The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,347
- 11,849
Biblia pamoja na simulizi nyingi za kale kutoka sehemu mbalimbali za dunia zinaashiria uwezekano wa wanadamu wa zamani kuwa na mawasiliano na viumbe wa ajabu waliotoka mbali maarufu kama Ancient Aliens.
::🙁Rejea mada tuliyowaongelea ANUNNAKI).
Simulizi la bustani ya Edeni katika kitabu cha Mwanzo sura ya 3 limekuwa kiini cha tafsiri mbalimbali kwa karne nyingi, likielezwa kama simulizi la "anguko la mwanadamu" kutoka hali ya usafi na utii kwenda kwenye uasi.
Hata hivyo, mtazamo mbadala unaibuka ukisema kwamba badala ya kuwa anguko, tukio hilo linaweza kuwa ni kubadilishwa au kuimarishwa kwa hali ya mwanadamu, hasa kiakili. Hili linaonekana wazi pale tunapotafsiri neno “Elohim” katika wingi wake (si Mungu mmoja, bali "Miungu" au "Wenye Nguvu").
Tafsiri hii inabadilisha kabisa maana ya simulizi hilo: badala ya Mungu mmoja anayekasirika, tunapata picha ya viumbe wa ajabu wenye mamlaka tofauti wakigombania mustakabali wa “mradi binadamu”.
Katika simulizi hilo la Edeni, nyoka ndiye anayeonekana kumshawishi mwanadamu kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya. Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna mahali popote katika simulizi hilo ambapo nyoka anatajwa kama Shetani au Ibilisi.
Kwa nini basi kwa karne nyingi amekuwa akihusishwa na uovu?
Jibu linaonekana katika kitabu cha Ufunuo (Revelation) katika Agano Jipya, ambako maneno "nyoka wa zamani" na "joka" (dragon) yanatumiwa kwa maana ya Shetani.
Hili limechangia sana kuunda picha ya nyoka kama kielelezo cha uovu, ingawa tafsiri hii haipo katika maandiko ya awali ya kitabu cha Mwanzo. Biblia inataja "majoka" au "dragons" mara 34, lakini tafsiri nyingi zimeficha uwepo wake kwa kutumia neno “nyoka,” jambo ambalo limepunguza uelewa wa asili halisi ya viumbe hawa wa ajabu.
Katika maandiko ya kale, hasa ya Kiebrania, tunakutana na viumbe wanaoitwa seraphim, au "nyoka wa moto" (fiery serpents).
Mfano maarufu upo katika kitabu cha Hesabu, ambapo Waisraeli wanapolalamika kwa Musa kuhusu njaa jangwani, Yahweh huwatumia nyoka wa moto kuwaadhibu. Lakini nyoka hawa si wa kawaida—wanaitwa “saraph” kwa Kiebrania, neno linalomaanisha "kuwaka" au "moto."
Katika kitabu cha Isaya, seraphim wanaelezewa kama viumbe wa ajabu wenye mabawa sita: kwa mawili wanaficha nyuso zao, kwa mawili miguu yao, na kwa mawili wanapaa. Moja yao anapaa akiwa amebeba kaa la moto.
Hili linaibua swali kubwa: je, hawa “nyoka wa moto” walikuwa kweli nyoka wa kawaida au walikuwa viumbe wa teknolojia ya juu au wageni wa angani waliotazamwa kwa mshangao na hofu na watu wa kale?
Zaidi ya hayo, baadhi ya watafiti wa historia ya kale na masimulizi ya kitamaduni wanaona kufanana kwa hadithi mbalimbali za asili ya mwanadamu, zote zikianzia kwenye mazingira ya kuangamia kwa dunia au mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa. Hadithi hizi zinaweza kuwa kumbukumbu ya kijamii kuhusu tukio kubwa la kihistoria kama vile Clovis Comet Impact na kipindi cha baridi ya ghafla kilichoitwa Younger Dryas (takriban miaka 12,800 hadi 11,600 iliyopita).
Majanga haya yangesababisha moto wa angani, tsunami kubwa, na baridi kali ya ghafula yote yakibaki katika kumbukumbu za tamaduni nyingi kama kipindi cha hasira ya miungu au mwanzo wa historia mpya ya mwanadamu.
Kwa hivyo, tukilichunguza simulizi la Edeni kwa jicho la tafsiri za kale, muktadha wa kihistoria, na fasihi za mataifa mengine kama zile za Mesopotamia (ambazo ziliathiri sana simulizi la Biblia), tunaweza kuona hadithi hiyo kama simulizi la kuingiliwa kwa mwanadamu na viumbe wa ajabu waliompa maarifa; si la anguko bali la kuinuliwa.
Nyoka wa Edeni anakuwa mjumbe wa ufunuo, si adui wa maendeleo ya mwanadamu.
Tafsiri hii ni yenye utata kwa wengi, hasa kwa waliolelewa katika imani za kidini, lakini inazidi kupata mvuto miongoni mwa wanafalsafa, wachambuzi wa maandiko ya kale, na wanaoamini kuwa historia ya mwanadamu ina sura iliyofichwa kuhusu chimbuko lake halisi!.