Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki, akiongea na Mwananchi juu ya ujumbe aliouandika kwenye Akaunti yake ya Twitter, amesema hawezi kuongeza neno juu ya ujumbe alioandika.
Katika Akaunti yake, ameandika kuwa: "Nimeyaelewa vizuri sana maelezo ya Dr. Bashiru kuhusu upigaji kura wa wananchi, uhalali wa Serikali, matamshi ya Viongozi nk. ..... Maneno yale ningeyasema mimi naamini baadhi ya wanachama wenzangu wasingeniacha salama."
Hapa Kagasheki atakuwa anamaanisha akina nani?
Je, hajaingilia tayari integrity ya Wana-CCM wenzake kuwa wanambagua kwa kuwa yeye ni Kagasheki?
Je, hiyo inamaanisha Kagasheki anataka Dk. Bashiru ajiuzulu?