..unataka shughuli ya kukuingizia kipato kila uchwao au una utayari iwe inakuingizia baada ya muda Fulani ..
Kama ni ya kila uchwao ( biashara asubuhi jioni mahesabu ) jaribu biashara zifuatazo
1. Bodaboda - comes with highest risk
2. a) Goli la chips/ndizi/mishikaki/kuku - mwanzoni kulingana na eneo utakalojiset itakuwa ngumu mpaka pakishazoeleka
2. b) Goli la chapati/maharage/supu ya ng'ombe ...bado kwa Moro mjini na viunga vyake vijiwe hivi havijasambaa sana
Kama unataka ya msimu nunua nafaka kipindi cha mavuno weka store then uza baadae, hii inataka umakini wa quality checking unaponunua, nafaka kama mpunga, mahindi, maharage , mtama (mweupe au mwekundu) n.k
Biashara nyingine kwa mtaji wako nenda minadani nunua mbuzi safirisha kupeleka Dar, (Anza na mbuzi wachache) ila kwanza pata taarifa na maarifa namna ya kuwafikisha, vibali, n.k