Waziri wa TAMISEMI, shusha rungu huku halmashauri. Wapigadili wanabugia pesa za walimu ajira mpya

ENANTIOMER

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
1,419
804
Kutokama hali ya kimasiaha ya mwaka huu kutoautiana na ya mwaka juzi ambapo walimu wa ajira mpya waliajiriwa, serikali yetu kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imeamua kuongeza fungu ktk pesa ya kujikimu ya walimu. Ushahidi wa hili ni kutokana na baadhi ya halamashauri nyingi kutoa au kuahidi kutoa kiasi halali cha Tsh. 700,000 kilichotolewa na serikali yetu pendwa kama pesa za kujikimu kwa kila mwalimu wa ajira mpya wenye degree, na Tsh. 560,000 kwa walimu wenye diploma. Halamshauri hizo ni kama:
  1. halamshauri ya manispaa ya Kasulu
  2. halamshauri zote za Dar es Salaam
  3. halamashauri ya manismapaa ya Iringa
  4. halmashauri ya jiji la Tanga
  5. halmashuri ya wilaya ya Lushoto
  6. etc
Ila zipo baadhi ya halmashauri zenyewe kwa kuzoea kupiga dili, wameamua kubugua pesa za walimu, na kuwapia walimu pesa pungufu, hali inayowafanya walimu kuhisi kuonewa hivyo kushusha morali yao ya kujituma kazini. Halmashauri hizo ni kama:
  1. halamshauri ya wilaya ya kibondo, wametoa Tsh. 420,000 kwa mwalimu wa degree,
  2. halamshauri ya wilaya ya uvinza, wametoa Tsh. 420,000 kwa mwalimu wa degree,
  3. halmashauri ya wilaya ya mbeya, wametoa Tsh. 560,000 kwa walimu wa degree
  4. halamshauri ya wilaya ya Itilima, wametoa Tsh. 560,000 kwa walimu wa degree
  5. etc
Kuna watu watasema kua kuna tofauti ya malipo kwa halamshuri za manispaa na za wilaya, ila ukweli ni kwamba, mwaka huu hakuna huo utofauuti. Hii imekuja ili kuwapa motisha walimu wanaoenda kufanya kazi vijijini, waone kama wamependelewa kupewa kiasi sawa na wale wanaofanya kazi mjini kwenye gharama kubwa za maisha. Ona mfano huu hai:
  • halamashauri ya wilaya Lushoto wao wameahidi kwa kuonyesha dokument, kua watawalipa walimu wa ajira mpya wenye degree kiasi cha Tsh. 700,000, ambayo ni sawa na zile zinazotolewa na halamshauri za manispaa.
Zipo halamshauri zimezoahidi kubugia pesa za walimu na kuwapa walimu hao pesa pungufu. Hamashuri hizo hazijali kushusha morali za walimu wapya na zinaona kwao sio jmbo baya kubugia pesa kwa ufisadi. Halmshauri hizo ni:
  1. halamshauri ya wilaya ya Bariadi
  2. halamshauri ya wilaya ya kyela
  3. halamshauri ya wilaya ya Missenyi
  4. halamshauri ya wilaya ya Nkasi
  5. halmshauri ya wilaya ya Iringa
  6. etc
Wewe mwalimu mwenzangu wa ajira mpya, tushirikiane kuzoorodhesha halamshauri zote zilizobugia pesa za walimu, na zile zinazopanga kubugia pesa za walimu, ili mamalaka za juu ziwachukulie hatua.

Tunaomba mamlaka ya juu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, iwachukulie hatua hawa wapigadili wasiotaka kubadilika kuendana na kasi iliopo.
 
Shikamoo uliyendika huu uzi. Huku kwetu Missenyi DC tunaona giza sana. kuna afisa nilimsikia anasema atatoa elfu 60 kwa walimu wa degree kwa siku, sawa na 420,000 kwa siku saba. Huyu afisa anataka abugie pesa zetu zote avimbiwe. Ama kweli kuna watu waliumbwa ili wawe wezi.
Marhabaa kijana unayetaka kuibiwa. Wezi tunaishi nao na tunacheka nao kila siku. Hao ni sawa na Majambazi yanayoua askari wetu na raia wenzetu. Tukio la kumuimbia mtu, linakaribiana na tukio la kuua mtu.
Hata kwetu Sengerema DC naona kama sielewielewi hivi. nimeamua kuacha kuwaandika hapa, kwakua kesho nitaenda kuwahoji ili nipate uhakikika kama na wao wanataka kutuibia au laa!
 
Mmh je muandishi umefanya utafiti kujua sababu au umekurupuka tu duh hili ni tatizo la watanzania kila mmoja anajua vitu vyote fuatilia ujue sababu inawezekana halamshauri nyingine zineongeza kutoka kwenye ownsource na nyingine hazina uwezo huo
 
Bora yenu mnapewa hata hizo pesa maana wengine hatujawahi pewa toka kuajiriwa wala pesa za nauli
 
Thibitisha kuwa TAMISEMI wametoa pesa ya kujikimu kwa viwango Sawa bila kujali mtumishi yupo manispaa /jiji, makao makuu ya mkoa au Wilaya

Lete uthibitisho hapa, otherwise utakuwa unawachafua watu tu
 
Haiwezekani halamashauri nyingi zilizo makini, zote ziongezee mpaka kufikia Tsh. 700,000. Hizo halamshuri makini zingetofautinan ktk kuongezea ktk kile zilichokipokea ktoka tamisemi, na hivyo jumla ya pesa zingetoautiana na sio zote kua laki saba.
Kwanza halamshauri zina miradi mingi sana ya kutekeleza, hivyo haziwezi fikia hatua ya kuwaongezea pesa walimu ambao wamepewa pesa na serikali kuu. Kikao gani cha madiwani kilichopitisha hizo pesa za kuongezea?
Kama wewe ni mmoja wa waliobugia pesa za walimu, tafuta ujanja wowote uwambie walimu uliowaibia waje kuchukua kiasi kilichobaki.
 
Thibitisha kuwa TAMISEMI wametoa pesa ya kujikimu kwa viwango Sawa bila kujali mtumishi yupo manispaa /jiji, makao makuu ya mkoa au Wilaya

Lete uthibitisho hapa, otherwise utakuwa unawachafua watu tu
Halmashauri za majiji (mfano Tanga) na manispaa makini (mfano Kasulu) wametoa kiasi cha Tsh. 100,000 kwa siku, hivyo julmla kua Tsh. 700,000 kwa siku 7 kwa kila mwalimu mwenye degree. (kama hujui, fuatilia ktk halamshauri za majiji na manispaa tajwa hapo juu ili ujue)
Pia hamashauri ya wilaya ya Lushoto wamewaonyesha walimu wapya document inayoonyesha kua kia mwalimu wa degree atakipwa Tsh. 100,000 kwa siku, hivyo jumla kua Tsh. 700,000 kwa siku 7. (kama hujui, nenda Lushoto ukaulize, au waulize waliopangiwa Lushoto.
Kufanana kwa malipo kati ya halmshauri za majiji, za manispaa na za wilaya kama nilivyoonyesha hapo juu, kunathibitisha kua, kiasi kilichotolewa na serikali kuu kupitia Ofisi ya Rais TIMISEMI ktk halmashauri zote ni kiasi sawa, ila kuna baadhi ya halmashauri wanahisi mpaka sasa bado tuko gizani na hivyo kuendelea ja taratibu zao za kubugia pesa za walimu.

Naona hapa nimegusa ulaji wenu, ila hakuna namna. Tafuteni mbinu muwaite walimu mliowaibia, muwape kiasi mlichowaibia.
 
Bora yenu mnapewa hata hizo pesa maana wengine hatujawahi pewa toka kuajiriwa wala pesa za nauli
Poleni sana. Nanyi mliibiwa na hao wapigadili. Na sasa hao wapigadili wanahisi kasi ya upepo bado ni ile ile, hivyo wameendelea kuiba kama kawaida yao. Sijui wanapima kina cha maji, au walishayaona kama yanakina kifupi. Tusubiri tuone hatma ya mazoea yao ya wizi.
 
Halmashauri ya jiji la tanga na halmashauri ya manispaa kasulu kulipa 100,000 kwa siku kwa mtu mwenye degree sio kwa sababu ya umakini bali ndiyo matakwa ya sheria.

Manispaa na majiji yote kwa mtumishi mwenye degree anapaswa alipwe 100,000 kwa siku na mwenye diploma ni 80,000

Kwa halmashauri za Wilaya ambazo sio majiji wala manispaa, mtumishi mwenye degree stahiki yake ni 80,000 kwa siku.

Ni vema ukaomba upewe waraka wa posho za kujikimu kuliko kulaumu watu kuwa wamekula hela zenu tu.

Kazi yenyewe hujaanza tayari ushakuwa mtovu wa nidham hivyo.
 
Tukianza na Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, ambayo wao wametoa Tsh. 60,000 kwa siku, kwa walimu wenye degree. Unawazungumziaje hao, ni wapigadili au sio wapigadili?
 
Halmashauri ya jiji la tanga na halmashauri ya manispaa kasulu kulipa 100,000 kwa siku kwa mtu mwenye degree sio kwa sababu ya umakini bali ndiyo matakwa ya sheria.

Manispaa na majiji yote kwa mtumishi mwenye degree anapaswa alipwe 100,000 kwa siku na mwenye diploma ni 80,000

Kwa halmashauri za Wilaya ambazo sio majiji wala manispaa, mtumishi mwenye degree stahiki yake ni 80,000 kwa siku.

Ni vema ukaomba upewe waraka wa posho za kujikimu kuliko kulaumu watu kuwa wamekula hela zenu tu.

Kazi yenyewe hujaanza tayari ushakuwa mtovu wa nidham hivyo.
Lakini pia, Halmashauri ya wilaya Lushoto, ambayo imewaonyesha walimu wa degree, document iliyoandikwa 100,000 kwa siku, je hao wana waraka wao? Tupe waraka wa mwaka huu unaoonyesha malipo ni kama hayo uliyoyataja.

Kiufupi wapigadili wanapiga dili, na ndio maana unaona kuna halamashauri kama Uvinza na Kibondo na nyingine ya mkoa wa Mara, wao wamelipa walimu wenye degree elfu 60,000 tu kwa siku, ambayo ni kinyume na hata hayo maneno yako ya utetezi kwao.
 
Kama halmashauri ya wilaya ya Missenyi wakitaka kutupa pesa pungufu, nitampiga picha yule afisa aliyeonyesha nia ya kubugia pesa zetu tangu mapema, kisha nimuweke humu mumuone mwizi wetu. Kwakweli wezi siwapendi kabisa:(
 
Poleni sana. Nanyi mliibiwa na hao wapigadili. Na sasa hao wapigadili wanahisi kasi ya upepo bado ni ile ile, hivyo wameendelea kuiba kama kawaida yao. Sijui wanapima kina cha maji, au walishayaona kama yanakina kifupi. Tusubiri tuone hatma ya mazoea yao ya wizi.
Nauli kila siku tunaambiwa andikeni barua ya madai ya nauli wakati tiketi wanazo huko kwao, yaani hayo mauzauza ndio mnayaanza kuyapata maana kuna miungu watu wanakula bata tu
 
Nauli kila siku tunaambiwa andikeni barua ya madai ya nauli wakati tiketi wanazo huko kwao, yaani hayo mauzauza ndio mnayaanza kuyapata maana kuna miungu watu wanakula bata tu
Kumbe kuna haja ya kutoa kopi tiketi, ili wakizingua tu, mtu unapeleka kopi.
 
Back
Top Bottom