We yangekukuta ya padre huyu ungefanyaje?

Hmaster

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
346
86
[FONT=tahoma, new york, times, serif]Padri amekaa katika chumba cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili wa meza na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

Akisema "Padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

Padri "endelea"

"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi , ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua.

Je ! Yesu atanisamehe?"

Padri "utasamehewa"

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye.

Je ! Yesu atanisamehe na hiyo?"

Padri "utasamehewa"

"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua.

Je ! Yesu atanisamehe?"

Padri "utasamehewa"

"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kanisani kuungama dhambi mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena ! Akasema amefika nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua? akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto.

Je ! Yesu atanisamehe na hilo?"

Padri - kimya.......................................

"Padriiii, Je Yesu atanisamehe kwa hilo?"

- kimya..................................

Jamaa kutazama kwenye box la maungamo padri hayupo.

Lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri kama linatikisika! Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka sana.

"Sasa baba Paroko mbona umenikimbia?"

Padri kwa taabu akajibu ;

"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu








[/FONT]
 
Kwa nini vita na uhalifu
vimezagaa kila mahali bila
sababu za msingi ?
BIBLIA INAJIBU HIVI:
"Kisha aliwaambia, Taifa
...litaondoka kupigana na taifa,
na
ufalme kupigana na ufalme".
Luka 21:10.
 
Padri sasa nae ana wasiwasi gani!!!! .....Si mbinguni ni kuzuri kuliko hapa duniani??? mbona naye anapaogopa
 
Aliogopa jamaa akiangalia huku na huku akigundua wako peke yao wawili tuu kifo kilikuwa nje nje....maana huyu jamaa atakaekutana nae peke yake wakabaki wawili tuu...halali yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom