lingamba lidodi
JF-Expert Member
- Nov 15, 2018
- 964
- 1,137
Heri ya mwaka upya2019. Wakati inajengwa miundombinu ya mwendokasi,tulitegemea kuondokana na kero ya usafiri kwenye jiji la Dars s msaalam. Serikali ikazuwia daladala kupita na kufika baadhi ya maeneo.
Tofauti na tulivyotegemea,sasa hivi usafiri wa mwendokasi umekuwa kero mpaka wakazi wa Dar wamekumbuka daladala zao. Ili upande mwendokasi ni lazima ujitoe ufahamu,huko ndani watu wanajazana mithiri ya mihongo ikisafirishwa kutoa mkuranga.
Ni lazima uwe na nguvu za kupanda na kushuka. Kwa wale walioshauriwa na madaktari kufanya mazoezi kwa ajili ya kuondoa mafuta mwilini,mwendokasi inawafaa sana,maana siyo kutoa jasho tu bali kumwagika jasho.
Ni vizuri serikali kupitia wizara yenye dhamana iangalie jinsi ya kuufanya usafiri huu kuwa wa kisasa zaidi na matumizi yake yawe bora yenye heshima na staha kwa mtanzania. Usafiri hata wa Nguruwe una nafuu!
ONGEZENI BASI WATU WAKAE LEVEL SEAT, KAMA PESA HAZIPO RUHUSUNI DALADALA KWENYE NJIA MLIZOZUWIA.
Lakini kwa hali ya sasa usafiri wa mwendo kazi unamzalilisha mtanzania. Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app