Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,460
- 39,928
PIchani RC Paul Makonda akizuzungumza na wafanyabiashara wa kazi mbalimbali za sanaa ikiwa sehemu ya maandalizi ya ujio wa Mkutano wa SADC. (Picha na habari zaidi kutoka kwa Issa Michuzi. )
Kuna mambo mengine ukiyaangalia yanakufanya ujisikie kufyatuka kidogo. Sina tatizo kwa Makonda kuvaa tshirt au mavazi yoyote yanayoonesha imani yake juu ya Yesu Kristu - Bwana na Mwokozi. Anaweza kuvaa mavazi hayo akiwa nyumbani kwake, akienda zake kanisani au kwenye huduma fulani au hata akiwa likizo.
Nina tatizo na yeye kuvaa vazi hili linaonesha maneno ya "Jesus is my Hope" - "Yesu Tumaini Langu" akiwa katika kitu kinachoonesha ni shughuli ya kikazi au ambapo anafanya kama Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam. Kama Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam siyo jukumu lake kuhubiri Injili au kutangaza imani yake akiwa kazini. Hili ni kweli kwani hata mfanyakazi mwingine wa umma hawezi kwenda kazini asubuhi amevaa tshirt yenye maneno ya kiimani kama hayo.
Huku ndio kunaitwa "kuchanganya dini na siasa" na kuifanya serikali ionekane kama ina "dini". Makonda siyo kiongozi wa kidini hivyo ni makosa ya wazi na yanaoonesha kutokukomaa kisiasa au kiuongozi.
Kama lengo lake ni kutangaza Injili na kushiriki katika huduma ya mavuno basi anaweza kumuomba Rais Magufuli ukipita ugeni wa SADC (au hata mapema) ajiuzulu nafasi yake ili aende kumtumikia Mungu kama Mwinjilisti! Lakini kama ataona vigumu kuomba hivyo basi Rais Magufuli amsaidie kumwarakisha aende kwenye huduma akatangaze habari za wokovu; na kwa jinsi anavyoonekana ana kipawa fulani hivi cha uhubiri. Rais Magufuli amshukuru kijana huyu kwa kazi aliyofanya Dar na ampe likizo hata ya mwaka mmoja (sabbatical) ili aende akahubiri. Akiona inafaa anaweza kumrudisha tena baadaye...
Hili ni wazo korofishi tu...