we will make it through....!

we will make it through....!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
jumatatu hii inaweza kuonekana ni ya kawaida kama jumatatu nyingine zozote zilizopita, lakini hii yaweza kuwa tofauti sana hasa kwa wafanyakazi watu wa kutegemea mshahara mwisho wa mwezi
ni jumatatu ya tofauti kwakuwa watu ni kama ndio wameuanza mwezi wakiwa watupu kabisa vibindoni mwao, kamshahara kote kameishia kulipa madeni ya january, wanatafakari wataisongesha vp hii wiki na huu mwezi
ni jumatatu ya kipekee kwakuwa kuna watu hawakulala, wanadaiwa kila kona na mpaka ijumaa wiki iliyopita mshahara ulikuwa bado, wakaambiwa pengine leo jumatatu hii utatoka
ni jumatatu ya kipekee kwa wale wenye marejesho ya bank, asikudanganye mtu usiku wa rejesho ni mfupi mno hasa kama rejesho halijatimia
ni blue monday kwa wanafunzi na wafanyakazi wote wavivu, asikudanganye mtu siku hii inachukiwa mno
lakini vyovyote viwavyo ni lazima tupeane moyo kwakuwa pamoja na changamoto zote za kimaisha ni lazima maisha yasonge, Mungu hatatuacha kabisa atakuwa nasi kwa kila hali na kila changamoto
hivyo basi tuweke stress zetu kando na ku CHEER UP NA JF CAUSE WHATEVER THE CASE WE WILL MAKE IT THROUGH
 
Back
Top Bottom