Weekend story! BEN 10

Weekend story! BEN 10

Nimefika pale kituoni bado siamani amini, ila nisha jiandaa kwamba sio issue ndogo. Kilichonishangaza kwa mda ni kumkuta linda mule ndani. Na kiukweli she didnt look good at all. And she was the last person i needed. Mjue mpaka mi mtu mzima naamua kumchomeka bisu mtu mjue yalionikuta sio madogo.

Najua una hamu sanaa ya kujua kwanini nilimchoma kisu Hans naomba fundi utulize mshono huo. Ishu ilianzia mbali sanaa. Mnooo. Like evry other night mare inaanza kama story nzuri ila mwishowe ndo inakengeuka. Anyway ndo nishafanya nilichofanya wala sijutiii kabisaa. I never wanted to be a star, then i became a star overnight then now i am muderer overnight.

It all started baada ya Sam kunusurika kufumania kwa mara ya 2. Bado nilikuwa sitaki kumwambia. Bado nilikiwa na chekecha. Sam alishanifanyia umalaya sanaa yule boya. So design kama nalipiza vile twende aste aste chali yangu. Mambo yakikwenda yalivokwenda.

Bada ya Hans kuondoka nikaanza kumtongoza upyaaa. Hatakiii! Anauliza ushamwambia? Namwambia bado. Ndo mwisho wa mawasiliano. Nikakata tamaa, nikaamua kwa Sam kurudi siwezi, i am already past that with or without Hans. Na mimi nikaanza kumpotezea. Ikapita wiki kimya kimya. Nikasema duuuuh kweli ngoma ya kitoto haikeshi. Akaanza ungese wa kumpost mdada mwengine Insta. Nikasema naiweka wapi sura yangu. Kila mtu anajua niko na huyu shoga. Najuuuta. Nilimkumbuka Sam kwa asilimia 20 labda. Nika mu unfollow na kumblock kabisaa. Nikatoa oda akija dukani afukuzwe kabisaa. Sipendagi uhanisi.

Siku hio niko home, saa 7 nasikia mtu anafungua mlango. Nikajua yeye si ana funguo. Nikasema bora nimpore funguo zangu. Kumuonaaa ananilegezaga nguvu. Naona kama namuoneaaa sijui kwasababu ya umri wake. Nikaamua tu nikiache Diplomasia. Kaingia anaanza kuvua nguo. Nikamwambia vaa takataka zako acha funguo zangu sepaaa. Akauliza niende wapi sahizi? Nikamwambia kwa uliempost. Anisaidie na mimi kidogo maana tunapostiwa wote. Akaguna akamalizia kuvua nguo akaenda kuoga.

Mi nawaza hata mkononi hajai, mtu mwenyewe Skinny nikianza kupigana nae man to man hapa si namvunja mtu mwenyewe manzi wa chugga ariff. Ni shigidiii aisee. Akatoka kuoga. Nikamwambia Hans toooo toka kweliii! Anajikausha uchi uchi. Anasema tatizo Kyle unapenda ubabe sanaa, nitoke kivipiii? Kama kuchukia nilitakiwa nichukie mimi, bwana wako kanusurika kutufumania, afu kununa unanuna wewe. Sio fair hivo baby. Unalalamika post post. Haya ngalia video kamili unune vizuri sasa. Akanipa simu. Kumbe video vixen wa wimbo uleee alionisikilizisha.

Ikabidi nibadili gear angani, nilikumisi sanaa, afu ulivoniacha siku ile sivo sivo. Akazima taaa. Nikasema afadhaliii. Akaja, ananiambia leo nina ukamee sanaa, sijapiga show tangu siku ile. Design sijui tukaiendeleze pale pale.Namwambia hapa hapa. Anauliza ile post ilikutia wivuu. Najibu ndioo. Namwambia uka ni block kabisaa. Anasema ndio. Basi hapo ndo kunishika kwa hasiraa. Na mimi nina hasira zangu. Nilimmisi kiukweli sababu anajua kunifikisha pale napotaka kwendaa.

Tumeenda vizuri kabisaa kwa kasi ya 4g, nikachukua machine nijiwekee. Wote tuko speed 120. Hamu inaweza kuniua. Akaniuliza ulimwambia? Nikasema ndio. Ilibidi niseme ndio. Ningesema suuu show ingeishia pale. Akatabasamu, akaweka kidogooo ndo nikvurugikaa kabisaa, namwambia baby nipe yote. Akaniuliza akasemaje ulivomwambia. Nikamwambia kasema Poa tuuu, yeye hana shida kabisaa. Akauliza Sam ndo kasema hivo? Nikamwambia ndio baby. Akasema nakuja mara moja.

Nilichosikia ni mlio wa gari inaondoka njeee. Gademmmuuuuuu! Ndo nikajiona ndeziii! Sam kasema poa haina noma! Aiseee kama uwongo nimefeli vibaya vibaya. Jamanii! Nikawaza nikafanyane na mtu mwingine? Nalalaje hivo. Ila hawezi kunifanya kama dogo. Dogo anafanya. Siku ile niliuza mechi ila nilipakwa tushombo. Nikamtumia meseji sorry nilidanganya. Mi Sam namuogopa, labda tumwambie wote. Akajibu sawa. Panga mkutano mi nitamwambia. Namwambia rudi basi kimojaa tu cha kulalia. Akasema mpaka umwambie Sam.

Kikao hakikwenda shwari, balaa lilikuwa kubwa. Sam akawekwa ndani. Kiukweli Sam simpendi tena ila ni zaidi ya kaka angu. Nisingekubali alale ndani. Kumtoa siwezi. Nikampigia Linda akaenda kumtoa. Linda na Sam wanapendana mda sanaaaa. Maana tangu dukani Sam alikuwa anamkata jicho la kiume siku ya kwanza kabisaa. La matamanio. Bwana akiwa wako hata azuge vipi unamjua. Siku ya double date Sam hakuniambia Linda kamtongoza, nilihisi Sam kamtongoza nikamtega tu linda. Na Linda akawa anamkata jicho hilo hilo la loost Sam. Hata alivomkalia uchi dukani nilimuona vizuri.sema nishajikatia tamaa, kwa Sam nilifika bei. Mpaka wanatiana ukumbini niliiona ile, maana walipotea wote, nikaenda chooni nikawasikia. Na nikajifanya mjinga. Sasa jiulize kwa moyo wangu huu wa jiwe dogo kanifanya nini mpaka nimchomeke bisu? Kama haya yote nilivumilia. What i respect Sam ukiachaa tamaa tamaa za fisi nafasi yangu kwake ilibakia pale pale.

Tukarudi nyumbani, akatoka usiku huo huo. Akaja na bag 3 za nguo ndo kahamia jumla. Niliona poaaa tu manake ni unlimited game. Mimi tu. Ngombe ninae ndani, maziwa bwerere. Siku hio sitaisahau, tulipiga show leo usiku mpaka kesho saa 10, kazi ni moja tu. Hamu yote iliniisha. Niwekwa na insta live. Dogo alikuwa na mzukaa balaa. Nikaona haya ndo maishaa maishaaa. Maisha ndo haya.

Dogo anajua kupenda, anajua kuharibuuu. Yaani alivosema kujibana hawezi hawezi kweliii. Kumbi kumbi. Anajaliiii. Anamwambia mama yake kuhusu mimi mpaka basi. Mama kila siku jioni lazima apige simu. Mama akaniletea zawadi ya chupi. Nikawaza sanaa anasitiri anapopumzika mwanae , au mwanae kamwambia sina chupi, au upendo tu, au ndo kashazifanyia mambo ya kiswahili sikuelewa. Niliivaa lakini. Mama mkwe akawa mpaka shoga angu. Namvalisha mimi. Kumsindikiza sasa mpaka saluni. Nilitegemea ataniletea mambo ya mkubwa kwa mwanangu walaa.

Kumloga Hans umpende mama yake. Akiwakuta na mama yake hivi labda mnataka kwenda mahali atatoa burungutu lote la pesa mfukoni. Mama mtu mstaarabu. Sio mgumu kuishi nae kabisaa. Anatupikia mda mwengine, anamfulia mwanae mpaka mimi. Na anapenda mambo ya mjini balaa. I was happy na hii familia. Nikaona naweza kuishi na hii familia hata miaka 20. I was happy i had a family.

Acha surprise, nimekaa zangu dukani, akaja akaniambia baby leo nina pesaa. Nataka tutokee. Nikamwambia ngoja niende home nika chenchi, akasema hamna twende tukanunue nguo. Akanipeleka mwenywe dukani, nikachukua nguo, akalipiaa. Sio kitu kikubwa ila nilifarijika saanaaa. Anasema tuone ilivokaa. Akanikumbusha Sam tulivogongana na Linda.

Akaanza kusema nataka mtoto. Hasemi direct anachomeka ningekuwa na ka junior mda huu nakabeba beba.Nikamwambia mtoto na ndoa. Akasema kama upo tayari namwita sheikh anakutia maji, unakuwa Kayla tunachoma ubaniii. Nikamwambia dini sibadilishi. Akasema ndo maana mi sikutaka ubadilishe, nikataka mtoto. Dini mwenyewe ukirdhia kwa kunipenda kwako utabadilisha kwa nafsi yako. He was so sweet!

Nikaanza kuumwa umwa, mpaka ufunguzi wa kina linda sikuweza kwenda. Nilikuwa najisikia vibaya sanaa. Akaja mama mkwe akaniambia una mimba wewe. Nikapima nikakuta kweli. Sherehe wiki nzimaa. Jina limeanza kutolewaa. Nadekezwaa balaa. Mimba ukiwa na mtu anaejua thamani yake raha sanaa.

Ikabidi nisafiri, akasema huendi peke yako, na hali hii, twende wote. Visa alitafuta mwenyewe. Safari nzima aliniuguzaa, nikashukuru alikuja. Na alinitunza kwa kweli. Kufanya kama kawaidaa. Nikamwambia mtoto atatoka mchafuu. Tumefunga mizigo tumerudi salama.

Nyumbani sasa kwenye kufungua mizigo ndo balaa lilipoanziaaa. Ugomvi, ugomvi na wewe. Zilianza ngumiii msione mama kija mkajua nilimwachia, tumezichapa. Tatizo langu pigana yangu chovhote kilicho mbele yangu, na siku hio kisu kikombele yangu. Akakidaka, nilipambana mpaka nikamchoma cha tumbo. Midamu mwaaaa. Nikampigia mama mkwe nishamuua mwanao. Akaja na watu fastaaa, ndo kuita polisi. Nikaletwa huku.

Linda sikujua kaja kwa kesi gani, sikuwa na shobo nae. Yeyendo alianza kushoboka. Ananiuliza kwanini umemchoma kisu Hans. Nikamuuliza na Hans unamtaka, Sam ashakushinda? Akasema usitaje hilo jina, nimempiga risasi hivooo sema marehemu Sam, Ina lillah wa inaallah rajioon! Sikustukaa. Akasema mbona hustukii. Nikamwambia nistuke nini kwa mfano? Namjua malaya mbwa, wewe si ulitembea nae nikiwa nae. Itakuwa umemfumaa hajuagi kujificha.

Ukapita ukimyaa mrefuuu. Nikamuita afande shostiii! Akaja nambie shoga angu. Nakuonaga instaaa! Nikamwambia eeeh, naomba panadol shoga angu na simu nimpigie mtu. Akaleta. Linda akasema na mimi, akaambiwa kelele weeee na msonyo juu. Nikamwambia mpe yule shoga angu pia. Akasema hapo sawa. Akapewa. Akanipa simu. Nikapiga kwa mama mkwe, ananiambia bora tumemuwahiii, sasa kwanini kwani ilikuwaje? Nikamwambia mama story ndefu sanaa. Nashukuru kama mwanao mzima. Nisamehe mie. Ananiambia nitakuja kesho kukuletea chai.

Linda anasema mbona wewe una tritiwa kwa upendeleo. Nikamwambia mimi star, na victim wangu star, wewe no body. Simu nilikaa nayo usiku kucha. Nikawapigia nyumbani. Linda akaomba. Nikamnyima, baadae nikamuonea imani nikampa. Akapiga ofisini kwake kuwaambia alipo. Akawapigia na watu wengine. Baadae nikarudisha kwa shostiii. Akaniomba selfie, shoga usinipost nitadhalilika.

Linda akaniambia niambie ilikuwaje nikupe ushauri, unaweza kuwa star ila haupo juu ya sheria. Nikamwambia Linda pambana na hali yako. Mi siwezi kukubali lawyer muuaji anitete kesi ya mauaji. Mwenzio Star kesho napandishwa mahakamani wa kwanza. Wewe bado upo sanaa. Tutakutana Segerea tukijaaliwa. Nina mengi kichwani niache nitulie.

Kesho kweli nikapandishwa mahakama ya mkazi kisutu, nikikabiliwa na makosa 6. Shambulio la mwili, kula njama za mauaji, kijaribu kuua. Kujeruhi kwa silaha kali, domestic violance, uharibifu wa mali, Nikasomewa pale mashtaka yote, media zimejaaa kama zote.Nikaulizwa ofcourse i pled NOT GUILTY to all six counts. Nikaambiwa haki zangu pale. Na nikapelekwa segerea mpaka tarehe ya kuanza kusikilizwa kesi.

Raha ya jela uingie na kosa KUBWA KUBWA. Nimefika pale, nikapangiwa VIP si star. Na kila mtu akishoboka kosa gani? Mauaji. Naonekana namba tasaaa ariiif. Sio kabisaa. Mahakamani walijaa watu wa chugga, mzee wangu alikuwepo, alitia huruma sikumuangalia mara mbili. Maana ana ma pressure na hii ishu ilimkalia vibaya sanaa.

Baada ya wiki nikakutana na Linda yupo on general population, kakonda sanaa. Maisha ya huku hayakumpenda kabisaa. Akaniambia I DONT KNOW ABOUT YOU KYLE BUT I AM GETTING OUTOF HERE SOON, I MUST, I HAVE TOO.BY ANY MEANS.

ITAENDELEA.
 
Ama kweli kila mtu na siku yake na ile haikiwa siku yangu.Ndugu msomaji usiombe kulichungulia kaburi na kuta zake 4. Nimelichungulia mwenzio. Now that i have cheated death it is time to move things my way.

Sawa ndugu msomaji i might be a little bad maybe a little out of hand ila sio kwa kuuwa kivile. Mpaka sasa sina uhakika Linda alikuwa ananiua kweli au anatishia. Na kilichonikera ni kitendo cha kutaka kuniua na ku get away with it. Angekuwa anapanga kuniua na yeye ajiue ningemsamehe kiroho safi. Sio kupanga kuniua aendelee kula bata mjini hapa. Hilo haliwezekani.

Kiukweli hili tukio lilikuwa la kuogofya sanaaa. Kwanza Linda alipanga kuniua kweli. Ila kiuhalisia haikuwa murder bali ni homicide. Maana ile risasi ilionipata bara bara kwenye kiuno ikimiss uti wa mgongo kwa milimita kadhaa, na kukwangua baadhi ya pingili za mgongo kuzi twist ilifyatuka bahati mbaya. Novosema nime ki beep kifonaomba mnieleweeendugu wasomaji.

Kilichoniokoa ni yule mwanamke niliekuwa namchumisha mchicha aliniambia Linda namjuaaa. Atakutwanga risasi. Huyu bibie ni mjeshi kwa profession. Nikamwambia nammudu. Akasema twende wote mimi sitajitokeza nikiona pako shwari nitaondoka, nikiona chenga naingilia. I can not take risks.

Tukaenda wote mpaka nyumbani. Ni appartments zipo coumpound moja. Mbali mbali ila geti la kuingilia ni moja. Nikazama ndani na kukita hali si hali. Uzuri sikufunga mlango maana una door lock system, niliutegesha ndo mjeda akapata chance ya kuingia. Londa hukuwaza hii posibility. Aka m time na kumuambush. Tatizo ndo risasi ikanipurusa kiuno mgongo. Na kibaya haikutoka.

Nimekaa hospital mwezi hawaioni, kwenye xray wala nini. Maana nje haikutoka na ndani hawaioni. Nimeumwa ndugu msomaji nimeumwaaa sana. Mpaka mda huu afya yangu sio nzuri kabisaa. Niko dhaifuu. Mgongo unaniuma sanaaa, nashinda nimelala.

Mjeda akaja kuniambia ana mframe Linda for murder. Kiukweli nilikuwa undecided, mjeda ananiambia akitoka kule hatunaa bahatiiii. Yaani hatuna bahati. Lazima alipe kisasi. Na kisasi chake kitakuwa kibaya sanaa. Tuhakikishe tunammalizaa. Iwe siri yetu. After all i will get to keepthe bar.

Ila pia sikutaka kukubaliana na mjeda sanaa maana ingemaanisha naikomboa roho yangu toka kwa Linda na kuikabidhikwa mjeda. Bora Linda raia wa kawaida, mjeda huyu na uhanithiii wangu si ataniua na kunizika porini. Nitakuwa si solve kitu. Shit was already too deep.

Mjeda akanipa maelezo ya kuwapa polisi na maelezo hayo yakaonesha bayana ame tamper na crime scene. Kapandikiza ushidi sana. Kafoulisha mambo mengi. Mgongo mbovunabishana nae vipi? Nikatoa maelezo yake polisi.

Nikapata taarifa Kyle yuko Segerea. Sikufurahi ila nilifurahi. Adui muombee njaa. Na yeye ukame ukawa umemkumba. Nikaamua nikamuone huko huko sitakikuhadithiwa. Nikajikokota nimelala kiti cha nyuma, mpaka segerea. Nikafata taratibu nikaruhusiwa kumuona. Sikutegemea angekuja.

Alikuja. Tofautina nilivotarajia nitamkuta kakondeana, kachokaa. Nikamkuta kanenepa sanaa. Mwili wake mmbaya naujua ni mtu wa diet sana. Ila akawa kajiachia,ka relax. Kaja tumekaa dakika 5 bila kusemeshana. I wanted her to sayshewas sorry to me. Kanikosea sanaa arif afu mpaka mda huu design huo msamaha sijaupewa kabisaa.

Nilivvona kimya nikamuanza, maisha vipi? Akasema poa! Nikamuuliza Hans akuvumilia vishindo vyako akasanda maskini. Kaiga kunya kwa tembo sahivi msamba umembakia wazi. Akacheka. Nikamuuliza But WHY? Akabadilisha mada, akaniambia naona sasa umepata sizeyako. Sam chalii yangu ukiendkeza umalaya bado kupigwa risasi ya pumbu. Tukacheka wote.

Nikamwambia i am doing better, akasema ndo maana umekuja huku. Nikamuuliza tena but WHY? Akanitaza machoni akarudi zake gerezani. Nikabaki nimebungaa. Mara naona Linda anatoka kuja kwa mgeni wake. Tukagongana macho kama dakika 3 afu akaendelea na mishe zake. Nikaondoka. Jicho la Linda lilijaa roho mbayaa. Nikajua sona bahatii. Niliteemeka utumbo ndugu msomaji mpaka risasi nikaisikia mwilini inatembea.

Ilianza kusomwa kesi ya Kyle, nilienda mahakamani sio kwamba bado nampenda, hapanaaa! Namjua Kyle kama bimemzaa mimi sio wa kumchoma mtu kisu. Afu nimeishi nae 10 years na namjua ni mwema mnoo mnooo sio wa kwenda jela. Utu wake naujua mimi. Na mpaka sasa nikawa sijui sababu ni nini. Nikajua mahakamani sababu itatajwa tu.

Tofauti na nilivotegemea atasimamiwa na moja ya malawyer wa Linda haikuwa hivo kabisaa. Alisimamiwa na lawyermpya kabisaa kijana mtanashatialiejaa matashtiti. Sijui kamuokota wapi. Na alikana mashtaka yote 6.
Upande wa mashtaka ukaanza kwa kule ushahidi, wakaanza na Hans! Nilichogundua Kyle hakumuangalia hata mara moja. Nae afya yake ikazidi kuwa mbaya maana hana afya kwa kuanzia. Na kuumwa akabakia skeleton.

Hans is just a kid trying tobe a man. Maana kwenye kesi Hans alijua kuwala viboga waendesha mashtaka. Maana anasema yeye ashamsamehe na anaomba mahakama itupilie mbali hili shauri ulikuwa ugomvi wa kifamilia. Akaambiwa hii kesi sasa ya jinai. Haimalizwi kiholela.

Anaulizwa asema nini kilitokea. Akasema ulitokea ugomvi ndo bahati mbaya baby mama wake akamchoma kisu. Lawyer akamuuliza alikuchoma nusu robo au kisuu chote? Akasita! Akletewa picha ya tukio ajikumbushe akasema chote. Akaulizwa je kalichungulia kaburi ? Akasema ndio.

Upande wa Kyle lawyer wake akamuuliza Hans je kwanini Kyle alikuchoma kisu? Anasema ilikuwa hasira. Anaulizwa mlikuwa mnagombana, anasema ndio. Kuhusu nini? Anasema mambo tu ya kifamilia. Yapi? Akaanza tumbo linamuuma sanaa, unaona kabisa kakimbia swali. Daktari akasema ashushwe kizimbani kwa mda.

Akaulizwa kisu kilikuwa wapi kabla hajakuchoma? Alikifata jikoni akaja kukuchoma nacho? Au ilikuwaje? Akasema kisu kilikuwa chini, wanakatia box za dukani. So ni kama alikibumba kibahati bahati.

Akamuuliza tena je alipokishika, ulimuona ameshika kisu mkononi, wewe kwanini hukukimbia nje? Au chumbani, na hali ishakuwa tete. Naweza kusema wote mlikimbilia kisu, sema mteja wangu ndo akakiwahi na wewe hukuwa na bahati sana? Akasema alikuwa anaamini Kyle asi geweza kumchoma kisuuu hata mwisho wa dahari, na alimfata kum disarm.

Akamuuliza je kwa ujumla Kyle ni mtu mmbaya? Anaeweza kuua mtu? Akasema hapana haamini hivo hata baada ya kuchomwa bisu. Akamaliza mzee baba. Kesi ilikuwa imemkalia vibaya sanaa Kyle! Maana ushahidi upo.

Nikajaribu kumpeleleza Hans kuhusu sababu haswaa ya ugomvi wao hasemi kinachoeleweka. Mahakamani ndo nikajua Kyle mjamzitoo. Mimi nimekaa nae miaka 10 hakunizalia chochote, Hans hana nae mwaka anamzali. Bora walivochomana visu shwainiii.

Ikaanza kuso wa kesi yangu. Na mimi ndo shahidi namba moja. Usiombe ushitakiane na X wako. Linda kama nilivotegemea alikuwa represented na moja ya lawyers wake. Na mimi nikawa na lawyer wangu.

Nikapanda kizimbani. Lawyer wangu akaniuliza namjua mshatakiwa? Nikasema ndio! Je ndo mtu alienipiga risasi? Nikasema ndio. Akasema eleza ilikuwaje! Nikaeleza kuanzia narudi home. Risasi ya ukuta na ki note na pen nilivokuwa nalazimishwa niandike suicidenote. Akauliza jeLinda navoona anaweza kuua? Nikasema uwezo uo ashauonesha kwangu.

Upande wa mshtakiwa waliuliza kabla sijarudi home kilitokea nini? Nikasema fumanizi kiukweli! Wakauliza Linda alikuwa na hasira right,na alitaka kukuuajekwa kwanini hakukupiga risasi ya kichwa au moyo akupige kiunoni? Sikujibu ndugu msomajii. Wakauliza Na angle ya mlengaji wa hio risasi ni tata sanaa. Lawyer wangu akaleta objection juu ya swali la angle. Wakaniuliza kwanini Linda alizimia? Nikasema aliteleza labda sikumbuki it was too fast. Nikashushwa.

Kiukweliwanasheria wana mambomengi sanaa. Wanakupekenyua weeee mpaka basi. Nilivurugikaaa sio kidogo. Sijakaa sawa natakiwa kutoa ushahidi kesi ya Kyle! Upande wa mashtaka. Zile ngumi zetu zileeee washazinyapia nyapia. Sikujua kiundani ila nikaenda kutoa ushuhuda.

Waliniuliza je nilikaa uchumba na Kyle miaka mingapi? Nikasema 10. Nikaulizwa je domsetic violance sio tabia sugu ya mshtakiwa? Nikasema kwa mimi na yeye mimi ndo nilikuwa nampiga. Ilibidi nijiokoe ndugu msomaji kujifanya kidume. Wakaniuliza swali moja la kingese sana! Ilibaki kidogooo niwaulize nyie wangese nini? Aliuliza je mnaendeleza mahusiano na mtuhumiwa? Nikasema hapana! Akauliza je mimba ya Kyle ni yako? Kidogo niseme ndio kutibua tu vuziii. Nikasema hapana! Nikaulizwa je ulikuja kumuona jela juzi? Nikasema ndio. Naona Hans anajipanikosha kingese na nini. Akasema hana swali zaidi.

Nilisikia kitukimenikabaaa. Yaani sasa i akuwa Kyle kamchoma Hans kisu sababu yangu kweliii? Demu wangu anitombeee, amjaze kibendi afu ndo nini sasa anataka kufanya. Niliamua kutii sheriabila shurti.

Upande wa mshtakiwa Kyle wakaniuliza je mpaka napigwa risasi nilikuwa na date na nani na ana uhusiano gani na Kyle? Nikaelezea. Nikaulizwa maraya mwisho Kyle kukupigia simu lini? Nikasema sikumbuki. Nikaulizwa je naona Kyle na Hans uhusiano wao ulikuwa deepkiasi gani? Nikasema siwezi kujua! Wakauliza je navoona Kyle anaweza kumuua Hans? Nikasema sikutegemea ila nilishangaa. Nikashushwa.

The bar was running smooth, pesa nikawa naipata. Walau nimeamvulia hii bar. Akaja Mozah kutaka maongezi, nilivomuona tu nikajua sio ya kheri. Kikubwa alichokisema Linda anaomba nibadilishe statement yangu, nijifanye ni domestic violance,ileilikuwa homicide, apunguziwe mashtaka.

In return atanipa shareza bar 100 percent. Nikawaza sanaa! Sikupata jibu.

ITAENDELEA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom