Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Na. M. M. Mwanakijiji
Ni kana kwamba Oktoba 29 haikutokea. Wanaendelea kutenda kana kwamba yaliyotokea siku ile ya giza ni mambo tu ya kufikirika. Wanaendelea kutenda kana kwamba tunawaonea, tunawasingizia na kuwa yote yanayosemwa ni uzushi tu uliopitiliza. Wanajitahidi kupuuzia, kutokujali na kutenda kana kwamba damu waliyoimwaga si ya Watanzania.
Tunaambiwa katika kutetea kiti chake Rais aliidhinisha ubakaji, ulawiti wa watoto wetu na zaidi mauaji. Mwenyewe kasema "nguvu iliyotumika" inaendana na tishio lililokuwepo. Ati wangetumia nguvu kidogo wangeondolewa kwa mapinduzi (msisahau chama kinaitwa ni 'cha mapinduzi'). Kama walivyofanya kabla ya Oktoba 29 walitoa vitisho na mikwara ya nguvu na kweli kabisa wakaenda kutekeleza walichokipanga kiwe funzo kwa yeyote atakayewapinga.
Miili tuliyoiona imezagaa, picha za video na za kuganda tulizoziona za watu waliouawa kinyama na kuachwa hadharani kama vibudu vyote hivyo ni makosa ya Mange, Maria Sarungi, na wanaharakati. Kwamba, watu walioko Tanzania wanatakiwa kupiga makofi kila wakubwa hawa wanapopita, walioko Tanzania hawatakiwi kusema siyo kwa jina letu. Walioko Tanzania tunaambiwa ni lazima wakubaliwa kutawaliwa bila kujali wanavyotawaliwa. Mauaji ya Oktoba 29 ilikuwa ni "fanya fyoko ukione"; watawala wetu hawa walioshindwa wanarudia tena - 'fanyeni fyoko muone kama hatutawachinjilia mbali".
Wanatukumbusha vikundi visivyo vya serikali kama kule Sudan na sehemu nyingine ambavyo vilishiriki mauaji ya wananchi wao kwa jina la kuitetea serikali. Tunawasikia wengine wanajitokeza na kupiga mikwara kuwa wako tayari kuitetea serikali; hawa wanaweza kupewa silaha, za moto na za jadi kuingia mitaani kuua. Kama ilivyotokea Oktoba 29 hawa wauaji wa serikali hawahitaji kujitambulisha; vitambulisho vyao ni bunduki, alama zao ni bastola!
Ni kweli wataua tena; wameonja damu na wameongezeka hamu! Wanajua sasa hivi hawawezi kutawala tena kwa hoja; isipokuwa hoja za risasi na visasi! Zamani waliposhindwa hoja walikuwa wanaleta vihoja; sasa wameshindwa hoja kwa kasi sasa wanaleta risasi na visasi. Tunawathubutisha tena! Ueni tena wananchi wetu; jitangazeni mipango yenu, semeni kuwa mnaenda kuua tena kama mlivyofanya hadi Watanzania wote wasalimu amri!
Hawa wamenza kufanana na utawala ule dhalimu tuliowahi kuuona katika bara letu la Afrika; wamefanana kila kitu isipokuwa rangi tu. Watawala hawa wanataka kutawala kwa kuua; na niwe wa kwanza kutabiri baada ya mauaji yaliyopita na haya yajayo; Samia hatoweza kutoka madarakani; na hatoachwa atoke madarakani na watu wanaomtegemea kuwalinda. Sasa hivi naamini kuna uwezekano wa asilimia 99 watakapopendekeza Katiba Mpya wataondoa ukomo wa madaraka (term limits) ili Samia aendelee baada ya 2030. Atoke achekwe?
Lakini vyovyote vile ilivyo, kuelekea Disemba 9 wao ndio wanauamuzi wa kufanya; watoke waue tena mamia wengine au watafute hekima ya jinsi gani kudifuse the situation. Lakini kwa vile wameshajawa na roho ya ubabe na kuwa wanataka kulinda "dola" aka familia na maslahi yao uwezekano wa wao kurudi nyuma ni sifuri. Kweli hawa wanaweza kuua tena; lakini wajue kuwa wao wameshajifunza kuua na Watanzania wamejifunza kufa kwa ajili ya nchi yao.
Ila waue tena; ili waharakishe mwisho wao. Imebidi nifunge safari ya ghafla kuja kufuatilia ya mambo ya Disemba 9; tunakusanya ushahidi vizuri zaidi sasa kuliko ile Oktoba 29. We double dare them.. do it again. Please.