Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar anazungumza na Wanahabari, Machi 2, 2026

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar anazungumza na Wanahabari, Machi 2, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohame : Ndani ya siku 100 za Rais Dkt. Mwinyi tumekusanya mapato ya 192,997,450 yanayotokana na Makosa ya usafiri wa ardhini Lengo letu si kukusanya mapato tunataka kudhiti makosa



Waziri Dkt. Khalid Salum Mohame: Katika usafiri wa anga na viwanja vya ndege tunatekeleza ibara ileile ya ibara 102 ya ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi 2025-2030.
Maelekezo ni kwamba:
  • Tuongeze idadi ya abiria wanaopita kwenye viwanda vyetu vya ndege ambapo lengo lilikuwa kutoka 2, 140, 988 ikifika 2030 tufikie abiria 2,824,011 lakini kwa sasa kwa mwaka wanapita 2,500, 000 na ndani ya siku mia moja abiria wamefika 878,698. Tunafikiria kwamba kama mambo yatakaa sawa abiria watakuwa 3, 000, 000 kuvuka malengo ya ilani.
  • Katika uwanja Abeid Amani Karume tunataka kujenga karakana kuu ya matengenezo ya ndege.
  • Ndani ya siku 100 tumekamilisha jengo la biashara kwani huduma za usafiri wa anga unazidi kuhitajika.
  • Tuna ujenzi wa vituo viwili vya mafuta, tunaendelea kujenga lengo tuwe na vinne
  • Tunaendelea kujenga logistics centre
  • Pia kuna ujenzi wa maegesho mapya ya ndege code C na Code D
  • Tumeanza matayarisho kujenga Airport nyingine kubwa, Nungwi
  • Tuna mipango ya kujenga jingine la abiria Terminal 4
  • Uwanja wa ndege Pemba unaendelea kujengwa kuifungua Pemba kiuchumi kama alivyohaidi Rais Mwinyi na tayari kwa siku 100 wameshajenga mita 600 upande wa kaskazini
  • Ndani kipindi hiki tumeanza maandalizi ya jengo la ofisi ya Mamlaka ya viwanja vya ndege.
Katika usafiri wa Majini/ bahari
  • Tunaendelea na ujenzi bandari
 
Back
Top Bottom