Leo nilishawishika kufungua website ya Arusha City Council kwaajili ya kupata taarifa za msingi hasa kuhusu kata na idadi ya watu na ikiwezekana majina ya viongozi wa sasa; kilichonishangaza ni aina ya taarifa nilizokutana nazo kama ifuatavyo;
Nadiriki kusema hii webiste ni kichefuchefu.
- Kuna taarifa ambazo ni irrelevant
- Data ambazo zipo ni za zamani kwa mfano bado wametumia taarifa za sensa ya 2002
- Pia kwenye eneo ambalo wanaelezea kuhusu halmashauri ya meru imeandikwa kutoka makao makuu ya halmashauri ya meru hadi uwanja wa ndege wa kilimanjaro ni umbali wa km 15 ambayo ni uongo
- Hii website pia haieleweki kama ni ya mkoa au ni ya jiji la arusha kutokana na jinsi taarifa zilivyokaa
- Maelezo yametolewa kwa lugha ya kingereza kibovu kwa mfano kuna neno linalosomeka e-pats ambalo ni kama ilimaanishwa kuwa experts.
Nadiriki kusema hii webiste ni kichefuchefu.