Waziri wa TAMISEMI, shusha rungu huku halmashauri. Wapigadili wanabugia pesa za walimu ajira mpya

Yaani unapoajiriwa andaa file kabisa LA mambo ya halmashauri maana hawachelewi kukupiga, mimi namatatizo nao makubwa na tutafikishana nao mbali maana wamejaribu kuniibia wameshindwa
hahahahaaaa!
wanajaribu kukuibia ila wanashindwa, kwanini wasikuache kisha wakawaibia wale wapole? ina maana wao hawasomi ramani kabla ya kufanya uporaji?
 
hahahahaaaa!
wanajaribu kukuibia ila wanashindwa, kwanini wasikuache kisha wakawaibia wale wapole? ina maana wao hawasomi ramani kabla ya kufanya uporaji?
Hivi inawezaje ukakopa alafu makato hayaendi hazina na wanapeleka wapi? Ntawafungulia kesi waache tu
 
Kikubwa huwa wanaamini walimu ni watu wasiokuwa na shida ni watu wa kuwaonea maana wanajua hawawezi kufanya fujo yoyote na huamini walimu wengi ni wanyonge na hawajui kudai haki. Ajira zilipotolewa mara ya mwisho na Kikwete kuna walimu walipewa fedha ya kujikimu laki moja na 20 na nyingine hawakupewa mpaka kesho na kosa lao lilikuwa kusaini hivyo hawawezi kushtaki kokote maana wataambiwa walipewa zote.
 
Mi naona ni vizuri TAMISEMI kwa ajira zinazofuata watoe utaratibu wa kuwa mwenye elimu ngazi gani na aliyepangiwa halmashauri gani apewe kiasi gani kama fedha ya kujikimu hii itasaidia kupunguza wizi huu sasa wanapotoa kimya kimya watu wanashindwa kuanzia wapi kudai na hawana uthibitisho kuwa anapaswa apewe kiasi gani cha fedha.
 
Kutokama hali ya kimasiaha ya mwaka huu kutoautiana na ya mwaka juzi ambapo walimu wa ajira mpya waliajiriwa, serikali yetu kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imeamua kuongeza fungu ktk pesa ya kujikimu ya walimu. Ushahidi wa hili ni kutokana na baadhi ya halamashauri nyingi kutoa au kuahidi kutoa kiasi halali cha Tsh. 700,000 kilichotolewa na serikali yetu pendwa kama pesa za kujikimu kwa kila mwalimu wa ajira mpya wenye degree, na Tsh. 560,000 kwa walimu wenye diploma. Halamshauri hizo ni kama:
  1. halamshauri ya manispaa ya Kasulu
  2. halamshauri zote za Dar es Salaam
  3. halamashauri ya manismapaa ya Iringa
  4. halmashauri ya jiji la Tanga
  5. halmashuri ya wilaya ya Lushoto
  6. etc
Ila zipo baadhi ya halmashauri zenyewe kwa kuzoea kupiga dili, wameamua kubugua pesa za walimu, na kuwapia walimu pesa pungufu, hali inayowafanya walimu kuhisi kuonewa hivyo kushusha morali yao ya kujituma kazini. Halmashauri hizo ni kama:
  1. halamshauri ya wilaya ya kibondo, wametoa Tsh. 420,000 kwa mwalimu wa degree,
  2. halamshauri ya wilaya ya uvinza, wametoa Tsh. 420,000 kwa mwalimu wa degree,
  3. halmashauri ya wilaya ya mbeya, wametoa Tsh. 560,000 kwa walimu wa degree
  4. halamshauri ya wilaya ya Itilima, wametoa Tsh. 560,000 kwa walimu wa degree
  5. etc
Kuna watu watasema kua kuna tofauti ya malipo kwa halamshuri za manispaa na za wilaya, ila ukweli ni kwamba, mwaka huu hakuna huo utofauuti. Hii imekuja ili kuwapa motisha walimu wanaoenda kufanya kazi vijijini, waone kama wamependelewa kupewa kiasi sawa na wale wanaofanya kazi mjini kwenye gharama kubwa za maisha. Ona mfano huu hai:
  • halamashauri ya wilaya Lushoto wao wameahidi kwa kuonyesha dokument, kua watawalipa walimu wa ajira mpya wenye degree kiasi cha Tsh. 700,000, ambayo ni sawa na zile zinazotolewa na halamshauri za manispaa.
Zipo halamshauri zimezoahidi kubugia pesa za walimu na kuwapa walimu hao pesa pungufu. Hamashuri hizo hazijali kushusha morali za walimu wapya na zinaona kwao sio jmbo baya kubugia pesa kwa ufisadi. Halmshauri hizo ni:
  1. halamshauri ya wilaya ya Bariadi
  2. halamshauri ya wilaya ya kyela
  3. halamshauri ya wilaya ya Missenyi
  4. halamshauri ya wilaya ya Nkasi
  5. halmshauri ya wilaya ya Iringa
  6. etc
Wewe mwalimu mwenzangu wa ajira mpya, tushirikiane kuzoorodhesha halamshauri zote zilizobugia pesa za walimu, na zile zinazopanga kubugia pesa za walimu, ili mamalaka za juu ziwachukulie hatua.

Tunaomba mamlaka ya juu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, iwachukulie hatua hawa wapigadili wasiotaka kubadilika kuendana na kasi iliopo.
Kamanda ENANTIOMER hizo halmashauri zilishazoea. Nakupa uzoefu wa KIBONDO.
Mwaka flani hivi tulipoanza ajira serikali walileta hizo pesa za kujikimu kwa walimu. Ukiripoti baada ya taratibu flani hivi unapewa mzigo wa kitita unaenda kutoa vumbi manake kibondo ina vumbi sana.

Pia mwaka ule serikali ilileta pesa za usafiri, pesa zile zilitakiwa kulipwa kulingana na umbali unaotoka. Kuna waliotoka kilwa, mtwara, mara, tanga, dsm. So wanapiga hesabu km zako na aina ya mizigo na usafiri. HAPO NDIO PALIKUWA NA KASHESHE SASA.

Kibaya walimu wengi walikuwa dip na degree hivyo uelewa ulikuwa mzuri kidogo. Ile vita ilikuwa kubwa sana, kila siku watu wanafanya maandamano kuja kwa Afsa Elimu secondary (Alex). Sio kwamba walitaka kuzikata, walitaka wasitoe kabisa, kwamba utaratibu huo hautuhusu sisi na pesa imeletwa kimakosa.

Watu wakaingia mzigoni zikapatikana nambw za Waziri wa tamisemi, wakati ule alikuwa Ghasia nafkiri na Waziri Mkuu Pinda, kipindi hicho walikuwa bungeni, wakapigiwa simu wakapewa mkasa mzima, hadi kufika asubuhi hundi zote zipo tayari na jamaa wamekasirika hatari, wanalaumu kwanini tulipiga simu kwa mawaziri.

Aliyekuwa anastahili kupata 1.6m alipata 1.2 au 1.3 basi ikawa mziki umeishia hapo na wale waliokimbia kabla ya mshiko pesa zao zililiwa.

Kibondo kwa sasa kuna mama Kabunduguru, huyu niwapande zile za mzee magu, ni muhangaza, alianza kwa mbwembwe sana ila kwa sasa naskia ameanza kunyooka.

Katika halmashauri ngumu kufanya kazi yoyote Kibondo ni miongoni mwao
 
Halmashauri ya jiji la tanga na halmashauri ya manispaa kasulu kulipa 100,000 kwa siku kwa mtu mwenye degree sio kwa sababu ya umakini bali ndiyo matakwa ya sheria.

Manispaa na majiji yote kwa mtumishi mwenye degree anapaswa alipwe 100,000 kwa siku na mwenye diploma ni 80,000

Kwa halmashauri za Wilaya ambazo sio majiji wala manispaa, mtumishi mwenye degree stahiki yake ni 80,000 kwa siku.

Ni vema ukaomba upewe waraka wa posho za kujikimu kuliko kulaumu watu kuwa wamekula hela zenu tu.

Kazi yenyewe hujaanza tayari ushakuwa mtovu wa nidham hivyo.
Mishahara je? Walio kwenye majiji wanalipwa zaid ya walio halmashauri
 
Lakini pia, Halmashauri ya wilaya Lushoto, ambayo imewaonyesha walimu wa degree, document iliyoandikwa 100,000 kwa siku, je hao wana waraka wao? Tupe waraka wa mwaka huu unaoonyesha malipo ni kama hayo uliyoyataja.

Kiufupi wapigadili wanapiga dili, na ndio maana unaona kuna halamashauri kama Uvinza na Kibondo na nyingine ya mkoa wa Mara, wao wamelipa walimu wenye degree elfu 60,000 tu kwa siku, ambayo ni kinyume na hata hayo maneno yako ya utetezi kwao.
Kipindi kile serikali walikuwa hawalipi posho, ni pesa zakujikimu. Walikuwa wanalipa kutokana na ngazi ya elimu na sio mahala ulipo. Ndio maana waraka ukitoka kama una familia mkeo analipwa sawa na wewe, mtoto analiopwa nusu yako. Kama ulitakiwa kulipwa 500,000 na una mke na watoto 2, hapo utaondoka na 2,000,000/=.

Utaratibu wa sasa hatujui ukoje kwa kweli. Inawezekana serikali wakaweka flat rate kwa wenye viwango sawa vya elimu bila kuangalia mahala walipo.
 
Kuna Halmashuri imeshindwa kulipa mishahara ya wauguzi sababu ya bajeti finyu..sasa hiyo hela ya kupiga wanaitoa wapi?
 
Hela ikiwa pungufu hakuna kusaini na unapaswa utoe taarifa hawa wahasibu hiki kipindi cha walimu wa ajira mpya wanakipenda kweli kunyonya wengine
Wakati ule kuna jamaa aliripoti akaenda kwanza kituoni, baada ya wiki akafuata pesa zake, akakuta wameshazisaini, akawaambia hapa naondoka na kichwa cha mtu, aliyesaini anipe pesa zangu.

Jamaa waliona inawezekana jamaa hakuripoti, kumbe jamaa yupo kituoni anasoma mazingira. Walimpa pesa zake akajitafutia kuku
 
Barua yoyote utakayoandika kwenda kwa hao wendawazimu ipige kopi na uiweke kwenye faili lako nyumbani. Na barua yoyote utakayopokea iweke vizuri sana.
Asante kwa ushauri. Sijaandika barua ya kuomba pesa, ila nikiandika, nitapiga kopi
 
kumbe gharama za maisha za mwl kwa siku ni 100000 kwa mwalimu wa degree??? hahahaass sasa mbona mshahara anaopewa mfukoni hauzid 500000 kwa mwezi hahaaa nimecheka sana waangalie kotekote
 
Kama halmashauri ya wilaya ya Missenyi wakitaka kutupa pesa pungufu, nitampiga picha yule afisa aliyeonyesha nia ya kubugia pesa zetu tangu mapema, kisha nimuweke humu mumuone mwizi wetu. Kwakweli wezi siwapendi kabisa:(
Thubutu yako upige picha
Kama ubavu huo unao Fanya sasa
Wewe unafikiri tupo chuo
 
Halmashauri ya jiji la tanga na halmashauri ya manispaa kasulu kulipa 100,000 kwa siku kwa mtu mwenye degree sio kwa sababu ya umakini bali ndiyo matakwa ya sheria.

Manispaa na majiji yote kwa mtumishi mwenye degree anapaswa alipwe 100,000 kwa siku na mwenye diploma ni 80,000

Kwa halmashauri za Wilaya ambazo sio majiji wala manispaa, mtumishi mwenye degree stahiki yake ni 80,000 kwa siku.

Ni vema ukaomba upewe waraka wa posho za kujikimu kuliko kulaumu watu kuwa wamekula hela zenu tu.

Kazi yenyewe hujaanza tayari ushakuwa mtovu wa nidham hivyo.
Exactly hapo umesema kweli na pia waangalie rate ambazo zinalipwa kwa miji mikuu ,manispaa na majiji pamoja na halmashauri za miji. Ingawaje kwa ajira ya mwaka 2011 walimu Wote walipewa flat rate ila ya usafiri na mizigo ndio ilitofautiana
 
Marhabaa kijana unayetaka kuibiwa. Wezi tunaishi nao na tunacheka nao kila siku. Hao ni sawa na Majambazi yanayoua askari wetu na raia wenzetu. Tukio la kumuimbia mtu, linakaribiana na tukio la kuua mtu.
Hata kwetu Sengerema DC naona kama sielewielewi hivi. nimeamua kuacha kuwaandika hapa, kwakua kesho nitaenda kuwahoji ili nipate uhakikika kama na wao wanataka kutuibia au laa!
sengerema leo tumeambiwa pesa bado haijaja na tumeambiwa tuwe wavumilivu bro.. hali ni tete mpaka sa iv hatujui tutapata hela lini??
 
Back
Top Bottom