Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Bashungwa ajiuzulu mara moja

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
7,195
Reaction score
9,812
Nakumbuka miaka 1970s hapa Tanzania kulitokeza matukio yalosababisha mauaji ya mamia ya Watz wasio na hatia kwa madai kuwa ati walikuwa ni waganga wa kienyeji, wachawi na majambazi!

Lawama za mauaji hayo zilielekezwa kwa Jeshi la Polisi wakti huo Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi chini ya Rais Mwl.J.K. Nyerere.

Kutokana na tuhuma hizo kwa Jeshi la Polisi, Marehemu Mwinyi alimwandikia Rais barua ya kujiuzulu na Rais akamkubalia. Mzee Mwinyi hakuwa ameua raia hata mmoja, lakini kwa vile Polisi ndo walihusika Mwinyi akaachia ngazi kwa kuwajibika na baadae mwaka 1985 akateuliwa kuwa Mgombea wa Urais na akachaguliwa.

Kwa sasa Jeshi la Polisi lina laumiwa kila kona kutokana na matukio ya utekaji, utesaji, upotezaji na mauaji kwa raia wasio na hatia. Eti kosa lao ni kuwa Wapinzani tu. Huu ni wakti wa Mhe. Bashungwa, Waziri wa Mambo ya Ndani kujiuzulu kwa tuhuma na lawama hizi. Hii itaonesha kuwajibika kwake na Serikali yake ya CCM. Vinginevo wananchi wenye hasira watamu wajibisha.
 
Hawa wa sasa hivi ni wahuni tu na dawa yao ni kushughulikiwa na Jeshi la Polisi. Hapo sasa anajiuzulu kwa lipi?
 
Anatakiwa kujiuzulu kwa kuwajibika maana Mapolisi wako chini yake. Asipojiuzulu atashughulikiwa na nguvu ya umma.
 
Siku hizi wanabadilishwa wizara! Katika utawala wa Maza ambaye angekuwa wa kwanza kujiuzuru angekuwa mzanzibar mwenzake Hamad Masauni! Bashungwa ameangushiwa jumba bovu tu.
 
Back
Top Bottom