Wazo tu;msirudi tanzania mtajuta

Wazo tu;msirudi tanzania mtajuta

KWANZA HONGEREN KWA KUMALIZA SHULE VYEMA
PILI KAZI ZA HUKU NISHIDA JAMANI
877.JPG



TATU WAMEANZISHA KIPENGELE CHA MIAKA KWENYE KUOMBA KAZI AMBACHOA KIKUWEPO MKIONDOKA NA HILI NAHISI AMKULIJUA
NNE:AJIRA MTAKAYOPATA KWA UMERI WENU HATA MSHAHARA WATAWABANA SANA
TANO NASHAURI KAMA MNA CHANNEL NZURI ZAIDI HUKO WALA SIO KWA KUJA KUOMBA AJIRA MTAISHIA CLOUDSSSSSS FM MSIJE ITWA WAMBEA NA ELIMU ZANI

SITA
NAWATAKIA KILA LA KHERI BWANA WA BARIKI NA KUWALINDA

Kama je wamepelekwa kusoma na waajili wao na waajili wanawasubiri ili kusaidia kuendeleza institutions zao au wanaweza kuwa wajasiliamali, je ushauri wako si sawa na kushindwa kufikiria sababu za elimu kwa ujumla?
 
Mkuu naona hapo umejipendelea zaidi na hujaangalia wingi wa vijana wa kibongo katika state mbali mbali wanaopiga box kama kawaida ambao population yao haiwezi kuwa sawa na hao wa white collar job mkuu

Mkuu naona hapa umefanya generalization kidogo...wewe huna tofauti na wale watu wanaosema wanawake wa kabila x ni malaya, au wanaume wa kabila y ni wabahili....hizi ni generalization tu hakuna scientific proof. Kama sample size yako ina watu 2, au 4 basi ni ndogo mno. I wish ungetokea huku uone mwenyewe jinsi watu wanavyojitahidi. Halfu kitu kingine kizuri kuhusu Marekani watu hawachagui kazi. Sasa nyumbani mtu anasoma Chuo Kikuu umwambie afanye kazi part time Cafeteria, au kazi ya u-custodian....Ouch Umemdharau msomi....nyumbani kutaendelea kuwa nyuma kwa sababu ya kudharau kazi, kila mtu anataka awe bosi.
 
bora kurudi nyumbani kuongeza mapambano ya kuboresha hali kuliko kubaki unamtumikia capitalist huku moyoni unawaza ningekuwa nyumbani .... it is more satisfying kufanya kazi nyumbani. hata frustrations za nyumbani are more bearable and manageable kuliko za ughaibuni. ukiwa home hata ubabaishwe vipi you can easily raise your voice na ukajitutumua kwa uwezo wako wote without fear ya aina yoyote. ughaibuni bado unahisia za being a second class citizen na inferiority fulani hivi. anyway in the end, ndo maana ya home is best

Sio kweli mkuu, tunapigiana kelele kwa kwenda mbele, tatizo hapa hakuna uzembe wa ajabu ajabu. Kwa hiyo Mmarekani akiwa mzembe nina haki ya ku complain nimeshapiga sana kelele sana kwa kutoridhika na huduma tena unapiga simu tu 1-800 number unalalamika na wao wakikundua uzembe unapewa apologies, wakati wa process hakuna mtu anayeangalia wewe ni wa taifa gani, so long as you are a customer. Bongo nimeenda benki (Barclays) na rafiki wa kizungu wale mgambo wanaolinda geti wakanizuia mimi wakamwambie jamaa (my white friend aende), Mzungu akawashangaa akawaambia yeye ni company tu mwenye shida ya huduma ni mimi, jamaa wakaona aibu. Kwanza huku hakuna benki inayolindwa na hao magwandwa, na hata kama ninaenda ku deposit $1 hakuna teller anayeniangalia kwa dharau kama nikiwa Bongo..tatizo Bongo ubishoo kazini to the maximum.
 
Jamani kuondoa umaskini TZ bado kazi ni nzito mana attitude za watu na nchi yao ziko so negative!!! imagine mtu unaencourage brain drain, hao wamesoma badala waje home wawe economically productive unawaencourage watumikie mataifa ambayo they dont belong, waje they should start from scratch watasurvive tu after all we are survivors!! huko majuu zaidi ya kupanda treni za umeme usidhani wanaenjoy kihivyo!

Hatuna ma referees je? na hatuwajui watu kwenye hii system ya "Nipe Nikupe". Hapa U.S. nikipeleka resume yangu mahali so long as I meet the requirements nitapigiwa simu kupangiwa siku na tarehe ya interview ya kwenye simu. Nikifanya vizuri, hiyo Company ita arrange usafiri na malazi kwa ajili ya second interview. Hapo ndio watakapoona sura yangu as a candidate for that position. Bongo vimemo kibao...kazi zipo lakini mpaka uende nyumbani kwa mtu usiku au ukutane nae mahali...Why?
 
Hatuna ma referees je? na hatuwajui watu kwenye hii system ya "Nipe Nikupe". Hapa U.S. nikipeleka resume yangu mahali so long as I meet the requirements nitapigiwa simu kupangiwa siku na tarehe ya interview ya kwenye simu. Nikifanya vizuri, hiyo Company ita arrange usafiri na malazi kwa ajili ya second interview. Hapo ndio watakapoona sura yangu as a candidate for that position. Bongo vimemo kibao...kazi zipo lakini mpaka uende nyumbani kwa mtu usiku au ukutane nae mahali...Why?

Na ukiipata hiyo position unapewa na signing bonus!! Kaeni huko huko
 
Back
Top Bottom