Wazo tu;msirudi tanzania mtajuta

bora kurudi nyumbani kuongeza mapambano ya kuboresha hali kuliko kubaki unamtumikia capitalist huku moyoni unawaza ningekuwa nyumbani .... it is more satisfying kufanya kazi nyumbani. hata frustrations za nyumbani are more bearable and manageable kuliko za ughaibuni. ukiwa home hata ubabaishwe vipi you can easily raise your voice na ukajitutumua kwa uwezo wako wote without fear ya aina yoyote. ughaibuni bado unahisia za being a second class citizen na inferiority fulani hivi. anyway in the end, ndo maana ya home is best
 
Pdady
mbona mi niko hapa
nanimefanikiwa sana tena Acha kuwatisha watu badala ya we kuwaomba warudi waje kujenga TZ we unawakatisha tamaa sasa kwa
mtindo huu tutafika kweli????????
 
Jamani mimi siwezi kuchangia hii thread mpaka Pdiddy atujuze hao alioupload picha zao ni akina nani?
 
bora kurudi nyumbani kuongeza mapambano ya kuboresha hali kuliko kubaki unamtumikia capitalist huku moyoni unawaza ningekuwa nyumbani .... it is more satisfying kufanya kazi nyumbani. hata frustrations za nyumbani are more bearable and manageable kuliko za ughaibuni. ukiwa home hata ubabaishwe vipi you can easily raise your voice na ukajitutumua kwa uwezo wako wote without fear ya aina yoyote. ughaibuni bado unahisia za being a second class citizen na inferiority fulani hivi. anyway in the end, ndo maana ya home is best

...mbona mkuu watu wanalalamika kila kukicha humu jamvini kwamba wabongo tu wapole sana na hatujui kudai haki zetu hasa huko makazini nasikia kuna wengi tunanywea wakati wakenya wakipendelewa waziwazi in terms of pay, promotions etc?
 
...mbona mkuu watu wanalalamika kila kukicha humu jamvini kwamba wabongo tu wapole sana na hatujui kudai haki zetu hasa huko makazini nasikia kuna wengi tunanywea wakati wakenya wakipendelewa waziwazi in terms of pay, promotions etc?
Hii ni kweli na inasikitisha sana mkuu, sasa tutafanyaje kuondoa hii hali?
 
mh hapo ambao tupo nje mnatuonea,but lazima turudi kwenye nchi yetu,tunaimiss,tunaipenda,maisha hata yakiwa magumu but ukiwa kwenu ndo starehe.i love my country na msipende kutenga watu.
 
Nilishawahi kuchangia kwenye thread inayolingana na hii hapa...https://www.jamiiforums.com/interna...kweli-kuhusu-tunaoishi-nje-ya-tanzania-2.html

Re: ukweli kuhusu tunaoishi nje ya tanzania

Wapendwa nitatoa maoni yangu binafsi. Wazo la kuwa nje ya nchi au kusettle nyumbani linachangiwa sehemu kubwa na uchumi. Ni sawa na yule aliye-relocate toka Nchinga-Mtwara kuja Dar es Salaam. Lakini pia kuna suala la feeling za ki-binadamu; hebu fikiri.. umeamua kurudi home baada ya kuangaika sana..na pia umeweza pata kagari kako kamtumba...umepiga kiyoyozi unapita pale kituoni..watu wamejaa ile mbaya hakuna usafiri..roho inakuuma ..Ok,,, unarudi nyumbani ambako umeweka Kagenerator pale nyumbani..baada ya Tanesco kuishiwa umeme..wakati kagenerator kanaunguruma na unapata mwanga..Nyumba ya jirani hakuna umeme..watoto wachanga wa majirani wanalia unasikia huruma ..dhamira inakusuta.unaangalia utawaze kusaidia jirani..lakini masikini kagenerator kenyewe kadogo..Anyway... una kajumba kako umeweka uzio mzuri..lakini kila siku vibaka wanakusumbua.Unaamua kuchukua wamasai..kesho yake wamasai wanafanya nyumba yako ndio Ngome..wanawaleta wenzao kushinda..Unaona karaha unawatimua..Ok.. Unaanza na ka Investment..unapata kahela ambako kanakuwezesha kubadili mboga ....lakini duh! extended family kuna watoto wanataka shule, ndugu wengi maisha magumu..unajitahidi kusaidia unashindwa... Anyway...Unajaribu kujiliwaza kwa kuangalia TV ..au kusikiliza Taarifa ya habari ..unasikia utumbo wa wanasiasa wanaoshindwa kuwathamini wananchi...wanasiasa wanagombana wenyewe kwa wenyewe chama A na B..Mafisadi na walalahoi..Unaudhika kwani kuna ka-chama kanajaribu kuwatetea walalahoi na kuna ka-chama kanajaribu kuwatumia walahoi hao hao kuwatetea maslahi ya matumbo yao na mafisadi..unakasirika na kuzima TV....Unaamua kuondoka.. unatoka kidogo traffic anakukamata..huna tatizo..lolote..kwani Maisha uliyoishi huko nje yamekufundisha kuwa na ka-discipline..Huyu Traffic anazunguka gari.. ..anajenga hoja isiyo na masingi eti Fire Extinguisher ni ndogo kutokana na ukubwa wa gari yako ..Mnabishana sana..Afande anaishia kukwambia ukweli anataka kahela akapate supu..unakasirika unampa unaondoka huku Moyo ukidunda ile mabya yaani kama unataka kutoka nje..una hasira kali....Hapo mbele kidogo unasimama ..unataka upost "status" umeshaamua ku - postpone kurudi settle..home ..Unaandika kwenye Face-book..kwa marafiki zako.. "Aluta -kontinua..Narudi ughaibuni" Binafsi unajipa moyo..wacha nikaangaike kidogo kama miaka miwili au mitatu nitarudi home..Well, ni -round nyingine umeshindwa ku-settle --ingawa ulikuwa na nia ya kweli..

Ndugu zangu, ukiondoka tu Tanzania ..wewe tayari u-second class citizen..hata kama utapata makaratasi, dual citizenship etc. Hasa pale dhamira yako itakapokuwa inakusuta wakati wa lile swali ambalo silipendi... "where r' u from? yaani linakukubusha..Nikiwa nyumbani Tanzania hakuna anayeniuliza hilo swali....

Conclusion -- Umasikini wetu watanzania..na mazingira ya siasa na uchumi wetu vinatuchanganya sana kupata wazo la ku-settle home.. Ingawa, ni kweli ni kuna mifano mizuri ya rafiki zetu wengi ambao wamesha-win baada ya kurudi home.yaani wameweza kujibadili ghafla na kukumbatia tena maisha ya nyumbani..Lakini kama ni kweli tuliishi nyumbani kwenye umasikini na maisha ya dhiki halafu..tukatoka nje ya nchi tuka-experience kuishi kwa utii wa sheria, Kupata hela kwa kipato halali bila kuomba rushwa, kutokuwa na shaka na vibaka, kutosikia Miziki ya mafisadi..Jamani inakuwa ngumu kuchukua maamuzi ya kurudi nyumbani kwani unajua unaenda kutoa rushwa, unaenda kugombana na utii wa sheria..unaenda kwenye umasikini ule ule ambao unajua ni umasikini wa kujitakia...Yaani inachanganya kweli lakini, All in All...Tutarudi tu..kwani ni nyumbani pekee ambako unakuwa "First Class Citizen"​
 
Mi nitabaki hapa hapa Kariakoo, mradi kuna uzima na afya maisha yataenda tu, sio lazima kuajiriwa nakopa huko Jf sacos nauza nyanya chungu, nikipata kahela nanua na kavitz na kakiwanja basi tena....Hakuna cha where are you come from wala nini.
 
ld
swala si kubaki hata ahera utabaki muda ukifika swala ni jinsi gani inaumiza unakuja na elimu yako nzuri ya garama unakuja kulipwa ela za kishenzi na mbaya zaidi anakuja mkenya aliezaliwa morirono kisa tu kingereza chake anakupita mshahara zaidi ya mara tatu na bado tukae kimya lipi bora

ambao amjarudi nyie potezeeni tu tanzania mkiweza
 
Jamani kuondoa umaskini TZ bado kazi ni nzito mana attitude za watu na nchi yao ziko so negative!!! imagine mtu unaencourage brain drain, hao wamesoma badala waje home wawe economically productive unawaencourage watumikie mataifa ambayo they dont belong, waje they should start from scratch watasurvive tu after all we are survivors!! huko majuu zaidi ya kupanda treni za umeme usidhani wanaenjoy kihivyo!
 
Back
Top Bottom