Wazo: Kusoma ni kupoteza muda

Wazo: Kusoma ni kupoteza muda

Mimi naona tunawahitaji wote. Waliosoma sana na wenye elimu ya kawaida. Jambo la msingi la kujiuliza ni kuhusu ubora wa elimu utolewao nchini. Je wahandisi wetu wanaiva kweli? Madaktari Je? Wataalamu wa sheria Je? N. K
 
Bakhera ana elimu gani mkuu?:mtaani kwetu kunao matajiri kama kumi wote hawana shule
Ila amewaajiri waliosoma ndio wanaoendesha makampuni kuanzia Maafisa masoko, Wahasibu, Ma IT, Mainjinia n.k yeye anabakia kuwa Chairman tu ila kazi zote amewaachia Wataalamu(Waliosoma)

Bila hao waliosoma sidhani kama yeye angefikia hapo alipo.

Kusoma sio lazima ila muhimu.

Tajiri aliyesoma na tajiri asiyesoma wanatofauti kubwa sana!
 
Kataa usikatae, kusoma sana ni kupoteza mda
Wengi wanaofanikiwa sana ni wale waliopanga maisha au ambao hawajapoteza miaka yao mashulen
Kwa nchi zilizoendelea kusoma ndio dili sana
Wewe hukusoma ndio maana.Aisee yaani unaona mwisho wa pua yako.Kwa kuwa umepata vihela vyako vichafu vya ngada or whatever unaona kusoma hakuna haja.Si kila mtu anapenda hela chafu wewe.

And then tusingesoma kama wewe Wizara na Taasisi mbali mbali zingeongozwa na nani.Ugali na mboga ungepata wapi,maana hivi vyote vimepatikana kwa kufanya utafiti wa kisomi.Simu na Ndege,nguo nk. tungepata wapi maana waliounda hivi vitu vyote ni wasomi.Acha ujinga na wivu dhidi ya wasomi wewe,nenda kasome.
 
Elimu ni ya muhimu sana maana madaktari amainjinia na walimu pia huwezi wapata bila ya kuwa na Elimu.ila sio watu wote wanaweza pata elimu kubwa mfano masters na phd na uprofesa muda mwingi upotea na wakistuka wakiwa wazee .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kataa usikatae, kusoma sana ni kupoteza mda
Wengi wanaofanikiwa sana ni wale waliopanga maisha au ambao hawajapoteza miaka yao mashulen
Kwa nchi zilizoendelea kusoma ndio dili sana
Bila kusoma hata wewe usingepata hii sehemu ya uliyotolea mawazo yako.
 
elimu ni muhimu sana.. katika kuuondoa ujinga.. ila ukisoma ili uajiriwe jijue wewe ni mjinga wa mwisho pamoja na mavyeti yako..

unakuwa na elimu basic tu kama mengi, dewji, etc.... sio unakuwa na ma masters na phd halafu mjinga kama lipumba au prof muhongo
 
elimu ni muhimu sana.. katika kuuondoa ujinga.. ila ukisoma ili uajiriwe jijue wewe ni mjinga wa mwisho pamoja na mavyeti yako..

unakuwa na elimu basic tu kama mengi, dewji, etc.... sio unakuwa na ma masters na phd halafu mjinga kama lipumba au prof muhongo
Labda wasomi type ya Lipumba ambaye siamini kama anamiliki hata baiskel
 
elimu sio kukaa darasani tu,elimu ni pana sana ata mtu anapokufundisha kuendesha baiskeli, hiyo nayo ni elimu.dhumuni kubwa la kupata elimu ni kumwezesha mtu kuweza kuyaendesha maisha yake kiurahisi yaani apate mwanga utakao mwongoza katika maisha yake,na kwakawaida binadamu tunatofautiana katika uwezo wa kuelewa mambo,ndo maana darasani kuna wakwanza na wamwisho.kuna watu ambao wanaelimu kidogo sana lakini wanamafanikio makubwa katika maisha yao na kuna wengine wanaelimu kubwa lakini mafanikio yao katika maisha ni yakawaida sana,hapo unaweza kugundua kuwa elimu ya darasani na elimu ya kuendesha maisha ni elimu mbili tofauti, lakini zinategemeana kwa kiasi kikubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kataa usikatae, kusoma sana ni kupoteza mda
Wengi wanaofanikiwa sana ni wale waliopanga maisha au ambao hawajapoteza miaka yao mashulen
Kwa nchi zilizoendelea kusoma ndio dili sana
Kwani umelazimishwa kusoma mkuu?! Ukitoa kauli kama hizo ukumbuke pia ukiugua unakimbilia hospitali kwa waliosoma ili wakusaidie kuondoa maradhi yako ya mwili na akili. Kama unaona ni kupoteza muda, fanya maisha kivingine tu. Si lazima wote mfanane.
 
Elimu muhimu acha porojo, kikubwa kutambua kwanini unasoma unachokisomea.
 
Kama kusoma nikupoteza muda bac kutokusoma ni kuongeza muda wa matatizo katika maisha yako, zero wewe unarukia misemo wakati chanzo cha umaskini wetu ni elimu, juzi tu benk ya dunia wamesema hatuna wasomi wa kutosha kuikuza nchi yetu
Wasomi wa kutosha??
Hapo ndo huwa sielewi, serious kuna siku serikali imetangaza nafasi katika sekta fulani eti wasomi wakakosekana??
 
Bakhera ana elimu gani mkuu?:mtaani kwetu kunao matajiri kama kumi wote hawana shule

Swali ndugu yangu labda tukichukua sample ya ambao hawakusoma ni wangapi wapo kama Barkhesa. Mimi naamini utajiri hauna uhusiano na elimu. Unaweza ukasoma ukawa tajiri na unaweza ukawa hujasoma ukawa tajiri. Na vile vile unaweza ukawa hujasoma ukawa sio tajiri na unaweza ukawa umesoma usiwe tajiri. Ila kitu nacho kifahamu ni kwamba ukiwa na akili ya biashara basi shule inaweza ikawa ni kupoteza muda. Lakini kama huna ile wanaita business acumen unahitaji shule labda kidogo. Kuwa tajiri ni akili yako binafsi ya maisha. Ingekuwa kama kutokusoma kuna uhusiano na utajiri basi tungekuwa na watu kama Barkhesa wengi. Na hivyo hivyo kwenye kusoma. Asante.

www.facebook.com/mrictguru/
 
Mafanikio ni nini au yapi?

Mtazamo,malengo na matamanio ndiyo vigezo vya "kufanikiwa au kutofanikiwa".

MTU anayetamani kuwa mhandisi wa mitambo asipofikia hatua hiyo atajiona kashindwa. Haijalishi atakuwa na nini ( elimu,familia,Mali,nafasi ktk jamii).

Kadhalika mwenye lengo/tamanio LA kuwa mfanya biashara,mwanasheria,daktari,mchumi au vinginevyo.

Mafaniko ya mmoja yanaweza yakawa " kushindwa kwa mwingine".

Mfano kuna matajiri,wasomi,wanasiasa na wasanii wengi ambao kwa mtazamo wao binafsi wanajiona "hawajafikia malengo. Lakini kwa upande mwingine ni role model wa wengine( hutamani wafikie viwango vya hao). Je,kwa muktadha huo nani kafanikiwa au la?
Ishi na weka malengo yako,ukiyafikia jipongeze. Haiwezekani wote tukawa Bill Gates,Reginald Mengi,Bakhresa,Maprofesa,Ronaldo/Messi,Obama/Nyerere,Kagame au Pablo Escoba! Hata enzi ya Yesu/Mtume Mohamed wote hawakuwa sawa, na haitatokea!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom