Website ya NACTE haifunguki

Jun 13, 2016
1
0
Jamani hii website ya NACTE haifunguki kwa mimi tu au na kwa wengine?

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI,

DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaoratibiwa na NACTE.

Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilishwa mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki nne (4) kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.

Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopanga kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.

Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa hazijajazwa na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.

Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza wiki ya mwishoni mwa mwezi wa Sita, 2016.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 9 Juni, 2016
 
Ni kweli wamefunga lakini mbona mwanzoni profile binafsi zilikuwa zinafunguka lakini toka Jana hata profile binafsi haifunguki kuna nini
 
walisea watafungua na kuendelea na application tena kwa sasa wanachambua walioleta au waliotuma maombi yao kwanza...
 
wako wanatumbua majipu.so kwa wale wacha mungu huu ni mda wa kusali sana na kwa wale wanao amini vingine huu ndo mda wenyewe wa kupeleka kuku.
 
mkuu we noumer sana umpelekee kuku mtu kisa kuchaguliwa ,system hairogwi kwa kuku wala mbuzi labda maombi yanaweza saidia
 
Nimepita pita kuangalia status ya Application kwenye website ya www.nacte.go.tz hicho ninachokiona ni kama wajanja washaitumbua
 
Attachments

  • Nacte.png
    Nacte.png
    147.9 KB · Views: 79

Back
Top Bottom