Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa pamoja na wabunge wasafiri kwa treni toka Dodoma hadi Dar.

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa pamoja na kamati ya wabunge wasafiri kwa treni toka Dodoma hadi Dar katika zoezi la kujionea miundo mbinu ya njia hiyo ya treni ambapo inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha Standard_Gauge, ujenzi utakaoanza Mwezi December mwaka huu ambapo baada ya kukamilika kwake;

Prof. Mbarawa amesema kwamba treni zinazotarajiwa kupita katika reli hiyo zitakuwa na uwezo wa kutembea kwa mwendokasi wa spidi kati ya 120 hadi 150 na itachukua takribani saa 2 toka Dar hadi Morogoro na saa 4 toka Dar hadi Dodoma.

image.jpeg

image.jpeg

image.jpeg

Chanzo: Chanel Ten habari.
 
Vijiji vingi na mbuga na wanyama wanaofugwa wanakatiza sana kwenye hizi njia za treni katika shughuli zao na maisha ya kila siku hivyo spidi ya treni ikiwa kubwa inaweza kuleta madhara. Elimu yakutosha inahitajika kwa jamii kuwa na tahadhari mapema kwenye maendeleo haya ya sayansi na teknolojia ya kisasa. Hongera kwa Prof Mbarawa kuwa mfano bora katika wizara yako
 
mimi nilijua itakuwa ile ya kupita kwenye handaki!
 
mikatabafeki;
Utanishitaki kwa lipi hapo ka sio kuoneana. Sijamtaja mtu wala cheo chako nimewaza tu jinsi Tz tulivyo wepesi kutangaza mafanikio hata kabla ya kuotesha nyanya.
kwanini hii reli haijawa ya ardhini jamani nchi kavu huku si itakuwa hatari sana? Na miundo mbinu pia itakuwa salama kweli dhidi ya wezi?
 
  • Thanks
Reactions: MC7
mimi napata ukakasi hapo kwenye hizo spidi 120 mbona kama mwendo wa lori? Nilijua ni kuanzaia spidi 360

Vijiji vingi na mbuga na wanyama wanaofugwa wanakatiza sana kwenye hizi njia za treni katika shughuli zao na maisha ya kila siku hivyo spidi ya treni ikiwa kubwa inaweza kuleta madhara. Elimu yakutosha inahitajika kwa jamii kuwa na tahadhari mapema kwenye maendeleo haya ya sayansi na teknolojia ya kisasa. Hongera kwa Prof Mbarawa kuwa mfano bora katika wizara yako

Wewe umeona ni speed kali kuna mwingine ka comment huko juu kasema ni speed ya Lori
 
kwanini hii reli haijawa ya ardhini jamani nchi kavu huku si itakuwa hatari sana? Na miundo mbinu pia itakuwa salama kweli dhidi ya wezi?

Mkuu nilifurahi tu pale huyo waziri alipomtembelea yule jamaa aliyejenga house juu ya reli. Sijui amemlipa fidia kabla ya kuanza huu ujenzi mpya kwani uliwahiwa na hiyo nyumba. Tungojee lakini, December sio mbali
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Back
Top Bottom