Waziri wa Wizara ya Ulinzi, Bashungwa azindua Bodi ya Shirika la Mzinga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Lugha Bashungwa (Mb) amezindua Bodi ya Shirika la Mzinga lililopo Mkoani Morogoro, Shughuli hiyo iliyofanyika Magadu Mess Mkoani Morogoro, ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali kutoka Makao Makuu ya Wizara, Makao Makuu ya Jeshi pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo.

Bash.jpg


Akitoa taarifa ya Shirika la Mzinga, Meneja Mkuu na Katibu wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Brigedia Jenerali Seif Hamisi, amesema uzinduzi wa Bodi hiyo utasaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Shirika la Mzinga pamoja na kuongeza chachu ya ili kufikia azma na Serikali.

Bash3.jpg


Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga, Luteni Jenerali Samweli Ndomba (Mstaafu), amempongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Innocent Bashungwa kwa namna alivyohakikisha upatikanaji wa wajumbe wa bodi hiyo, kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Bodi alimweleza Mheshimiwa waziri kuwa, Mzinga kama Shirika la Kimkakati litaendelea kufanya majukumu yake ya msingi pamoja na kuongeza ubunifu katika teknolojia na kuongeza wigo wa kuzalisha mazao ya aina tofauti tofauti.

Bashh.jpg


Akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Bodi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Innocent Bashungwa amempongeza Mwenyekiti wa Bodi, Luteni Jenerali Samweli Ndomba (Mstaafu) kwa kuendelea kuaminiwa na kuteuliwa kwa mara nyingine na Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, kwamba inaonesha namna ambavyo Mheshimiwa Rais anayo imani kubwa kwake.

Vile vile Mheshimiwa Waziri Bashungwa amewapongeza Wajumbe walioteuliwa na kusema anayo imani kuwa watatoa mchango mkubwa ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Akihitimisha hotuba yake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameiasa Bodi hiyo kuweka utaratibu wa kutambua juhudi za Wafanyakazi katika idara na vitengo mbalimbali shirikani hapo " Mfanyakazi akifanya vizuri jitahidini kumwambia kazi yako ni njema" alisisitiza Waziri Bashungwa.
 
Back
Top Bottom