FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,821
Tanzania hivi karibuni kumesikika habari nyingi mbaya za watoto wadogo kupotea. Tusikiapo habari hizo mara nyingi tunazihusisha na mambo ya kishirikina.
Sikatai, ushirikina upo na kwa kiwango fulani unaweza kabisa kuwa na uhusiano na watoto kupotea.
Kwa fikra mbadala...
Tanzania kuna wimbi pia linaibuka, ingawa si kubwa lakini linakua, la vituo vya kulelea "yatima". Nimeweka neno yatima kwenye mabano kwa sababu naamini idadi (asilimia) kubwa ya watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo si yatima. Mimi napendelea kuviita vituo vya "watoto wasio na bahati".
Ni wakati muafaka serikali ivitazàme kwa ukaribu sana vituo hivi kwani vinaweza pia kuwa ni chanzo cha upotevu wa watoto.
Ni wazi kabisa vituo vya kulelea "yatima" vinaendeshwa kwa faida ya waliovianzisha kwa namna moja au nyingine, na chochote kinachozalisha faida ni biashara. Biashara yoyote huhitaji mtaji/mitaji. Mtaji mkuu wa hivi vituo ni watoto, wakipungua au wakikosekana ina maana mtaji unapungua. Mtaji ukipungua au kukosena ina maana biashara hakuna.
Swali, mtaji (watoto) wa hivi vituo wanaupata wapi? Kuna uwezekano njia moja ya kuupata huo mtaji mkuu wa hivi vituo ni kununua watoto?
Tujadili.