Wazo Korofishi: Magufuli Amuondoe Makonda Aende akawe Mwinjilisti!

Mzee Mwanakijiji, kuna wabunge waislam wenye kuvaa kanzu bungeni na wanafanya shughuli zao za kibunge bila ya kubughudhiwa. Ni haki yao ya kiraia.

Siku za ufunguzi wa miradi ya awamu ya tano, Baba Askofu Pengo akiwa kavaa joho la kiaskofu anakaa pembeni ya yule shekhe wa Dar, na hakuna anayejiona kama vile yupo mahali asipotakiwa kuwepo.

Nchi yetu haina dini ingawa watu wake wanazo dini zao - Marehemu Julius Nyerere.
 
Hii si mara ya kwanza kufanya kosa kama hili, hivi karibuni aliwaandalia waislamu futari pale Diamond Jubilee Hall, huku akijua asilimia kubwa waliopo pale ni waislamu akaomba aletewe T-shirt iliyoandikwa JESUS IS MY HOPE.

View attachment 1171793

Huwezi kwenda kanisani na maneno ya kuonyesha wewe ni wa Muhammad ni dharau au Msikitini na maneno ya Yesu ni dharau,Najua Makonda utasoma hapa Acha hiyo tabia mara moja
 
Umenikumbusha zile cheni za dhahabu za Mzee wa Masasi.
 
Shida ni tisheti au maneno yaliyoandwikwa?
Wewe fuatilia tu anayoyafanya achana na Hiyo t shirt yake ila ukiona anayoyafanya ni mazuri juwa Yesu ndio tumaini lake.
 
Badala ya kumwambia Magufuli amuondoe ili akawe mwinjilisti kwanini usimshauri Makonda in polite language namna nzuri ya kutumia mavazi yake kwa jamii?
Makonda ni muhimu kuliko uzi wako wa changamsha genge
 
Gussie,swadakta!
 
Unachosema ni sahihi na kibaya zaidi it seems anatumia dini kama siasa, yaani kuvuta hisia za watu na ndiyo maana kipindi kile akiharibu breki ya kwanza ni church na anamake sure camera zimemchukua akisali kwa hisia ili kuvuta public sympathy
Mlikwisha sema dini na siasa ni mapacha,hao maaskofu wenu uchwara waraka zao zinakujaje kwa serikali?
Ifike mahala muache unafiki
 
Wanajificha kwa Mungu, lakini ndio wauaji wa kutisha hapa Tanzania. Ila iko siku kila ovu litakuwa hadharani.
 
GUSSIE kunywa soda mbili, nitalipa
 
Umeongea pumba tupu.
Barakashia, kanzu ni ustaarabu wa middle east havihusiani na dini
Ndiyo maana hata Nyerere na Mrema walikuwa wakivaa hivyo vibaraghashia,
Tshirt pia siyo tatizo, ila maandishi hayo ukiwa ofisini haijakaa sawa kwa mtumishi wa wote
 
Umenena vyema kabisa
 
Kwenye dress code ya serikali sina hakika kama tshirt inaruhusiwa
 
Si mara moja au mara mbili ninamuona Makonda akiwa amevaa Kanzu na baragashia
ikiashiria imani fulani na hakuna aliyewahi kujenga hoja kama hii,Ni vema tukajikita kwenye mambo ya msingi zaidi itapendeza.
Kinadharia dini zipo ili kuhuisha maisha ya mwanadamu yawe bora. Kwa bahati mbaya sana katika nchi masikini, dini zinageuka kuwa kichocheo cha ujinga kutokana na wengi kutojifunza, kudadisi, kuuliza au kusoma

Kanzu ni neno linaloonyesha aina ya vazi. Ni kama vile ukisema ''kapelo' mtu anajua ni kofia ya aina gani. Sisi watu wa pwani gauni la mwanamke tunaita kanzu. Maana yake ni kuonyesha utofauti wa na mavazi mengine kama vile khanga n.k.

Kanzu siyo Uislam, bali ni vazi linalovaliwa na Waislam kutokana na stara yake inayokidhi mahitaji ya dini katika kujisitiri.

Ni mahitaji kama hayo ndiyo yanayowafanya Makadinali kama Pengo na Maaskofu Wavae kanzu. Yale mavazi wanayovaa ni kanzu kwa maana ya aina ya vazi wala si kitu cha dini

Baraghashia si dini, kofia zilikuwepo tangu enzi na enzi.
Baraghashia ni aina ya kofia na jina hilo tumelipata kwa waarabu chimbuko la Uislam.
Baraghashia haina tofauti na Sombrero, Pama, Kapelo. Ni jina linalotofautisha aina ya kofia

Tena baraghashia zinavaliwa na Waislam na Wakristo.

Vile vikofia vidogo vinavyvaliwa na papa wa Vatican au Makadinali ni aina ya baraghashia fupi kichwani. Asili yake ni kutoka kwa Wayahudi na jina lake ni ''Kippa''

Siku hizi matangazo ya TV ya neno ''Mubashara'' kwa maana ya ''live''
Huo si Uislam, ni neno la Kiarabu, maana yake ni moja kwa moja!

Ni lazima uelewe unaongelea nini na kwa maana gani na tafsiri gani

Ni kutokana na uelewa hafifu na ubutu thabiti wa kutoelewa, wengi hawaelewi hoja ya Mzee Mwanakijiji .

Ile T-shirt ina maneno yasiyo sahihi kwa kiongozi wa umma ambaye Vigagula, vibaka, Waumini na wasio waumini wote ni watu wake

Lakini uzito wa hoja ya MM ni kuwa, kuna message inaweza kutafsiriwa vibaya hasa na watu wenye mitazamo tofauti na kuichonganisha serikali na wananchi

Hivi kwa t-shirt na maneno yale, akitokea mtu akasema serikali ina dini, tutampingaje?

Hivi kwa t-shirt na maneno yale nani anaweza kukemea kuchanganya ''dini na siasa''?

Leo Askofu au Sheikh wakivaa majoho yenye maandishi ya ''ACT Wazalendo na Chadema'' mbingu na ardhi zitatetemeka kwa makemeo ya kuchanganya ''dini na siasa''

Kiongozi akivaa vazi la Jesus is my hope hilo ni sawa kwasababu wao wanaruhusiwa kuchanganya ''siasa na dini''!!!
 
5Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki,
bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.

6 Maneno ya waovu huotea kumwaga damu,
bali maneno ya waadilifu huwaokoa.

7 Watu waovu huondolewa na kutoweka,
bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.

8 Mtu husifiwa kulingana na hekima yake,
bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.

9Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi,
kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.

10 Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake,
bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.

11 Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,
bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.

12 Waovu hutamani mateka ya watu wabaya,
bali shina la mwenye haki hustawi.

13 Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi,
bali mwenye haki huepuka taabu.

14 Kutokana na tunda la midomo yake
mtu hujazwa na mambo mema,
hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza.
 
Mungu akubariki sana...huyu jamaa ana matatizo katika hili nasimama na Makonda...nilitamani kuongeza neno ila umesema yote...unajua ukiwa mshirikina mambo kama haya lazima yakuchukize..
 
Barakashia SIYO nembo ya imani yeyote! Usichanganye madesa! Inaonekana hata hujui mantiki ya thread hii.
 
Tusiende Iraq, huko ni mbali sana. Hapo Zanzibar tu. Nimewahi kusali kanisa Katoliki pale Zanzubar na waumini walikuwa wamevaa kanzu, wengine baraghashia, huku wanawake wakiwa wamevaa hijabu zao.
So, hayo mavazi ni utamaduni tu wa huko middle east wala siyo ishara ya imani fulani. Huchukuliwa kuwa ni ishara ya imani fulani sababu majority ya watu wa eneo hilo ambako utamaduni huo upo wao pia ni wa imani hiyo
 
Kumbe una akili ndogo namna hii kiasi cha kushindwa kuona madhara ya viongozi wa serikali kuvaa mavazi yenye maandishi ya kidini kwenye shughuli za serikali? Kila kiongozi angezuka amevaa mavazi yenye ujumbe wa kidini unafikiri nchi ingeenda wapi? Akili ndogo mpaka unashindwa kuona madhara ya jambo sensitive kama hili?
 
Hapo yupo sokoni tu kwani maandishi ya yesu wewe yanakuumiza nini,yesu si wa kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…