Waziri wa Ulinzi wa UK: Kipindi cha mvuno wa amani kimeisha, nchi zijipange kwa vita zaidi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,634
46,277
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza amenukuliwa akisema "the era of the peace dividend is over" kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili ikimaanisha kipindi cha mvuno wa amani kimeisha.

Ameendelea mbali akisema kwa kuangalia tu juu juu hali inayoendelea duniani sasa kuanzia Russia, China, Iran na Korea Kaskazini na migogoro mengine kila mtu atakuwa na jibu endapo miaka mitano ijayo migogoro itaongezeka au kupungua duniani.

Amesema sasa ni wakati wa nchi washirika na za kidemokrasia kuzidisha bajeti zao za ulinzi kukabaliana vyema na hali ijayo.

Hata hapa Tanzania tunapaswa kujipanga vizuri zaidi kiulinzi kwa kuzingatia migogoro inayoendelea kuanzia ndani ya Jumuiya ya Africa Mashariki hadi nje kwa ujumla
 
Yaani wao zaidi ya mataifa 100 wanaojiita wa kidemoghasia

Wanatiwa wasi wasi na mataifa mawili tu yasio ya kidemoghasia ya korea na china kwaushirikiano wa mataifa mawili ya demokrasia zaidi duniani ya shirikisho la Russia na jamhuri ya kiislam ya iran

Ukuwapi usupa pawa wao
 
Baada kufanya toba mnapanga kuuana. Sasa kwa Muumba mtaenda kusema nini?
 
Sisi bado tuna manati ndio silaha zetu
Sijajua bei tunazonunua ni sh ngapi lakini kwa kukisia ni bei ya antiaircrft artillery

Nilichangia mada na kuandika ni mda sasa wa waziri kuongeza bajeti ya ulinzi kwa sababu ya chokochoko za jirani
 
Uingireza huwa ni kijitaifa kilicho jaa ukihelehele sana na kipenda shari hata kuliko Marekani, wakati kinchi chenyewe ni mabomu mawili tu ya nyukilia yanatosha kukizamisha baharini na kikafutika.

Kati ya nchi zote hizo alizo zitaja hakuna hata moja yenye mpango nao lakini ona anavyo zitolea mbovu.
 
Uingereza ni jeshi namba 5 kwa ubora duniani, Mataifa zaid ya 60 hupeleka maafisa wao kupata mafunzo Sandhurst. Hakuna chuo kingine cha kijeshi kinachopekea wanafunzi wengi kama The Royal Military Academy Sandhurst.
 
Yaani wao zaidi ya mataifa 100 wanaojiita wa kidemoghasia

Wanatiwa wasi wasi na mataifa mawili tu yasio ya kidemoghasia ya korea na china kwaushirikiano wa mataifa mawili ya demokrasia zaidi duniani ya shirikisho la Russia na jamhuri ya kiislam ya iran

Ukuwapi usupa pawa wao
Inamaana kama ni mataifa ya kidemokrasia wananchi wao wamepiga kura ya maoni wamechagua vita?
 
Uingereza ni jeshi namba 5 kwa ubora duniani, Mataifa zaid ya 60 hupeleka maafisa wao kupata mafunzo Sandhurst. Hakuna chuo kingine cha kijeshi kinachopekea wanafunzi wengi kama The Royal Military Academy Sandhurst.
Sijaongelea ukubwa wa jeshi nimeongelea ukubwa wa eneo lake ikitokea vita ya kinyukilia atafutika ndani ya muda mfupi sana aache kihelele.
 
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza amenukuliwa akisema "the era of the peace dividend is over" kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili ikimaanisha kipindi cha mvuno wa amani kimeisha.

Ameendelea mbali akisema kwa kuangalia tu juu juu hali inayoendelea duniani sasa kuanzia Russia, China, Iran na Korea Kaskazini na migogoro mengine kila mtu atakuwa na jibu endapo miaka mitano ijayo migogoro itaongezeka au kupungua duniani.

Amesema sasa ni wakati wa nchi washirika na za kidemokrasia kuzidisha bajeti zao za ulinzi kukabaliana vyema na hali ijayo.

Hata hapa Tanzania tunapaswa kujipanga vizuri zaidi kiulinzi kwa kuzingatia migogoro inayoendelea kuanzia ndani ya Jumuiya ya Africa Mashariki hadi nje kwa ujumla
tanzania wajipange ccm na ulinzi na kubaka uchaguzi labda maana hakuna mengine
 
Sijaongelea ukubwa wa jeshi nimeongelea ukubwa wa eneo lake ikitokea vita ya kinyukilia atafutika ndani ya muda mfupi sana aache kihelele.
Vita ni akili na ubora wa silaha, teknolojia na majeshi. Uingereza anavyo vyote. Vita sio suala la ukubwa wa ardhi, Ingekuwa hivyo DRC isingekuwa inasumbuliwa hivyo na Rwanda.
Hii ndio sera ya nuclear ya Uingereza, akili kubwa kuliko nguvu.
"The UK maintains only the minimum amount of destructive power needed to guarantee our deterrent remains credible and effective"
 
Uingereza haina suala la ukubwa wala udogo yaani
Ikitokea wale wakapondwa na nyuklia yaani nilazima wadambaratike
Njia pekee ya kuizuia Uingereza isisambaratike nikuhakikisha mabomu ya nyuklia hayatui nchini kwao
Ila yakifanikiwa kutua tu kwisha habari yao watapunguza madhara ila hayo madogo yatakayopatikanika hayatakua madogo kama udhanianvyo!!!
 
Uingireza huwa ni kijitaifa kilicho jaa ukihelehele sana na kipenda shari hata kuliko Marekani, wakati kinchi chenyewe ni mabomu mawili tu ya nyukilia yanatosha kukizamisha baharini na kikafutika.

Kati ya nchi zote hizo alizo zitaja hakuna hata moja yenye mpango nao lakini ona anavyo zitolea mbovu.
Wheeee! weeee! weeee ati wasema nini The Great Britain, hakunaga inchi yaweza gusaa palee, hiyo ndo nchii imefunguwa wanadamu kwenye hili dunia, ina nguvu kubwa sanaa
 
Dunia haijawahi kuwa na amani huyo Waziri wa ulinzi wa Uingereza ni mpumbavu kama wapumbavu wengine tu.

Russia, China, Iran, Nk hazina muda na nchi yake atulie.

Wao wakiimarisha ushirikiano wa kiulinzi na kuanza kuvamia nchi za watu hovyo hovyo na kufanya regime change wanaita demokrasia ila wenzao wakiimarisha ushirikiano wa kiulinzi wanaita vita imesogea ulimwenguni.

Dunia ya sasa sio ya miaka 70 iliyopita propaganda za kishenzi kama hizi zimepitwa muda atulie.
 
Umetokwa povu jingi sana!
 
Migogoro imesambaa sehemu nyingi Duniani kuliko kipindi chochote tangu mwisho wa Vita ya pili ya Dunia, Kama hali itaendelea hivi analosema prime Minister lina uwezekano wa kutokea.
 
Vita ni akili na ubora wa silaha, teknolojia na majeshi. Uingereza anavyo vyote. Vita sio suala la ukubwa wa ardhi, Ingekuwa hivyo DRC isingekuwa inasumbuliwa hivyo na Rwanda.
Hii ndio sera ya nuclear ya Uingereza, akili kubwa kuliko nguvu.
"The UK maintains only the minimum amount of destructive power needed to guarantee our deterrent remains credible and effective"
Tatizo hujanielewa mantiki yangu

Hiyo akili itaweza kuzuia mlipuko wa nyukilia na mionzi isisambae baada ya hilo bomu kutua kwenye ardhi yake?
Mfano leo hii ikitokea vita ya kinyukilia nchi kama Urusi na Marekani kuna baadhi ya maeneo yatanusurika kwa sababu ya ukubwa wake wa kieneo tofauti na Uingereza ambayo kieneo chake ni kidogo.

Inabidi aache kiherehere maana hii tabia zake za uhasama zitafanya awe target ya kwanza pale vita ya kinyukilia itakapo tokea.
 
Back
Top Bottom