Wazo langu kuhusu uwekezaji kwenye mobile money kufanya manunuzi ya gesi

Machepele

JF-Expert Member
Jun 28, 2019
289
419
Naomba nitumie ile salamu inayozidi kuchukua sura mpya kila kukicha, ambayo mwasisi wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassani (SASHA au SSH).

Ninawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Unaweza kuitikia kimoyomoyo) Kazi iendelee

Mara baada ya salamu nijikite moja kwa moja kwenye jambo langu.

Kama kichwa cha uzi huu kinavyojieleza hapo juu, kuwa nina wazo fulani mzuri tu kwa ninavyoliona mimi binafsi, wazo langu ni kuhusu uwekezaji kwenye mambo ya mobile money kufanya manunuzi ya gesi.

Sijawahi kuandika wazo la mradi Lakini nimejaribu kugoogle nikafahamu ABC ya namna ya kuandika short summary ya wazo la mradi/Biashara, hivyo nimeandika nipo asilimia kama 84%.

Wazo langu litahusisha makampuni na taasisi ya kifedha yafuatayo:
1. Makampuni ya kusambaza gesi za majumbani kama vile Manji Gas, Mihan Gas, Oryx Gas, Lake Gas, O gas nk..

2. Makampuni yanayotoa huduma za simu hapa nazungumzia Vodacom (M-PESA), Tigo (Tigo-PESA), Airtel (Airtel Money), Halotel (Halo PESA), TTCL (T-PESA) nk.

3. Makampuni/Tasisi zinazotoa Huduma za kifedha hapa nazungumzia mabenk. CRDB BANK, NMB BANK, AZANIA BANK, NBC BANK, STANIBIC BANK, ABSA, FNB BANK, TANZANIA POSTAL BANK, AKIBA BANK, ACB nk.

4. Mawakala na wasambazaji wa gas nk.

(a). Ninachoomba kama kuna mtu hapa Jf anaweza nisaidia namna mzuri ya kufanya wazo langu liwe bora ni nitambulike kama mtu mwenye wazo (credit), usajili wa wazo, gharama za kusajili nk.

Ili kama nitamweleza mtu asichukue wazo langu kama lilivyo na kulifanyia utekelezaji, Bila mimi mwenye wazo kunufaika kwa namna yoyote ile hata tu kuwa mentioned kuwa ni mimi mwenye wazo.

Nimeandika hivyo nina mfano hai. Wakati nasoma nachukukua masomo ya ICT ngazi ya cheti pale UCC nilikutana na rafiki yangu mmoja nikamweleza wazo fulani, akalichukua kama lilivyo akaenda kulifanyia kazi kama lilivyo bila mimi kushiriki na wazo likafanikiwa.

(b). Kama kuna mtu hapa JF anaweza kuniunganisha na mtu ambaye yupo katika ngazi za juu kwenye taasisi nilizozitaja hapo juu au makampuni niliyo yataja hapo juu basi nitashukuru sana.

(c). HILI NI KAMA SWALI AU HOJA
Ni kwa nini serikali isiunde baraza/taasisi/idara au kitengo cha ubunifu wa mawazo yenye kuleta mafanikio chanya kwa nchi au jamii. Na watu wenye mawazo tuwe tunaenda kueleza na kufanyiwa uchambuzi kwenye kitengo hicho? Ili kuwasaidi watu hao kuwekeza kwenye mawazo yao na kutengeneza ajira, na kutengeneza walipa kodi wengi zaidi nchini kwetu.

Kuhusu mimi: Ni Mtanzania, Mwenye umri 25, Ninaamini katika creativity, ninauweza kiasi fulani cha kufikiri na kubuni mawazo fulani fulani lakini implementation huwa inashindikana kwa sababu ya mtaji (Financially).​

#Karibuni kwa mchangie
 
Nadhani ungefika Brela kwanza huenda wangekupa ushauri mzuri zaidi kulingana na hoja yako. Hongera sana!
 
Hamna kitu hapo. Mambo ni magumu kote kumebana we Bora utulie tu uuze matunda utapata hela nakuhakikishia.
 
Hamna kitu hapo.mambo Ni magumu kote kumebana we Bora utulie tu uuze matunda utapata hela nakuhakikishia
Au uza vitu vya watoto utapiga hela nikwambie
Asante Mkuu.

Shida yangu ni siyo kwamba sina hela kabisa no no no.

Pesa ya kulipa kodi ya baba mwenye nyumba na kulipa bill ya maji na umeme ninazo. Hili ni wazo tu ambao naona zinaweza kutengeneza au kuongeza fursa nyingi kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom