USHAURI: Ununuaji wa magari... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHAURI: Ununuaji wa magari...

Discussion in 'JF Garage (Magari na Vyombo vya Usafiri)' started by libaba PM, Oct 4, 2010.

 1. l

  libaba PM Senior Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nilikua naangalia mitandao mbali mbali ya magari ambayo wanaleta magari used hapa Tanzania, Bahati nikapata mtandao ambao umenivutia, una magari yanayoonekana ni mazuri kwa Picha, lakini kwa kuwa uelewa wangu juu ya biashara hii ya magari ni mdogo, naomba wenye ufahamu mnisaidie.

  Je Toyota Opa ni gari ambayo haisumbui spares..
  Je ina ugonjwa wowote wa kudumu ?
  wao wamesema Bei ni FOB US$ 2,200/=

  JE MPAKA IKIFIKA HAPA DAR KWA UZOEFU WENU KWA MAKADIRIO ITANIPASA NIWE NA KIASI CHA TSH NGAPI ? Baadhi ya taarifa ni hizi.

  Year / Month2001/12
  Odometer38,000 km
  Displacement1,800 cc
  Steering Right
  Transmission Automatic
  Fuel Gasoline/Petrol
  Model codeTA-ZCT10

   
 2. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Libaba OPAL siyo mchezo, inachagua vituo vya mafuta (wewe utakuwa na undugu wa karibu na BP tu). kuhusu spare sijajua sana ila nilishawahi kusikia watu wanasema eti vifaa vyake ni aghali.

  Subiri watu wengine wachangie pia. yangu ni hayo tu
   
 3. l

  libaba PM Senior Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  asante Danzi, nashukuru kwa hayo.
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  BP imekufa, hapa Tz haipo,zimebaki rangi za BP ndugu yangu. Sasa hivi mafuta ni chakachua kwa kwenda mbele. Teheeeee.
   
 5. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mi natumia OPA kwa miaka miwili na wiki 2 sasa, haijanisumbua hata kidogo, zaidi ya kupata pancha tu.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Beuty Pancha inasababishwa na matatizo ya gari au ni tyre zinakuwa sio nzuri?
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Tafuta Tshs ziwepo tayari tayari 9,004,875:A S 13:
   
 9. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,758
  Likes Received: 2,353
  Trophy Points: 280
  matumizi yke ni kwa barabara za lami tu na ambazo hazina mabamus makubwa kama ya segera
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  zinapendeza
   
 11. YoungCorporate

  YoungCorporate JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 30, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  kaka kutokana na ka-uzoefu kangu katika hethabu actual cost ziko more/less equal to 8.8m....  Usiteme big-g kwa karanga za kuonja......
   
 12. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  :a s 13:
   
 13. l

  libaba PM Senior Member

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  daaah asanteni kwahiyo Tsh 8.5m inatosha kununua hiyo gari.
   
 14. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiyo bei ni kubwa kidogo ukilinganisha na makampuni mengine kwenye tradecarview list. Gonga HAPA. Hapo makampuni yako mengi na mengine sina uzoefu nayo, ila kuna mtu ninayemfahamu amenunua gari kwa kampuni ya Carnival ambao wanauza Toyota OPA ya mwaka 2001 kwa USD 1813 (FOB), gonga HAPA na waweza kuomba wakakupunguzia kidogo.
   
 15. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #15
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Unachopaswa kuzingatia ni bei ya CIF (Cargo In Freight) ambayo huwa tofauti kulingana na mahali gari itakaposhushwa. FOB (Freight On Board) bi bei ya gari KABLA ya kutumwa, maana yake, on Board (tayari kwa kutumwa). Kumbuka FREIGHT na BOARD ni vitu viwili tofauti.

  Kwa hiyo unapaswa kupata bei ya CIF Dar es Salaam, kisha uende TRA (inategemea uki wapi), wao ndio watakupa makadirio mazuri zaidi.

  Gharama za ushuru hukokotolewa kutokana na Ujazo wa Injini (CC), mwaka ambao gari ilitengenezwa, na kama inatumia mafuta ya dizeli au petroli. Kama umri wa gari ni zaidi ya miaka kumi, kuna ada ya ziada ambayo utatozwa, nadhani ni asilimia 15. Kiwango hiki kimewekwa ili kuepusha magari machakavu kuingizwa nchini. Minimum unapaswa kuwa na gari ambayo imetengenezwa kuanzia mwaka 2000. Ifikapo mwaka 2011, basi, kiwango hiki kinasogea hadi mwaka 2001.

  Nakutakia mafanikio mema. Naipenda sana hii gari, kwa hiyo uniambie wapi ulipopewa bei nzuri kama hiyo, na mwisho wake, umelipia jumla ya gharama kiasi gani mpaka ikawa ON THE ROAD! Usiwasikilize watu wanaoongea bila kuwa na uhakika wa wanachokisema.

  -> Mwana wa Haki
   
 16. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Cha Msingi Ndugu ni kusoma reviews za wataalamu kupitia car reviews webistes ambapo utapata detailed information kuhusu gari husika na kutoka hata kwa wanaotumia gari ya aina hiyo. Ila elewa kuwa gari yeyotec ni matunzo yako tu japo OPA haifai sana kwa njia zetu za Bongo kwa kuwa ipon chini na bodi yake ni very right..

  Toyota Opa -Frist Impressions


  Kuhusu gharama halisi, kwa mitandao ya wauza magari unaweza kufanya mahesabu mwenyewe kupitia bei za FOB na unakujua CIF kwa bandari utakayosushia ni ngapi kisha ukaipeleka katika bei za madafu. Kwa mfano ukienda katika mtandao wa Tradecar view.
  http://www.tradecarview.com/used_car/japan%20car/toyota/opa/967478/ AU Japan Partner Toyota OPA Used Cars - Japan Partner - Japan Partner Wanakuonyesha bei halisi CIF na ipo nyingine unapewa kwa madafu ukitaka.

  Kuhusu Kodi na gharama za Utoaji gari bandarini hizo waweza kupata kwa madafu.

  Kodi tembelea mtandao wa TRA utapata details zote. Hpa link.

  http://www.tra.go.tz/documents/Motor%20Vehicle%20Tax%20Computation.doc

  Kutoa gari check na Mawakala wa Kutoa mizigo (clearing and forwading Agents).
   
 17. telele

  telele Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nakushauri usipitie kwenye website ya tradecarview, kuna gharama zitaongezeka, maana wao wanakukutanisha na makampuni yanayouza magari, wao siyo wauzaji, so kuna cost zinaongezeka kutokana na wao nao hutakiwa kulipwa na hiyo kampuni baada ya gari kuuzika. ingia moja kwa moja kwenye website za makampuni. jaribu hii www.beforward.jp then utaniambia kuhusu bei zao. magari ni mazuri na bei zipo chini ukilinganisha na makampuni mengine. nakushauri kama dealer wa magari. TOYOPA OPA zipo za kumwaga
   
 18. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu si kweli unayosema. Kwenye tradecarview magari yaliyopopale tayari makampuni yake yameonyeshwa na baei za magari yao pia na si kwamba magari yanauzwa na tradecarview, wao ni mkusanyiko tu wa makampuni mengi yanayouza magari. Uzuri wa kwenye tradecarview kuna wigo mkubwa wa kuchagua magari tofauti na hiyo beforward.jp maana nimeangalia ni wachovu kwelikweli hawana Harrier ya kuanzia mwaka 2001 hata moja, Suzuki escudo ya kuanzia mwaka 2001 hakuna hata moja na pia hawaonyeshi mileage ya magari yao kitu ambacho ni hatari maana unaweza kununua gari lililokongoroka hasa. Kuna watu kadha wa kadha niliokaribu nao wamenunua kupitia tradecarview magari mazuri kabisa kwa bei nzuri.
   
 19. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pancha ni tyres zenyewe, 4 that case nasema OPA ni nzuri sana, coz matatizo ya gari kama gari bado sijapata kwa muda wote huo, na ninazingatia sana ule msemo wa kitunze kidumu!
   
 20. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  aisee...kwanini?
   
Loading...