina kukimbia mateso waliyokuwa wanafanyiwa na washirikina wa Makka....kwahiyo ndugu zao wa Madina waliwakirimu kwa kuwapa wake zao...tena sio kwamba labda anamwacha mke Fulani na kumpa ndugu yake muislamu laa! Bali anamwambia chagua unayempenda wewe nimwache umuoe Mashallah walikuwa wakarimu Sana...

Pili yule Tajiri akamwambia...katika hii Mali yangu...nitaigawa nusu mbili,moja yako na moja yangu tuendeshe Maisha yetu...ebu angalia jinsi hawa watu WA enzi zile wenye hofu ya Mungu walivyokuwa wanajali! Lkn ndugu yako Tu anakuomba laki mbili ya mtaji unamnyima na uwezo huo unao...pumbavu Sana! Lakini Yule anayesaidiwa akamwambia mwenyeji wake naomba tu unionyeshe soko lipo wapi penye kuuza na kununua Kwa maana akafanye biashara na hakuhitaji hela zake...ingawa huenda alimpa cha kuanzia biashara au mtaji.

Undugu ni kusaidiana kuonyeshana njia....kupeana ramani na kupeana ushauri ili wote msonge mbele na si kuwabania wenzako ili ubakie bwana mkubwa na kupata sifa za kijinga.

Ni hayo tu
Wengi wetu tunapenda sana kutukuzwa
Kwahiyo kufanya hii kitu inahitaji akili ya ziada "Maono ya mbele"
 
Back
Top Bottom