Web ya JamiiForums imelipuliwa kwa mafataki. Inawaka miale ya moto wa kila rangi

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Katika maisha haya, najivunia vitu vitatu muhimu

3. Najivunia kuwa mtu wa watu i.e mchapakazi, mcheshi, bidii katika kazi bila kujali hasara, moyo usio na chuki, usio na hasira, usio na wivu wa kijinga n.k

2. Najivunia kuwa mwanachama wa mitandao ya kijamii ya JamiiForums na X

1. Najivunia kufunguliwa dunia na kuwa ninachotaka. Clouds Media iishi daima. Kila nikiusikiliza ule wimbo wa

🎶Nioneshe ishara,
Nitakufuatilia,
Nikabidhi jukumu,
Nitalisimamia,
Niagize chochote,
Nami nitakuwasilishia,
Nitume kokote,
Na safari nitashughulikia aaha,🎶

I feel blessed

Kama ilivyokuwa kipindi cha sikukuu ya X mass, na leo muonekano wa web ya JF ni wa kipekee sana na wenye kuvutia.

a) Display ya JF Web imepambwa kwa milipuko ya fataki za kila rangi

b) Vichwa vya majukwaa vimepambwa kwa milipuko

c) Avatar zetu zimewekewa madoido

Yaani inaburudisha hata kuitizama, nilitaka kuleta kisa cha kuumizwa na mwanamke, lakini baada ya kukutana na uzuri huu wa kuvutia, nimejikuta nasahau shida zote. Ndugu zanguni tuendelee kupiga vitu mpaka pale tarehe za simu zetu zitakapoandika 1st Jan 2024

Niwatakie maandalizi mema ya Mwaka Mpya. Mola awaongoze, uwe ni mwaka wetu wenye mafanikio

Sisi sote tu watoto wa Baba mmoja. Watoto wa Maxence Melo

🎶Nia ya kukutumikia,
Nathibitisha kwa juhudi na nia,
Kama ilivyo jana najaribu tena leo,
Nitakutumikia,
Nia ya kukutumikia,
Nathibisha kwa juhudi na nia,
Kama ilivyo leo nikaribishe tena kesho,
Nitakutumikia

Nakuona juu,
Ya mawingu,
Ukivinjari kwa bashasha,
Naiona dunia yangu, ikiwa imefunguliwa🎶

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Back
Top Bottom