We Must Boycott VODACOM

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Hii Kampuni inayolindwa na Wanasiasa Mafisadi, licha ya malalamiko mengi kwa uongozi wa VODACOM kutupilia mbali udhamini wa tovuti unaowafundisha watoto wetu ukahaba, yaanu U-turn Blog, uongozi wa Vodacom umeweka Pamba masikioni. Hii inaashiria kwamba, hawa watu wanajiona kama vile "they are not accountable" kwenye jamii yetu. Hii kampuni inalindwa na wanasiasa Mafisadi

Kusema kweli hii blog inavunja misingi ya maadili yetu. Watoto wadogo na wanawake wanadhalilishwa huku wakifundishwa ukahaba, yaani kuwa na mume mzungu ndio bora zaidi. Kama jamii tunaomba siku ya Jumanne Ijayo iwe ni sku maalum ya kutokutumia Mtandao wa Voda hadi waondoe udhamini wao dhidi yah ii tovuti. Tayari tumeshapeleka malalamiko FBI pamoja Homeland security. baadhi yetu tuliyoko kwenye vyombo vya usalama tunashindwa kuelewa ni nini kinachoendelea na hii kampuni.

TUNAOMBA EMAIL YA MD WA VODACOM ILI TUMALIZE TATIZO LA U-TURN
 
ingekuwa bora ungeweka na mifano ya huo udhalilishaji hapa jukwaani.... Sio mpaka tuende tena kutafuta kuna nini kwenye hiyo blog?
 
U turn ni ya mange kimambi, while vodacom bosi wa mambo ya mahusiano sijui matangazo ni mwamvita makamba ambaye ni shosti wa mmiliki wa blog wanakula wote bia wekend,,, hapo hata tugome mwaka mzima mashost lazima walindane kupeana madili
 
Haina mashiko kulalamikia vodacom wanatangazia wapi. Wao wanatafuta wateja. Hata wauzaji miili wa corner bar wanatumia voda kuwasiliana na watej, hawawezi kuwakataza! Kama una vita na Mange ama umeachwa kwa tuition anazotoa kamalizane nae kule kule.
 
I understand si wote wa jf ni GT. Mtu katoa maoni yake watu wanaponda tu na kuita ujinga grow up members
 
hivi ukileta mada inayotokana na ujinga bado unategemea u-GT

unajua yale matusi yanayoporomoshwa dhidi ya wanawake wawili ndiyo yanayoleta yote haya?
 
Join Date : 21st September 2012

Posts : 5

Rep Power : 303

Likes Received:1
Likes Given:0
Hapo ndipo uliponiacha hoi umeingia juzi leo hii unataka kuingiza mkenge Wazee ACHA MARA MOJA.
 
Sikiliza mkuu sometimes kabla hujaja post vitu jaribu basi kutumia akili vodacom wale wanafanya biashara hawana makosa so long as mange havunji sheria ya nchi wao vodacom wanaangalia blog ina traffic ukubwa gani kama watu wengi wanatembelea hiyo ndio marketing opportunity yao wanadhamini tu...
Tatizo sio vodacom tatizo ni hao watu wanaotembelea mtandao huo... Kwani kama watu wakiacha kutembelea lazima traffic itashuka na definetely voda wataacha kudhamini so kwa ushauri ungeanza kuelimisha watu waache kutembelea ile blog something am pretty sure huwezi ...
Mange kama mange simpendi but sina tatizo nae kwani kwa chochote anachokifanya anafanya kwa ajili ya maisha yake na anaongelea zaidi kuhusu maisha yake so hana kosa wake zenu ma girl friend zenu na mama zenu ndio muwaambie waache kutembelea huo mtandao...
Watanzania still tuna matatizo kwenye masuala ya advertising, marketing na tunahitaji elimu na utaalamu kwenye hivi vitu kwa staili hii tutakuwa tunalalamika kila kitu kwakweli na kingine tujifunze kuishi kwa kukocentrate na maisha yetu tuache kusema sema watu ambao tumeona wanaingiza mshiko kama unavyotaka kumfanyia mange
 
ladies ladies ladies na drama za ajabu ajabu......

Kwa nini tuisusie vodacom?

Huo ugomvi wenu wa facebook na uturn mmalizie facebook na uturn..... Vodacom hata jamiiforums huwa wanaidhamini kwa hiyo tuisusie pia?

Hao wanawake watu wazima wanaojidhalilisha wenyewe mlipaswa kutoingia uturn wala facebook pages za hao wadada....na kuwafunza watoto kuchagua kilicho chema, tena unaposema watoto unamaanisha watoto wa wapi? Maana huku madale uswazi kwangu watoto hawajui fesibuku wala uturn?

Kama kuharibu watoto kuna anayeharibu watoto kama magazeti ya kiu, ijumaa, risasi na mengine ya udaku? Mbona wazazi hamlalami?
 
point ya msingi hii, pokea like....

Laiti kama kila mtu angekuwa busy kujishughulisha na mambo yake huo muda wa kutukanana wangeutoa wapi?
 
Sikiliza mkuu sometimes kabla hujaja post vitu jaribu basi kutumia akili vodacom wale wanafanya biashara hawana makosa so long as mange havunji sheria ya nchi wao vodacom wanaangalia blog ina traffic ukubwa gani kama watu wengi wanatembelea hiyo ndio marketing opportunity yao wanadhamini tu...
Tatizo sio vodacom tatizo ni hao watu wanaotembelea mtandao huo... Kwani kama watu wakiacha kutembelea lazima traffic itashuka na definetely voda wataacha kudhamini so kwa ushauri ungeanza kuelimisha watu waache kutembelea ile blog something am pretty sure huwezi ...
Mange kama mange simpendi but sina tatizo nae kwani kwa chochote anachokifanya anafanya kwa ajili ya maisha yake na anaongelea zaidi kuhusu maisha yake so hana kosa wake zenu ma girl friend zenu na mama zenu ndio muwaambie waache kutembelea huo mtandao...
Watanzania still tuna matatizo kwenye masuala ya advertising, marketing na tunahitaji elimu na utaalamu kwenye hivi vitu kwa staili hii tutakuwa tunalalamika kila kitu kwakweli na kingine tujifunze kuishi kwa kukocentrate na maisha yetu tuache kusema sema watu ambao tumeona wanaingiza mshiko kama unavyotaka kumfanyia mange

Kwa logic yako hii makampuni ya tumbaku yasingewekewa sheria inayowataka kutoa tahadhari juu ya athari za matumizi ya tumbaku. Kusingekuwa na sheria pia inayokataza kutangaza junk food. Not everything that is accepted by law is moral!
 
ladies ladies ladies na drama za ajabu ajabu......

Kwa nini tuisusie vodacom?

Huo ugomvi wenu wa facebook na uturn mmalizie facebook na uturn..... Vodacom hata jamiiforums huwa wanaidhamini kwa hiyo tuisusie pia?

Hao wanawake watu wazima wanaojidhalilisha wenyewe mlipaswa kutoingia uturn wala facebook pages za hao wadada....na kuwafunza watoto kuchagua kilicho chema, tena unaposema watoto unamaanisha watoto wa wapi? Maana huku madale uswazi kwangu watoto hawajui fesibuku wala uturn?

Kama kuharibu watoto kuna anayeharibu watoto kama magazeti ya kiu, ijumaa, risasi na mengine ya udaku? Mbona wazazi hamlalami?

So, as long watoto wa uswazi (kama unavyowaita mwenyewe) hawaingii huko basi watoto wa mahali pengine "shauri zao" sio?
 
Nimesoma comment za Members wote mliotangalia na ninaheshimu mawazo ya kila aliyechangia, ila mimi kwa Mtazamo wangu nadhani Watanzania hasa wanawake wanapaswa kubadili mindset zao, kwa utafiti mdogo usiyo rasmi niliyoufanya nimejiridhisha kabisa Watanzania ndio Jamii pekee hapa Duniani ambayo haitofaidika na uwepo wa Internet.

Mimi binafsi nimeboycott mwenyewe kimya kimya kuingia kwenye blog ya Michuzi kwa miaka kadhaa sasa, na Mjengwa blog pekee ndiyo ilikuwa blog ambayo mimi naitembelea kwenye hizi local blog ingawa Mjengwa naye nimesiktisha kutembelea blog yake baada ya kujifungamanisha na wauwaji.

Kwakweli Frankly speaking mtu kama Mange mimi jina lake nimelijulia hapa JF kwa sababu huwa sina muda na blog ambazo hazina tija kwangu na isitoshe habari za kipashkuna kwangu huwa hazina nafasi, JF imesheheni kila kitu na ina majukwaa yote kwahiyo sioni kama napungukiwa na kitu.

Ombi langu kwa Watanzania wenzangu hasa kina Dada tutumie Internet kujifunza zaidi maana Internet ni zaidi ya Youtube, Facebook na hivyo viblog vyenu uchwara. kuna Link nyingi sana ambazo ni useful za kuzitembelea ili kupanuwa bongo zetu.

Mwisho kuboycott Vodacom kwa sababu ya U turn huo ni utoto kwa sababu dhambi kubwa ya Vodacom kwangu ni kuwahujumu Watanzania kwa kushiriki hujuma za uchaguzi mkuu kwa mtandao kutumika makusudi kueneza sms za chuki za kidini. mwenye nia njema na nchi yake alipaswa alione hili siku hizo na siyo kwenye blog ya mapushukuna.
 
Back
Top Bottom