WB yaipa Ilala Sh41 bilioni kuboresha miundombinu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
world%20bank.jpg
Pamela Chilongola
BENKI ya Dunia (WB) imetoa mkopo wa Sh41 bilioni kwa ujenzi wa miundombinu Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

Fedha hizo ni sehemu ya Sh150 bilioni ambazo ziliombwa na halmashauri nne za Dar es Salaam kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani, Meya wa Ilala, Jerry Silaa alisema Serikali iliomba mkopo WB kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya Da es Salaam.

Slaa alisema miundombinu hiyo ni barabara, mifereji ya maji, uzoaji taka, urasimishaji makazi, uboreshaji mapato ya halmashauri, ujenzi wa miundombinu kwenye makazi yasiyopangwa na utawala bora.

“Uboreshaji miundombinu ya barabara na mifereji ya maji ya mvua, zimetengewa Sh21 bilioni, ukusanyaji na usafirishaji taka ngumu umetengewa Sh5.3 bilioni, uboreshaji miundombinu kwenye makazi yasiyopangwa Sh 8.4 bilioni,” alisema Slaa na kuongeza:

“Urasimishaji na kutenga maeneo ya huduma kwenye makazi yasiyo rasmi imetengwa Sh1.6 bilioni.”
Pia, alisema mradi huo ni wa awamu ya kwanza ambayo itahusisha kata za Kiwalani, Gongolamboto na Ukonga na kwamba, wakimaliza wataingia awamu ya pili.

“Uboreshaji huo utakuwa Kata ya Kiwalani mitaa ya Minazi mirefu, Yombo, Kiwalani na Kigilagila; Kata ya Gongolamboto itahusu mitaa ya Gongolamboto, Ulongoni, Guluka Kwalala na Mongolandege na Kata ya Ukonga mitaa ya Makazi, Mazizini na Mwembe madafu,” alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Kivule, Nyasika Getema alisema kwenye kata yake ametengewa Sh6.29 milioni kwa ujenzi wa barabara ya Mombasa-Moshi bar. WB yaipa Ilala Sh41 bilioni kuboresha miundombinu
 
PCCB waweke ofisi pale Arnatoglo hall kwani mkopo huu ni kiashiria cha rushwa ijayo pale Ilala. Ogopa viongozi waliokwenye mchakato wa kura Kama kijana Jerry. Wanahitaji pesa ndefu kutimiza azma zao.
 
Back
Top Bottom