Wazungu walitufundishaje (Waafrika) Kiingereza?

Wazungu walitufundishaje (Waafrika) Kiingereza?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Binafsi huwa nastaajabu sana ninapoona Mwafrika akiongea lugha za Kizungu, iwe Kireno, Kifaransa au Kiingereza!

Swali ambalo hunijia kichwani waliwezaje kutufundisha Kiingereza? Walitumia mbinu gani?

Ukitaka kupata ukaribu labda wa ninachomaanisha, fikiria leo hii uende kwa Wahandzabe halafu uanze kuwafundisha Kifaransa, unaanzaje?

Izingatiwe kwamba ni rahisi kwa Mnyakyusa kujua Kiswahili kwani ni Mbantu hivyo ni lugha ya Familia moja au ni rahisi Mtanzania kujifunza Kizulu, lkn Kiingereza au Kifaransa ni Dunia nyingine kabisa, sasa walitumia mbinu gani mpaka leo tunaongea Kiingereza?
 
hata karabu

Ya Kiarabu pia nimesahau tu kukiweka, lkn hatuongei Kiarabu na Waafrika wanaongea Kiarabu kama Wasomali lugha yao ni jamii moja na Kiarabu hivyo haishangazi, lkn Mgogo na Kiingereza? Walitumia mbinu gani?
 
Lugha yoyote inayotumia mfumo wa alphabets (A to Z) inafundishika na kueleweka vizuri kwa wale wote ambao mother tongue zao pia zimejengwa kwa matamshi na maandishi ya alphabets hizo.
 
History inawataja watu wanaitwa WAKALIMANI, hata sijui walipatikanaje!

Japo nafahamu wazungu walijifunza Lugha za makoloni yao kwanza, kisha ndio wao wakawafundisha waafrika Lugha za kigeni!
 
Lugha yoyote inayotumia mfumo wa alphabets (A to Z) inafundishika na kueleweka vizuri kwa wale wote ambao mother tongue zao pia zimejengwa kwa matamshi na maandishi ya alphabets hizo.

Lkn hizo alfabeti siyo za asili yetu Wazungu waliziweka tu, hata Kichina au Kijapani unaweza kutumia hizi alfabeti, wanaita latinization, lkn haina uhusiano na Lugha, lugha yoyote ile Duniani unaweza kutumia hizo alfabeti!
 
History inawataja watu wanaitwa WAKALIMANI, hata sijui walipatikanaje!

Japo nafahamu wazungu walijifunza Lugha za makoloni yao kwanza, kisha ndio wao wakawafundisha waafrika Lugha za kigeni!

Hapo umetoa mwanga mzuri, vinginevyo nikijaribu kufikiria hapo mwanzo sipati picha!
 
Ukoloni mambo leo ndio iliyotufundiha lugha za mabara ya mbali na kutufanya ili tuonekane bora lazima tujue lugha hizo na kusahau tamaduni zetu na huu ndio umaskini wetu mpaka kesho
 
How did they teach us? I dont know to speaking and writing in swahili language but what I can say is Hii lugha ilikuja kwa meli kama baadhi ya waswahili wanavyosema ila sina ushahidi wa kutosha kuthibitisha hili maana me mwenyewe ni mswahili tu kama wewe hivyo naishia hapo tu.
 
Hawakuanza kufundisha kama unavyodhani labda walikuwa wanahitaji wanafunzi watakao faulu, no! kwa kuwa wao kwa mara ya kwanza walikuja kwa njaa ya malighafi kwa hiyo yale maingiliano yao na nyie waafrika ilijilazimu kimaumbile lazima lugha mtaifahamu tu hata kimakosa. Kwa mfano ikija gari ya polisi kisha mkasikia "fire" ukaona mtu kadondoka ukasikia tena "fire" ukaona mtu kadondoka tena, mara "fire" kafa mtu, sasa siku nyengine ukisikia fire sidhani kama utashindwa kulihifadhi hilo neno na kulitafsiri. Ndivyo hivyo lugha kimaumbile anavyoifahamu mtu hata kimakosa.
 
Hilo linawezekana kama lugha yako na hiyo mpya ni ya Familia moja, yaani kama zote ni kibantu lkn kama lugha tofauti kama Kiswahili na Kiingereza bila mbinu mbadala hatuwezi kujifunza tu kwa matukio, ndo maana unaona TZ ni Wamasai tu ndo wana shida na Kiswahili kwa sababu siyo Wabantu, ili Mmasai ajue Kiswahili kuna ziada unahitajika!

Ni lzm kuwe na kinachowaunganisha ninyi wawili mwanzoni kabisa!
 
Sasa wewe unadhani ni kitu gani kilichofanyika mpaka ikawa hivi? au ni Mungu tu maajabu yake.
 
Sasa wewe unadhani ni kitu gani kilichofanyika mpaka ikawa hivi? au ni Mungu tu maajabu yake.

Hata mimi sielewi, najua walichofanya Australia kwa mfano, Wazungu walikuwa wanawachukuwa watoto wa Kiaborigine wakizaliwa tu kwa nguvu unaweza kusema kuwapora ktk kwa Wazazi wao na kuwapeleka kulelewaa kwenye Familia za Kizungu, hivyo wale watoto walilelewa na Wazungu na lugha yao ya kwanza ikawa ni ile lugha inayoongewa pale nyumbani yaani Kiingereza!

Lkn huku kwetu sijui walitumia mbinu gani!
 
hapa ni sawa na kujiuliza kwa nini waswahili wengi hawajui matumizi ya ha
mf apana=hapana
ana = hana
ujambo= hujambo
nk
 
motto huwa anajuaje kuzungumza na huwa anafundishwaje wakati huwa hajui kitu chochote.jibu lake ni jibu kwenye swali lako
 
Back
Top Bottom