Wedding Anniversary

Asante sana mdogo wangu, ni kweli ni jambo la kumshukuru Mungu

Amina..............kwakweli anastahili sifa kwa kukutumia wewe dada yangu kutuonesha kuwa bado inawezekana kuwa katika ndoa aliyobariki Mungu, japo wengi wanaidhalilisha taasisi ya ndoa Takatifu...........umenipa moyo kweli. Uzidi kubarikiwa
 
hongera sana FP Mungu awape baraka zake nyingi na muishi kwa upendo, amani, utulivu na uvumilivu kwani ndo silaha ya upendo wenu, sijui kama mna watoto basi Mungu awape wattoto matwins doubledouble kama mchanga wa bahari

nakutakiaa siku njema na yenye furaha tele hebu furahia zawadi hii nimeituma kwenu na ndege ya furahia airwing
basi pokea hiyo hapo

kimoja ni chenu na kingine ni cha hao matwins doubledouble
hongereni sana msalimie shem basi mwambie twampenda mimi furahia na Ency
siku njema
 

Hongera my dear,Mungu aliekutoa tangu day one to date,azidi kukubariki akufikishe mwisho mwema wewe na mpenzi/rafiki yako!!Mbarikiwe sana sana!!
 
Asante sana na tunamshukuru Mungu kwa hilo
 
Last edited by a moderator:
Amina..............kwakweli anastahili sifa kwa kukutumia wewe dada yangu kutuonesha kuwa bado inawezekana kuwa katika ndoa aliyobariki Mungu, japo wengi wanaidhalilisha taasisi ya ndoa Takatifu...........umenipa moyo kweli. Uzidi kubarikiwa
Amina mdogo wangu. Ndoa ni taasisi ambayo ina challenges nyingi sana, yaani Mungu pekee ndio anaweza kuisimamia. Kila kitu kinawezekana kwa uwepo wa Mungu
 
Toleo la pili:
Masikio akaziba,mkafunga ndoa,
Akauanza ubaba,kwa mwendo wa kudonoa,
Kila kona amekaba, kwa upole anaamua,
Unastahili hongera.

Mwenzio anaitwaje, nitajie nimjue,
Alikupataje, wenzio tufafanulie,
Mlikutanaje, na sisi tuwavizie,
Unastahili hongera.

Mungu ndiye muweza, nadhani mwamuamini,
Yeye atawaongoza,njia njema maishani,
Kwa ubora mtachomoza, sasa hata mbeleni,
Unastahili hongera.

Wazazi na ndugu,marafiki na majirani,
Jitahidi panda mbegu, za ushirikiano makini,
Heshimu 'lihengu',mkono uende kinywani,
Unastahili hongera.

Usengwi sana...zikomu!
 
ha haaaaaaaaaa, amina na asante sana rafiki.
hao watoto double double tutakuita uje kutusaidia kuwalea. Tunamshukuru Mungu ametujalia wa3 mpaka sasa
 
asante sana Chelian.
Tunamshukuru Mungu ametujalia watoto 3, binti na wakaka 2

Wou!
Hongereni sana,
watoto ndo mbaraka mkubwa ndani ya nyumba
i like sana kuckia wanandoa wanaoongelea mazuri ya ndoa
na sio kila siku malalamiko kuhusu ndoa na mahusiano!

keep rocking the boat geantly down the stream!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…