Wazoefu wa gari hii naombeni ushauri wenu

Wazoefu wa gari hii naombeni ushauri wenu

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
Jamani mimi sio mtaalamu sana wa magari, nina uzoefu kidogo tu hasa katika kuendesha ila ubora sijui ila najua majadiliano ya hapa yatasaidia kunipa picha ya kuanzia.

Kuna gari nataka kununua na details zake ziko hivi:

Make: Nissan model: datsun model

no: GA-QD21

Body type: pickup

Year of manufacture 1996

Petrol, cc 2000.

Reg no yake ni CYP

Hebu nambieni wataalam mliowahi tumia hii gari ipoje kwenye spare, uimara na je inahimili ubebaji wa mizigo manake nataka kuitumia kwa biashara za mizigo.

Tafadhali nijuzeni kabla sijainunua
 
Ngoja wataalam waje. Sema mi najua gari hizo zilikuwa imara sana. Wasiwasi wangu mbona make yake ya zamani sana vipuri utapata kweli?
 
Kaka kwa uimara hiyo gari ni imara sana, ila tatizo ni kwenye spares, kupata spare mpya na genuine ni aghali kidogo, ila kwenye used zipo tatizo tu ni kuwa na uhakika na hiyo spare. Ila uimara wake pia utategemea sana na matumizi yako, ukiibebesha mawe na tofali haitafikisha mwaka, ila ikiwa ni ya kubeba box za wastani na masafa ya karibu karibu basi hesabu miaka 20 kama utafatisha misingi bora ya matumizi ya gari na kuijali!
 
Ngoja wataalam waje. Sema mi najua gari hizo zilikuwa imara sana. Wasiwasi wangu mbona make yake ya zamani sana vipuri utapata kweli?

1996 kwa pick up sio zamani sana, zipo show rooms mpaka za 1988 ma bado zinanunuliwa na ni imara km chuma ya Mjerumani
 
safi sana kwa maelezo mazuri. Vp kuhusu nguvu na ulaji wa mafuta
 
mkuu hiyo gari inakula mafuta kwa kuwa haliwezi kula ugali
 
spare sio dili kwa sasa kwa kuwa ulimwengu ni kijiji na hamna mtu mwenye kiwanda cha spare hapa jamvini.
 
Hii haina tofauti na hilux twelve R
Mkuu huwezi kuifananisha Nissan pick up na Toyota hilux
. Ninayo D/Nissan pick up (D/Cabin) ya 1990 ya diesel niliiagiza direct toka Japan iko poa sana mpaka sasa. Of current I am having a Teana model hatch back. So marvelous. Nissan gari wach mchezo. Take my suggestion, buy it.
 
aisee Mshomba umenifungua macho sana ishu ya spare sio tatizo safi sana ntainunua manake kuna jamaa yangu kainunua sa ametetereka kiuchumi anataka nimrudishie hela kidogo aniachie chuma hii
 
Last edited by a moderator:
jamani naomba mnijuze tena utofauti wa hizi zenye kabuleta na hizi ambazo sinatumia magneto sina uhakika kama nimepatia ila ipi nzuri kati ya zenye cabuleta na sizizo na cabuleta
 
mkuu wala usisite mimi kuna jamaa ameniuzia gari kama hiyo kwa kweli hipo vizuri spea ni nyingi sana bei sio mbaya kiivyo
 
Back
Top Bottom