Wazoefu wa incubator mashine njooni mnipe ushauri

SIPIYU30

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
1,698
2,274
Nimenunua incubator machine yenye uwezo wa mayai 700.
Nimeweka mayai, ila kati ya 700 nimepata vifaranga 300 tuu.
Binafsi sijafurahi kwa sababu matarajio yangu yalikuwa at least 500.
Kuna mayai mpaka yalionyesha kupasuka ikaishia kifaranga kutoa mdomo tu
na zoezi likaishia hapo.

Naomba mnishauri nifanyeje ili next round nisipate hasara?
Mayai ninayanunua kwa mfugaji wa kuku mtaa wa pili.
Niliyapima yalipofika siku ya 8 nikaondoa mabovu,
Lakini hata hayo yaliyobaki bado mengi hayakutotolewa.

Naombeni ushauri
 
Mkuu hiyo ni changamoto!mayai unayoweka hakikisha hayajazidi siku 7 baada ya kuku kutaga,hiyo kupasuka kifaranga kinashindwa kutoka ni kuwa baada ya mayai kukaa baada ya 7 days yanaanza kama kujitengeneza kifaranga!na yanapungua
 
Kifaranga kikiwa tayari na yai likiwa lipo vizuri lazima kifaranga kitoke ila kama halijajaa vixuri kinashindwa kutoka kwani kikipumua kasha halipasuki kwani kinakuwa hakijajaa sawasawa
 
Ok,
Lakini kuna mengine kwa mfano mayai ambayo yametagwa na kuku wangu mwenywe, na nimehakikisha yametagwa siku mbili au tatu, yet kuna mengine yametotoleshwa na mengine hayajatotoleshwa
 
Ok, nashukuru kwa ushauri, kwa kuwa ni mara ya kwanza nitaendelea na nitawapa updates
 
Pia usiweke kwenye joto!hakikisha unatumia tray za plastic na usiwekee tray zipandane kwan yanatengeneza joto
 
Kuna changamoto nyingi hasa ukizingatia mahala incubator ilipowekwa. Eg kama ipo eneo lenye uwazi mkubwa na hewa kavu usitegemee utapata matokeo sawa na mtu aliyeiweka eneo la kawaida na lenye hewa ya kawaida. Ili mayai yaanguliwe kuna vitu vya msingi baada yq yai kuwa limerutubishwa navyo ni joto(temperature) na hali ya unyevu kwenye hewa(humidity) kushindwa kubalance vitu hivyo kwenye incubator ni moja ya sababu za mayai kutokuanguliwa yote.
 
Back
Top Bottom