We Mungu wa kweli tuepushe na balaa hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

We Mungu wa kweli tuepushe na balaa hili

Discussion in 'International Forum' started by Pengo, Aug 29, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hali ya joto kali inawatesa watu nchini Sudan kiasi cha kwamba watu wanalazimika kuingia ndani ya mafriji makubwa ya viwandani ili kujipoozesha, watu watatu wamefariki dunia jana baada ya kushindwa kutoka ndani ya friji waliloingia.Joto kali nchini Sudan limepelekea kuibuka kwa biashara ambayo huenda ipo nchini Sudan pekee.

  Kutokana na joto kali nchini humo, kumeibuka biashara ya kujipumzisha kwenye mafriji makubwa ya viwandani.

  Watu wanalipa paundi tano za Sudan( Takribani Tsh. 2500) kwa kila lisaa limoja wanalotumia ndani ya mafriji ili kuipoozesha miili yao.

  Taarifa toka mji wa Port Sudan zinasema kuwa wanaume watatu walikutwa wamefariki ndani ya friji kubwa kama yale yanayotumika viwandani.

  Taarifa zinasema kuwa wanaume hao baada ya kulipa paundi tano za Sudan waliingia ndani ya friji kuipoozesha miili yao baada ya kupigwa na joto kali.

  Taarifa zaidi zinasema kuwa wanaume hao walifariki baada ya mlango wa friji walilokuwemo kujifunga na wao kushindwa kuufungua mlango huo kwa ndani.

  Katika mwezi huu wa nane ambao kawaida huwa ni mwezi wenye joto kali kuliko miezi yote nchini Sudan, watu 13 walikumbwa na shambulio la moyo wakiwa ndani ya mafriji kama hayo.
  Chanzo.AP
   
 2. 2my

  2my JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mmmh hili nalo neno!!!!
  kukaa kwenye fridge kwa one hr ataacha kuganda lol pole zao!
   
Loading...