Waziri wa Fedha Punguza Jazba

Waziri wa Fedha Punguza Jazba

Sisi tusio na elimu ya uchumi hatujui lolote zaidi ya kutambua kwamba huku mtaani hela hakuna, na tatizo siyo tu hakuna hela bali hata ukiipata thamani yake imeshuka hivo haikidhi mahitaji!

Gharama za maisha zimekuwa kubwa sana na kama Waziri Mpango anaona hao TRA wa bandarini ndiyo tatizo, basi awafukuze na yeye mwenyewe aige tabia ya yule bwana awe ndiyo mkuu wa kila kitu hapo bandarini!
 
Wizi wakuporwa pesa unataka kusema umeanza kipindi cha utawala huu?

Mimi navyoona utawala huu umedhibiti sana uporaji wa pesa kuliko tawala zilizopita,inatakiwa kusema ukweli kwenye ukweli sio kupotosha na unapotosha ili iweje? Na kwanini unamasisha importation badala ya exportation?

Na ukisema sijui pesa zimeamishiwa BANK kuu siwatetei serikali ila waliamisha kwasababu na kuna advantage kubwa kuliko disadvantage.

Na unajua BANK kuu wameshusha viwango cha Riba ivi karibuni? Labda nachotaka kuwa sisitizia BANK kuu wawe wafuatiliaji wa viwango vya riba kwa mabank ya biashara ili ziwafikie wafanyabiashara wadogo.
Mkuu kweli serikali imethibiti kwa kiasi kikubwa matumizi na wizi wa Fedha za serikali. Pili naipongeza sana serikali kwa kuangalia upya mikataba ya madini. Tatizo lipo kwenye serikali kuona kila mfanyabiashara ni mkwepa kodi, serikali kuu kupokonya serikali za mitaa vyanzo vya mapato nayo imesababisha ukata mkubwa kwenye halmashauri na majiji. Serikali kutoa fedha kwenye mabenki na kupeleka benki kuu, wakandarasi wengi kukosa tenda za ujenzi kwasasa sehemu Kubwa za tenda za ujenzi wa miradi ya serikali inafanywa na Suma JKT, mfano wa ujenzi wa Ukuta wa Mererani.
Serikali inatakiwa kuwa karibu na wafanyabiashara na kuwa na mazungumzo ya kila mara.
Wafanyabiashara ni nguzo muhimu kwa ujenzi wa uchumi imara. Serikali ya awamu ya 3 ilifanikiwa sana katika kukuza uchumi wa Tanzania
 
Ulitaka asemeje kwa mfano?
Wale si wapo chini ya wizara yake?
Kinachopigiwa kelele ni urasimu
wa watendaji wa TRA. Wafanya biashara
ukiwazingua wanakimbilia bandari za nchi jirani.
Na wewe unabaki na watu wanaohitaji mshahara
bila kukusanya kodi

Kwa nini asifoke?
Basi mdau, keshafoka tutulie. Tukae chini tuangalie grafu inavyopanda. Hata yule wa Mamlaka ya anga kumbe angefoka tu
 
Hivi kila cku unamkamua ng'ombe maziwa ilhali humpi majani hayo maziwa atayatoa wapi!
 
Kadri siku zinavyokwenda yanazidi kushuka si wanataka watu waishi kama mashetani. Mashirika yakipunguza wafanyakazi wao wanakenua meno wanafurahia wanajua tunanyooka, makampuni yakifunga kampuni zao na wafanyabiashara wakifunga biashara zao wanafurahia wanajua wanatunyoosha. Wanasahau kua mapato yanapungua maana hata PAYE zinapungua pamoja na kodi mbalimbali

Hakuna nchi duniani unaweza kusema 100% hakuna Ufisadi. Kitu kikubwa ni kupunguza Ufisadi, mpe uhuru mfanyakazi kazi wa TRA katika kufanya kazi yake mwekee kiwango cha ukusanyaji mapato bila kumtisha wala kumwingilia kikazi. Neno KUTAIFISHA waache kabisa ukikuta mfanyabiashara amedanganya apigwe faini kazi iendelee. How comes mtu ameleta gari kwa kudangaya kuwa ni mitumba unataifisha kwanini usimpige faini ukampa gari lake, unadai kampuni imekwepa ushuru wa billioni moja kwenye Almasi Kwa uzembe wa watumishi wetu halafu unataifisha Almasi ya bilioni 64.
Wafanyabiashara siku zote huwa wanaleta mizigo kwa kujaribu kutafuta faida sio hasara. Mtu alipe kodi bandarini halafu wakati akiuuza awe na mashine, huko bandarini analipa VAT akiuuza analipa VAT akidai VAT kutoka TRA harudishwi.

wale jamaa wameendekeza sana urasimu na umangimeza...nilishangaa Masamaki alishindaje kesi.

Waziri Mpango haukuwa serious ktk kukusanya mapato; ulipaswa kuflash wapokea rushwa wote TRA na kuweka vijana wapya mpaka watu wa usalama.

Watu waliokuwa kwenye payroll ya home shopping mpk leo wamejaa ofisi zote za TRA na home shopping anaendelea na kazi zake km kawaida, unategemea mapato kweli? Hapo bado kampuni nyingne zenye kutumia mbinu za home shopping... ulitakiwa ufanye complete overhaul

na njia ni ndogo tuu, anzia na mali wanazomiliki compare na gross salary zao za 1,800,000...angalia biashara zao na source ya mitaji yao!!

Hao TRA Police n.k wameshakula nyama ya mtu hawawezi acha, fukuza wote tuingie nasisi tuitumikie nchi

Kwa kauli ya jana ya waziri wa Fedha inatoa picha hii...
1/Makusanyo ya TRA yameshuka sana japokuwa wanajaribu kuficha ukweli huo.

2/Mapato ya bandari yamepungua sana baada ya kupungua kwa watumiaji wa bandari.

3/Bandari ndio nguzo kuu pekee ya uhakika ya mapato ya serikali ya sasa.(Ndio eneo limekuwa na Ziara nyingi za kushtukiza za viongozi wa juu wa serikali ya awamu ya tano)

4/Hali ya kichumi sio nzuri, serikali haina majibu kilichobakia na kila mtu kumtupia mpira mwenzake ili kukwepa lawama.
 
Huo ushauri wape waume zako hapo ufipa .

Waambie wajenge ofisi ya chama
povu la nini? Zikishajengwa ofisi za Ufipa ndio mizigo itaongezeka bandarini? I wish ifungwe tu hiyo bandari ndio mjua sio kila kitu ni ubabe
 
Sasa bosi kasema alikuwa anatia tu hakuwa serious nao wakamsukumia. Ina maana mambo yote anayofanya ni hovyo kwa sababu hakuwa seious. Mliompa mlifanya serious au nanyi mlikuwa mnatania? Matokeo ndio hayo. Ukichagua nyuki utaambulia asali na sio vinginevyo, bali ukichagua nzi hutaambulia asali mpaka ufe.

Waziri analialia na matokeo badala ya chanzo. Wajanja huanzia kupata ufumbuzi toka kwenye chanzo.
Waziri anaingia biashara wakati hana historia ya kuuza nata karanga.
Waziri anatumia hisia ktika ulimwengu wa binadam. Ameshau hisia wanatumia wanyama tu, binadam hutumia kwa kuchagua tu. Bila shaka amechagua fungu bovu.

Matokeo yake sii la kufikiri. Bali ni dhahiri, ndio hiyo .... downfall!
 
Mkuu hizo gross za 1,800,000 wanalipwa watu wa customs au?
wingi wao kasoro hawa vijana wa juzi juzi hapa nahisi it's around 1.4 ..TRA ni taasisi ya maajabu nayo isingekuwa hizo rushuwa maisha yao yangekuwa ya ajabu sana...It's only TRA leo wanaweza ajiri watu wa kada flan wakawalipa 1.5M, mwaka unaofwatia kada hiyo hiyo wanaajiri na kulipa 700,000 only Tanzania

TRA sawa na CHAD EMA
 
Back
Top Bottom