Mkuu Rebeca wewe unakimbia ukweli au una kumbukumbu fupi.
Ukweli ni kwamba Raisi Magufuli anaamini yeye ni Malaika na hakuna Mtanzania mwenye akili kama yeye.
Raisi wa nchi alishasema wazi kabisa anatamani malaika washuke waje wazime mitandao ya kijamii kwa mwaka moja.
Hivi unategemea mtu kama huyo ndiyo amuone mtu kama
Al-Watan kwenye jina lake halisi atamuacha kweli ???
Kama ni kufanya Head-Hunting si waende kwenye taasisi za kielimu kama UDSM au MZUMBE ?
Ukweli Mchungu pengine ambao hata wewe huufahamu au umeufumbia macho ni kwamba JF Elites (Watumiaji )wengi ni kundi ambalo kwa bahati mbaya Serikali ya Magufuli na CCM wamewa-labell as Heretics.
JF toka mwaka 2006 imefikishwa hapa ilipo kwa makundi makubwa mawili ambayo huwezi yaacha kuyataja:
1. Watanzania wanaishi nje ya nchi (Diaspora)
2. Wanasiasa na wanaharakati tofauti tofauti (Watanzania waliokosa Uzalendo according to Magufuli )
NB 1: Haya makundi kwa bahati mbaya ni watu ambao Serikali ya CCM inawachukulia kama Waasi na maadui.
Jiulize kwanini huyu
Maxence Melo alikamatwa na kulazimishwa atoe taarifa zetu ???
Kama Serikali ya Raisi Magufuli ingekuwa na nia njema kulikuwa na ulazima wa kuwakamata na kuwaanzishia kesi ???
NB 2: Ile Slogan ya Where We Dare to Talk Openly haikutolewa tu angani.
Fuatilia vizuri utajua kinaga ubaga yaliyokuwa yanafanyika hapa Jukwaani hadi kuibua Ufisadi kama RICHMOND.
Unataka kuhatarisha maisha ya watu kitu ambacho mimi binafsi naona ni kuchezea Sharubu za Simba.
Nakushauri uache kabisa: Raisi anasema ana mawaziri wapumbavu ambao kawachagua yeye mwenyewe bila shuruti.
Kama kaitenda miti mibichi hivyo, sisi miti mikavu ambao siyo hata wana-CCM atatuacha kweli ????