Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Na. M. M. Mwanakijiji
Ni wazi kuwa kuna kitu kinawasumbua watawala wetu walioshindwa. Hawaamini kuwa wanakataliwa na maelfu kama siyo mamilioni ya Watanzania na kukataliwa huku hakuwaingii kichwani. Baada ya mauaji makubwa kutokea kati ya Oktoba 29 na Novemba 4 watawala wetu hawa wamebakia kujiuliza bila kupata majibu - ya kwanini wanaonekana kukataliwa hadi watu kuwa tayari kutoa uhai wao kuonesha kuwa wamewakataa. Tukumbuke kuwa mojawapo ya siasa mbovu tulizozizoea Tanzania ziliasisiwa na CCM wenyewe; walipotaka kuungwa mkono na mtu au watu walitengeneza mrungula kwanza. Waliwalipa watu ili walipe fadhila za kuwaunga mkono.
Siasa hizi za kulipana zimekuwa maarufu sana ndani ya CCM na kwa muda wake tumeziona zikivuruga siasa zetu kwa kiasi kikubwa. Katika kulipana huku kumekuwa ama kwa fadhila au kwa vyeo na fedha. Ni siasa ambazo zilivuruga uandishi wa habari Tanzania na tumeona miaka ya karibuni ikivuruga hata tasnia ya sanaa ya filamu, muziki na maonesho. Ukitaka kufanikiwa katika fani yako ni lazima kwa namna moja ujikombe kwa watawala na tumeona kiasi kwamba hadi wasanii wenyewe wanajua kabisa kuwa baraka na neema zao zinatoka CCM!!
Hivyo, siasa hizi za kubebana, kulipana na kufadhiliana zimekuwa maarufu sana kiasi kwamba, mtu yeyote anayejitokeza kuipinga CCM anaonekana kama 'hamnazo'. Anathubutuje mtu kusimama na kuwapinga CCM tena kwa ukali wote kama siyo kuwa amelipwa? Kilele cha fikra hizi muflisi tumekiona kufuatia mauaji haya ya majuzi na naogopa kusema kuwa tunaweza kuona ikijirudia tena ndani ya siku chache zijazo.
Alianza Rais na sasa tumeanza kuona wimbo usio na kibwagizo wa "wanalipwa, wamelipwa" ukiendelea kuimbwa nchini. Kwamba, vijana mamia na maelfu nchi nzima walioweza kujitokeza kukataa mchakato mzima wa uchaguzi mkuu walilipwa mamilioni ya hela. Mfano unaotolewa kuwa kuna kijana kalipwa karibu shilingi bilioni 5 siyo tu ni kejeli za utimamu wetu lakini wanataka kutuambia kuwa kuna watu wana fedha sana huko nje ya nchi kiasi cha kutoa mamilioni kwa watu waliojitokeza kuipinga serikali. Tukichukulia tu kuwa mtu mmoja amelipwa bilioni 5 je watu elfu kumi tu walilipwa kiasi gani? Ni wazimu kufikiria kuna mtu ana hela kiasi hicho cha kumlipa kila kijana wa kitanzania aingie mtaani!
Watawala wetu walioshindwa wanaendelea kushindwa kuelewa kuwa kuna watu wanaikataa CCM, ahadi zake, mipango yake, na siasa zake kwa kiapi kabisa kwa wazazi wao. Kuna vitu vimetokea ndani ya utawala wa CCM kiasi kwamba watu wanaona kabisa kuwa wao na sisi hatuwezi kukaa meza moja. Na sasa hivi, kwa vile wamekataa kubeba lawama za mauaji yaliyofanyika chini ya utawala wao wanajaribu kulaumu watu wengine wote isipokuwa wao wenyewe.
Ni kwa sababu hiyo ni vizuri kuwaandaa kiakili na kihisia kuwa kukataliwa kwao ni matokeo ya mambo yao wenyewe. Haitajiki mtu kumlipa mtu mwingine yeyote na wasipoangalia Disemba 9 akili inaweza kuwaingia kidogo maana sasa hivi wao wanaangalia miamala na akaunti za watu; na kama wanaamini watu wanalipwa basi wafunge akaunti zote za fedha kuelekea Disemba 9 ili mtu asilipwe au asilipe halafu waone kama kuna watu watatoka kuwapinga....
Na wakitokea inabidi ukoo wao mzima wajiuzulu.